Search This Blog

Saturday, October 30, 2010

KESHO TUFANYE UAMUZI MAKINI KWA UJASIRI.

SHUGHULI KUBWA NI KUPIGA KURA KUWACHAGUA RAIS, WABUNGE, NA MADIWANI. Hivyo tujitokeze kwa wingi kuwachagua wawakilishi hawa. Baada ya kupiga tu kura rudi nyumbani ukaendelee na shughuli zingine za ujenzi wa Taifa. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
TUKAPIGE KURA


TUNAOMBA HAYA YASITOKEE KABISA.............
............KUGOMBANIA KADI YA MPIGA KURA PALE INAPOFICHWA AU KUUZWA.
KUWALAZIMISHA WANAWAKE WAMPIGIE KURA MGOMBEA WASIYEMTAKA. Hapo ndo utasikia.............weee mama naniii kwa nini hutaki kumpigia kura yule mgombea?? Utanikoma leo.

LAKINI WADAU WANGU MIMI NINAWAAMBIA KWAMBA....KURA YAKO NI YA THAMANI KWA KIZAZI HIKI KINACHOHITAJI MABADIRIKO YA KIUCHUMI.

Your VOTE is your FUTURE


BREAKING NEWS !!!! SUPER COACH MZIRAI KATUTOKA!!!!

HABARI ZIMEINGIA ASUBUHI HII ZINASEMA SUPER COACH SYLLESAID MZIRAY AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO KATIKA HOSPITALI YA AGA KHAN JIJINI DAR ALIKOKUWA AMELAZWA AKISUMBULIWA N MALARIA. HABARI ZA MIPANGO YA MAZISHI ZITAFUATA MARA TU BAADA YA KUPATIKANA.


COACH MZIRAY , ALIYEKUWA MWAJIRIWA WA CHUO KIKUUU HURIA KAMA MHADHIRI, ATAKUMBUKWA KWA UMAHIRI KATIKA UFUNDISHAJI SOKA KATIKA VILABU MBALIMBALI HADI TIMU YA TAIFA ILIYOSHINDA UBINGWA WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI. ALIFUNDISHA PIA PILSNER, SIMBA, YANGA, PAN AFRICAN NA KABLA YA MAUTI KUMKUTA ALIKUWA MWALIMU WA VIUNGO NA SAIKOLOJIA WA KLABU YA SIMBA.
GLOBU YA BMUKAMA INAUNGANA NA WATANZANIA WOTE KUOMBOLEZA MSIBA HUU MZITO AMBAO NI PIGO KWA TASNIA YA MICHEZO NCHINI UKIZINGATIA TUNA MAKOCHA WACHACHE WALIOSOMEA FANI HIYO NA KUBOBEA.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU
MAHALA PEMA PEPONI
- AMIN

Thursday, October 28, 2010

Utachagua Kiongozi kwa UTASHI? , UFUASI?, AU UHITAJI?

Umeshajiuliza utamchagua (ama kwa wasio nchini ungemchagua) nani kati ya waonekanao hapo juu kuwa President  waJamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika jumapili?
Hapa 
sisemi kuchagua kutokana na jina ama chama, namaanisha SIFA za mgombea.
Ama ulishajiuliza kuwa unataka Kiongozi ajaye awe na utekelezaji wa lipi na lipi na awe na ILANI inayotekeleza vipi? Ama tulisubiri waje na UONGO WAO ndio tuanze kujipanga jinsi ya kukubaliana nao? 

Ama tulisubiri waje na pesa ndio tuangalie namna zinavyoweza kutufaa?Tulisubiri waje kutuambia matatizo yetu ilhali wao hawakai kwetu?Ama waje na takwimu njema zisizoeleza tulivyo na kisha kutuaminisha kuwa tunawahitaji wao badala ya kuhitaji suluhisho la matatizo yetu?
Je!! Ulibahatika kumuuliza yeyote maswali haya?
OMBI LA KWANZA LA BLOGU HII KWA MWANANCHI NI KWENDA KUPIGA KURA. NI HAKI YAKO NA "SAUTI" YAKO KATIKA YALE YAJAYO.

