Search This Blog

Wednesday, November 10, 2010

MAPINDUZI MAKUBWA CCM HAYA HAPA......SITTA, CHENGE NJE USPIKA

ANNA MAKINDA

ANNA ABDALAH

KATE KAMBA
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.

Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.

SITTA USO KWA USO NA CHENGE
SIKU ZOTE WANGEKUWA HIVI.....TUSINGEYASIKIA YA UNAFIKI.


No comments:

Post a Comment