Spika anayemaliza muda wake Mhe. Samuel Sitta amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.
Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha jana baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.
kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.
Wagombea wengine waliojitokeza kugombea kiti hicho ni pamoja na Mbunge metule wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela, Mbunge Mteule wa Njombe Kusini, Anna Makinda na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tambaza, Bw. Salim Kungulilo.
No comments:
Post a Comment