Ni Mdahalo wa Wagombea UBUNGE WILAYA YA ILEMELA jana tarehe 25 KITWIMA HOTEL MWANZA cha kushangaza ni Mgombea mmoja tu wa CHADEMA HAILE SAMSON ndiye aliyejitokeza katika mdahalo huo hivyo kupata muda wa kutosha kujitanua kumwaga sera za chama kwa wananchi na kujibu maswali. Wagombea wengine waliingia mitini.
Maswali yakiulizwa.
ALIPOPEWA FURSA YA KUJINADI NA KUOMBA KURA MGOMBEA HUYO WA UBUNGE ILEMELA ALISEMA "VYAMA VINAPITA LAKINI TANZANIA INABAKI PALEPALE, TUSICHAGUE VYAMA TUCHAGUE MTU. HATUNA TATIZO LA RASLIMALI, TATIZO TULILONALO NI VIONGOZI KUKIUKA MAADILI NA KUWA NA VIONGOZI MAFISADI" "MIAKA INAENDA MIAKA INARUDI MATATIZO YAKO PALE PALE, NA KILA KUKICHA NDIYO HAYO HAYO YANAYOZUNGUMZWA IWE NI MAJI, MIUNDO MBINU, MIGOGORO YA ARDHI, YOTE HAYA HAYAHITAJI DIPLOMA WALA DEGREE KUYATATUA, NI UMAKINI, UTASHI NA DHAMIRA THABITI YA KIUONGOZI"
No comments:
Post a Comment