Search This Blog

Tuesday, October 5, 2010

NI TAIFA STAR? AU MOROCO?



Kwa mara nyingine tena Tanzania tunakuwa na mchezo wa Stars na Moroco utakaochezwa Jumamosi ijayo kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2012 nchini Guinea. Viingilio viivyotangazwa katika mpambano wa kuwania kufuzu kushiriki fainali za Mataifa ya Afrika(AFCON) ni pamoja na kile cha Sh 5,000 ambacho ni cha chini kabisa wakati kile cha juu ni Sh30,000.

Akitangaza viingilio hivyo,Afisa habari wa TFF Frolian Kaijage alisema kuwa kiingilio cha Sh 5,000 ni kwa wale watakaokaa jukwaa la kijani wakati kile cha Sh 30,000 ni kwaajili ya jukwaa maalum (VIP A).

Kaijage alivitaja viingilio vingine kuwa ni Sh 7,000 kwa Jukwaa la Rangi ya Bluu,Sh10,000 kwa jukwaa la rangi ya machungwa wakati VIP C kiingilio kitakuwa Sh 15,000 na Sh 20,000 kwa jukwaa la VIP B.

Waamuzi wa mpambano ambao wote wanatoka Mauritius wanatarajia kuwasili nchini kesho sambamba na kamisaa wa mchezo anayetoka Kenya. Majina yao  ni Sochurn Raji atakayekuwa mwamuzi wa kati wakati Bootun Balkrishina na Bally Vivian wakiwa ni wasaidizi na kamishaa Muhammad Imterazi.


1 comment:

  1. i like your blog....and you knwow what? taifa stars will beatup..just wait and seee and then you remember me my tshirt you promised last year with my name at the back..........taifa stars twawapa shavu kwa sana huku rock city.......you notoriou seems to grow higher and higher.......kick the ball and get more scoars.....tchaaaaaoooooooooooooooo mr price

    ReplyDelete