Na japo siku zimekaribia, bado nahisi wengi hawana majibu na hili lanipeleka kujiuliza kama
TUNACHAGUA VIONGOZI WETU KWA UTASHI AMA UHITAJI?

Tuesday, October 26, 2010

WAANGALIZI WA UCHANGUZI WAPO NCHINI TAYARI

Tayari waangalizi wa Kimataifa wapo nchini wanafuatilia mchakato wa uchaguzi wa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani. Katika harakati hizi za kampeni tunategemea Waangalizi hawa watafuatilia kwa makini mwenendo mzima wa zoezi la uchaguzi mkuu 2010. Hapa ni leo jijini Mwanza wakati Mgombea wa CCM alipowasili kunadi sera za chama cha CCM viwanja vya Sahara jimbo la Nyamagana.

MDAHALO JIMBO LA ILEMELA...WENGINE WAKIMBIA!!!

Ni Mdahalo wa Wagombea  UBUNGE WILAYA YA ILEMELA jana tarehe 25 KITWIMA HOTEL MWANZA cha kushangaza ni Mgombea mmoja tu  wa CHADEMA HAILE SAMSON ndiye aliyejitokeza katika mdahalo huo hivyo kupata muda wa kutosha kujitanua  kumwaga sera za chama kwa wananchi na kujibu maswali. Wagombea wengine waliingia mitini.
Maswali yakiulizwa.
ALIPOPEWA FURSA YA KUJINADI NA KUOMBA KURA MGOMBEA HUYO WA UBUNGE ILEMELA ALISEMA "VYAMA VINAPITA LAKINI TANZANIA INABAKI PALEPALE, TUSICHAGUE VYAMA TUCHAGUE MTU. HATUNA TATIZO LA RASLIMALI, TATIZO TULILONALO NI VIONGOZI KUKIUKA MAADILI NA KUWA NA VIONGOZI MAFISADI" "MIAKA INAENDA MIAKA INARUDI MATATIZO YAKO PALE PALE, NA KILA KUKICHA NDIYO HAYO HAYO YANAYOZUNGUMZWA IWE NI MAJI, MIUNDO MBINU, MIGOGORO YA ARDHI, YOTE HAYA HAYAHITAJI DIPLOMA WALA DEGREE KUYATATUA, NI UMAKINI, UTASHI NA DHAMIRA THABITI YA KIUONGOZI" 


MBINU ZA KUTUMIA MTU MWINGINE ASIJUE PASSWORD YAKO

Keyboard na kiganja cha mikono vinafunikwa na kitambaa au mfuko.
Ukiona bado kuna mtu anakupiga chabo basi keyboard, kiganja na screen vyote funika kwa kitambaa.
Hii ndo komesha....FULL KUJIFUNGIA


mis TANZANIA 2010 mbona simuoni????

Hapa ni katika bichi la Sanya na washiriki wakipozi vibikini vyao mtoto wetu (Miss TZ 2010) sikumuona katika lukuki ya picha zilizotumwa.Contestants of Miss World 2010, the 60th Miss World pageant, pose for photos on the Yalong beach in Sanya, south China's Hainan Province, Oct. 25, 2010. A total of 120 competitors from around the world would take part in the 60th Miss World in Sanya this Saturday.

Ray akamilisha Pretty Girl sasa tayari kuitupa Sokoni



Mohamed Mwikongi na Vicent Kigosi wote walishakutana pia katika filamu ya Shakira kama ndugu wa mama mmoja waliopotezana ambao wanamuoa mke mmoja kwa vipindi tofauti na mwanamke mwenyewe alikuwa Irene Uwoya.



Wanaonekana tena katika kava ya Pretty Girl yenye kibwagizo not my fault mhh nyie haya nyie.

Monday, October 25, 2010

KATUNI YA LEO

KISWAHILI

Bango likiwa na ujumbe unaosomeka "SISI SOTE TUPIGANISHE UBAKAJI" Sina hakika kama neno TUPIGANISHE ni sahihi hapo, najaribu kujiuliza alikuwa anamaanisha awachukuwe wabakaji alafu awapiganishe au???  Hapana bado haiingii akilini...Nafikiri angeweka neno TUPINGE labda lingeleta maana zaidi. BAKITA Mpoooooo!!!

