Search This Blog

Friday, May 6, 2011

UFISADI WA RIDHIWANI KIKWETE, DR SLAA NINAMUAMINIA!!


Sakata linalomhusu Ridhiwani Kikwete,mtoto wa Mhe. Jakaya Kikwete-kwa upande mmoja,na Katibu Mkuu wa Chadema Dkt Willibroad Slaa na Mwenyekiti wa chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila-kwa upande mwingine, lina ukweli ndani yake. Ndani ya siku saba zilizotolewa na Ridhiwani kwa Dr. Slaa na Mtikila ili wakanushe lakini ebu tuangalie mazingira ya hili sakata yamekaaje.
Ridhiwani ni mwanasheria kitaaluma,pia  ni mtoto wa Mhe. Kikwete,kwa maana nyingine ufisadi huu unamhusisha pia baba yake (kwa maana ya kutumia fursa ya urais kumnufaisha mwanaye) inatarajiwa kuwa suala hapa sio kujisafisha yeye tu bali pia baba yake. Lakini kwa kuwa Dr. Slaa ni makini haya mazingira ni mepesi sana kwake kuyashughulikia.

Dokta Slaa,wengi tunamfahamu kama mmoja wa wanasiasa adimu kabisa ambao ni nadra kutoa matamshi pasipo kuyafanyia utafiti wa kutosha na kuwa na uthibitisho. Dr. Slaa hayumbishwi na nafasi ya mtu katika chama na serikali hasa linapojitokeza suala la uwajibikaji. Na pengine Mchungaji Mtikila, wengi tunafahamu kuwa Mtikila na mahakama ni kama mtu na nyumbani kwake na bado anatambulika kuwa anapoamua kupigania haki basi atakwenda umbali wowote ule pasipo kuchelea madhara ya kufanya hivyo.

Jumatatu ndo tutajua ukweli maana kama ni  kweli ufisadi wa Ridhiwani ukithibitika basi ni pesa zetu ndo ametafuna na kujinufaisha yeye na familia yake.
Aluta kontinua!!!!!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment