Mabadiriko ya hali ya hewa yanatokea kila siku za maisha yetu. Kiwango cha joto kimeongezeka toka 0.6 – 1.0 oC. Maeneo mengine ya Africa joto limepanda hadi 4.0 oC. mwaka 2100 kama hali hii isipodhibitiwa joto litafika hadi 6.3 oC.
CHANGAMOTO ZA KIDUNIA ni kama Ujenzi wa viwanda, Shughuli za kilimo, Shughuli za mawasiliano, Matumizi ya rasilimali (forestry) na Ukuaji wa miji.
Matumizi ya ardhi yamesababisha kutokuwepo kwa uwiano safi wa ukuaji wa viumbe hai na uzalishaji. Uzalishaji wa gesi zitokanazo na matumizi mbalimbali ya shughuli za binadamu.
VISABABISHI VYA UHARIBIFU WA ARDHI ni kama: Ukataji miti ovyo kwa ajili ya shughuli za kilimo, mafuriko, ukataji wa miti ya kuni na mbao, Utengenezaji wa mkaa, madini, makazi, Ufugaji holela na mioto na Maendeleo ya viwanda
MADHARA YA UHARIBIFU ni Ukosefu wa miti ya kuni, Upungufu wa mazao ya miti, Ongezeko la uchafu maji, Mafuriko, Kukauka kwa vyanzo vya maji, Ongezeko la magonjwa yatokanayo na maji- water-borne diseases;Ukosefu wa viumbehai.
UFUMBUZI UNAOWEZEKANA ni Hifadhi ya ngitiri,Upandaji wa miti katika vyanzo vya maji, Upandaji wa miti katika maeneo ya wazi,Kilimomseto, Hifadhi ya ardhi na maji na Kilimo hai.
UTATUZI WA SASA NI: Kushiriki pamoja kutunza na kuhifadhi rasilimali asilia, Hifadhi ya Viumbe hai, Hifadhi ya vyanzo vya maji, Hifadhi ya mazingira na mipango miji na Upandaji na utunzaji wa miti.
NAWAKILISHAAAAA.
No comments:
Post a Comment