USHABIKI HUANZA UTOTONI

Mmmmmh hapa nahisi wazazi ndio mashabiki na sio hao watoto.....Lakini waswahili wanasema mto umleavyo ndivyo .................

BREAKING NEWS !!!! GREGORY ISACK DIED IN LONDON

Reggae legend Gregory Isaacs died Monday morning after a battle with cancer.
Isaacs, who was 59 years old, died on Monday morning at his home in London where he spent part of his time.
He was surrounded by three of his eleven children and his wife Linda Isaacs who told BBC Caribbean that he passed away peacefully.
Neil Nunes of BBC Caribbean interviewed Gregory Isaac's wife, Linda, on her husband's passing.

R.I.P

Sunday, October 24, 2010

HAKIKI KAMA UTAPIGA KURA



Wadau wangu wote,

TIII KURA YAKO kwa kumchagua mgombea anayestahili

Ukiingia kwenye website ya NEC na kuweka nambari ya mpiga kura utaweza ona online status yako (mpiga kura) na kituo chako cha kupigia kura. Taarifa wanazozitoa ni sahihi kwa asilimia 100. Wadau wote tutizame status zetu ili kuepukana na disappointments za dakika za mwisho.

Hii itazidi kutupa uhakika wa kupiga kura zetu sahihi siku hiyo ya tarehe 31 Oct 2010.

Hongereni NEC kwa kuweza kufanikisha hili.

Link ya kufuata ni hii…

http://www.nec.go.tz/?modules=gallery⊂

CCM NA BIASHARA ZAKE ZINAMSAIDIAJE MWANANCHI MASKINI?

Maji ya kunywa ya chupa ya  CCM



Wakati hali halisi ya upatikanaji wa maji maeneo mengi nchini iko hivi. 
Kwa nini CCM wasijenge visima vizuri vinavyotoa maji safi na salama ambavyo vitawasaidia wananchi wengi masikini kuliko kutengeneza maji ya chupa ambayo wananchi wengi hawawezi kumudu kuyanunua??. Maana kulingana na hali ya umasikini ilivyo sidhani watanzania wengi wataweza kununua maji ya chupa wakati hali yao ya kipato ni duni.


HEBU CHECK HAPA CHINI
Raba bomba kichizi ya Rebo ya CCM (watengenezaji) kwa bei ya kawaida ni kati ya Tsh. 60,000/ hadi 100,000/ kwa maduka mengi jijini DSM na Mwanza.


Checkshia babaaake hali halisi hapo chini  vijana walivyotinga miguuni.
Ni Vijana wangapi nchini wenye kipato cha kuweza kununua viatu hivyo vya CCM?? 
Je Miradi hii ya CCM na mingine iliyopo inawezaje kumsaidia mwananchi mwenye kipato kiduchu? Kwa nini Serikali ya CCM isiwe na mipango yenye manufaa kwa jamii kuliko kuwa na mipango ya kuwanufaisha wachache?????Mafisadi??
KURA YAKO TAREHE 31/10/2010 Itaweza kuleta mabadiliko makubwa ya hali ya uchumi katika jamii na kuboresha huduma muhimu za jamii. 

NAWAKILISHA



SERIKALI INATAKA MAGAZETI YAANDIKE HIVI?

Serikali imekuwa ikiingilia vyombo vya habari kwa kuwapiga mikwara kibao ya kutishia kufungwa kwa baadhi ya magazeti!! Je wanataka sasa magazeti yaandike hivyo (kama linavyoonekana hapo juu) bila kugusia changamoto zinazoikabili jamii ili lisifungiwe????

..MSINISEMEEE KAMA MIMI NAPENDA KULA..

EXTRAORDINARY U-TURN

Wayne Rooney has made a shock U-turn and agreed a new five-year contract at Manchester United just two days after announcing his intention to leave.
On Wednesday, the 24-year-old striker said concerns over the strength of the club's squad were behind his original decision not to sign a new deal.
United boss Sir Alex Ferguson said: "I'm delighted Wayne's agreed to stay." 

