Search This Blog

Wednesday, October 13, 2010

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA UFISADI HII HAPA.


  • Ufisadi - tatizo sugu na hatari linalodidimiza maendeleo ya Afrika kumbe linaweza kupunguzwa kwa kutumia njia rahisi tu. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonyesha kwambaserikali zenye wanawake wengi madarakani (mf. Wabunge, Mawaziri) zina viwango vidogo vya ufisadi ukilinganisha na zile zilizosheheni wanaumeRwanda - nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuwa na wanawake wengi bungeni na serikalini inatajwa sana kuwa mfano wa kuvutia kuhusu suala hili. Ni kwa sababu hii kujitokeza kwa wanawake wengi kugombea ubunge na uwakilishi kule Haiti katika uchaguzi wa mwaka huu kumeleta matumaini makubwa kwamba pengine ufisadi utapungua.
  • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume, wana moyo wa kujinyima, wanaaminika zaidi na ni wepesi wa kuona na kukiri makosa na hatimaye kuomba msamaha. Pengine ni kutokana na sababu hizi wanawake pia wana uwezekano mdogo wa kuiba mamilioni ya pesa za umma na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka (wengi wao wanawake wenzao; na watoto). 
  • Serikali zenye wanawake wengi madarakani pia zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza sera imara zenye kumakinikia sekta za afya na elimu ya watoto, usawa kwa wanajamii wote na kuendeleza uchumi imara.

No comments:

Post a Comment