Baada ya Chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni kuwa ni Mhe. Mbowe, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI- source TBC1( MUKTASARI WA HABARI).
Ukiangalia ndoa ya CUF na CCM kule Zanzibar ni vigumu sana kuamini kuwa CUF inaweza kushirikiana na Chadema kwenye kambi ya upinzani. Sikushawishika kwa mara ya kwanza niliposikia kuwa eti CUF na Chadema watashirikiana. Labda kama CUF ni mbili. Lakini ikiwa CUF ni moja siamini kuwa CUF ile ile inaweza kuwa na muungano na Chadema.
CUF vile vile kwenye Bunge la Muungano wanajiona kama wamepotea kwani wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party. Wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party kwa Chadema si CCM. Kwa hiyo CUF haiwezi kumpenda Chadema. Hata ukiangalia kwenye uchaguzi, inaelekea mikakati ya CUF na CCM ilikuwa inafanana na wameshinda wote maeneo ya pwani. Kwa hiyo baadae ukiangalia vizuri kwenye tafakari yako, CUF wanajiona kuwa hawako tofauti sana na CCM.
Hata kampeni zao unaweza kuona kuwa CUF hawakuwa against CCM kihivyo.
Jingine ni kuwa CCM wanauona wingi wa Chadema kama TISHIO kwao. Hivyo wako tayari kurefusha mkono kwa chama kingine. NCCR alikuwa ni direct ally wa CCM. Kampeni za Kawe zilithibitisha kuwa NCCR ilikuwa adui wa Chadema kuliko kuipnga CCM. Hili ni la muda kidogo. NCCR kina MPs wanne tu. Kwa hiyo CCM kumvutia CUF upande wake ni kupunguza nguvu ya upinzani kwani wabunge 45 wa Chadema ukijumlisha na 30 wa CUF, upande wa wapinzani ilikuwa inakuja na wabunge 75. Hiyo si nguvu ya kupuuza kwa CCM hivyo kwao itakuwa vizuri Chadema wakibaki peke yao.
Kwa ujumla ni kuwa katika Bunge lijalo UPINZANI itakuwa ni Chadema peke yao. Na hilo litawajenga zaidi. Hawa wengine kina UDP, TLP, NCCR na CUF obviously watahamia kwa CCM. Pepo zote za kisiasa zinaonesha hivyo.
No comments:
Post a Comment