Search This Blog

Thursday, October 28, 2010

Utachagua Kiongozi kwa UTASHI? , UFUASI?, AU UHITAJI?

Umeshajiuliza utamchagua (ama kwa wasio nchini ungemchagua) nani kati ya waonekanao hapo juu kuwa President  waJamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika jumapili?
Hapa 
sisemi kuchagua kutokana na jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Ama ulishajiuliza kuwa unataka Kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi? Ama tulisubiri waje na UONGO WAO ndio tuanze kujipanga jinsi ya kukubaliana nao? 

Ama tulisubiri waje na pesa ndio tuangalie namna zinavyoweza kutufaa?Tulisubiri waje kutuambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwetu?Ama waje na takwimu njema zisizoeleza tulivyo na kisha kutuaminisha kuwa tunawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yetu?
Je!! Ulibahatika kumuuliza yeyote maswali haya?
OMBI LA KWANZA LA BLOGU HII KWA MWANANCHI NI KWENDA KUPIGA KURA. NI HAKI YAKO NA "SAUTI" YAKO KATIKA YALE YAJAYO.

Na japo siku zimekaribia, bado nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
TUNACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

No comments:

Post a Comment