Search This Blog

Tuesday, May 3, 2011

OSAMA AUAWA

Osama bin Laden Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden, ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema. Kiongozi huyo wa al Qaeda aliuwawa baada ya makabiliano na wanajeshi wa Marekani nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi. Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani yaliuchukua mwili wake. Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001. Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al Qaeda lakini kuna hofu kuwa huenda kukatokea mashambulio ya kulipiza kisasi. Msako Bw Obama amesema taarifa za mahali alikojificha zilianza kupatikana Agosti mwaka jana. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan. Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa shughuli ya ''kumsaka bin Laden'' kufanyika. Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, kaskazini mwa Islamabad. ''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. KUNRADHI kwa picha hiyo hapo chini.


Osama baada ya kipigo:
WASIFU WA OSAMA BIN LADENOsama bin Laden alizaliwa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia Ana zaidi ya ndugu na dada 50. Babayake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa amevalia mavazi ya kifahari na ya gharama kubwa, akiwa likizo katika miji mbali mbali barani Ulaya. Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themanini alitapa mgongo maisha haya ya kifahari na kitajiri na kujiunga na vuguvugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa Kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan. Wakati huo, akipigana pamoja na Waarabu wenzake, alizindua kundi la kigaidi la Al Qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Osama alisema alikasirishwa na hatua ya Marekani kuweka majeshi yake katika ardhi ya Kiislamu, katika nchi mbalimbali Mashariki ya Kati. Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama Bin Laden anaaminika kuwa na watoto 17.


No comments:

Post a Comment