Saturday, October 23, 2010

Friday, October 22, 2010

HII HESHIMA ILIKUWA WAPI SIKU ZOTE?????? KWA NINI KIPINDI HIKI???

Mhe. Shukuru Kawambwa akiomba kura kwa Wananchi huku akiwa amepiga magoti. Swali la kujiuliza ni ...Je siku zote huwa anapiga magoti katika shughuli mbalimbali za jamii. Mbona alipokuwa akiwakilisha bajeti bungeni hakuwahi kuonekana akipiga magoti kuomba bajeti ya wizara ipite?????? Jamani !!!!!!!!! Je ni kawaida yake??? Kwa nini hadi apige magoti kipindi hiki cha uchaguzi????  mwanamme mzima...*****????  Mmmmmmh!


HEBU CHEKI PANDE HIYO HAPO CHINI............KAMANDA ANAKOMAA TU KIAINA HAKUNA CHA KUPIGA MAGOTI.
Mhe. Zitto Kabwe akiomba kura kwa Wananchi.  

NOTE: Nadhani kinachotakiwa ni SERA tu siyo kupiga Magoti . Jamii iwe makini na wanaotafuta nafasi za Uwakilishi kwa njia zisizozoeleka katika jamii kama kupiga magoti na kulia.

Thursday, October 21, 2010

MAJI YAMEWAFIKA SHINGONI!!!!! HATUDANGANYIKI

Maelezo yanajieleza. Ukishindwa hoja unatumia vitisho. sERIKALI IMEANZA VITISHO KWA WANAHABARI, lakini Sisi tunasema HATUDANGANYIKI

MWISHO MWAMPAMBA AREJEA DAR

Mwisho Mwampamba akipokea shada la maua kutoka kwa ndugu zake mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jana jioni akitokea Afrika kusini kwa ndege ya shirika la ndege la SAA ambako alishiriki shindano la BBA 2010 All Stars na kushika nafasi ya 4 huku mshiriki Uti kutoka Nigeria akijinyakulia kitita cha Dola laki mbili za Kimarekani.
Mwisho kesho anatarajiwa kutembelea vyombo mbalimbali vya habari na kueleza mambo mbalimbali yaliyojiri kwa muda wote wa miezi mitatu walipokuwa kwenye jumba la Bigbrother na washiriki wenzake na keshokutwa atazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika picha kushoto ni baba yake mzee Mwampamba.

DR. SLAA ATIKISA KWA KISHINDO JIJI LA MWANZA

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Magomeni, Kirumba jana jioni .
Umati huu wa watu ulifurika kusikiliza sera mathubuti za mgombea huyo licha ya kupigwa virungu na Polisi.
Pamoja na Virungu na maji yanayowasha waliyomwagiwa wananchi lakini hebu check umati ulifurika. Hadi kwenye paa la choo wananchi walipanda kumsikiliza Mgombea wa Chadema, Dr. Slaa
Wakati mwingine hata kama ni nguzo ina ncha kali wananchi wenye uchu wa kusilikilza INAWEZEKANA.
Pipoooooooz!!!!!!! Pawaaaaaaaaa!!!!!!



Sunday, October 17, 2010

UKIONA MAMBO NI MAGUMU...JISALIMISHE TUUUUU!!!!

Huu ndio ujasiri, na demokrasia. Jamaa ilibidi apige salute kwa John Mnyika - Mgombea Ubunge Jimbo la Ubungo wakati wa kampeini. Ni uamuzi binafsi na sahihi hasa pale unapoona ni kiongozi gani anafaa kwa kizazi hiki cha sasa. October 31 KURA yako toa kwa KIONGOZI unayeona anafaa kuleta maendeleo endelevu kwa maslahi ya Taifa. Taifa hujengwa na viongozi IMARA, WAADILIFU,wazalendo  wanaofanya kazi kwa ajili ya jamii inayohitaji utawala bora.