Search This Blog

Saturday, November 6, 2010

MADAI YA DR. SLAA YASIPUUZWE HATA KIDOGO, YANA MSINGI.

Ndugu zangu wazalendo wa nchi hii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini mkubwa mwenendo wa matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo mbalimbali hususan kwa nafasi ya urais. Kwa wale wenzangu walioanza kufuatilia mapema kabisa, lazima watakuwa wameshtuka sana na namna "trend" ya matokeo ya urais ilivyobadilika ghafla. Matokeo ya awali kutoka mikoani yalianza kuonyesha tofauti ndogo ya kura kati ya Dr. Slaa na Jakaya Kikwete. Hali hiyo iliendelea kwa kipindi kirefu na kwenye baadhi ya majimbo kama Iringa, Mbeya, Moshi na Arusha Dr. Slaa alikuwa anaongoza kwa mbali kabisa. Baadaye nilishtuka nilipoambiwa kwamba matokeo ya urais yatakuwa yanatangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) na siyo wasimamizi wa uchaguzi kutoka kwenye majimbo. Kama suala la uchaguzi ni la wazi na huru, kwa nini wasimamizi wa uchaguzi wasitangaze tu matokeo ya urais sambamba na matokeo ya ubunge na udiwani. Ni nini kilichozuia????? Uhuru wa kutoa matokeo ulikuwa wapi???? Au wasimamizi wa kwenye majimbo hawakuwa na haki ya kutangaza matokeo ya uraisi????? 

Ndugu zangu ninachokiona hapa, ni kama kuna ujanja ulifanywa,  pia sisi watanzania wazalendo hatutakuwa hata mara moja kukaa kimya na kuridhika na matokeo ya urais yaliyotangazwa na NEC. Ninawaomba sana tena sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati wote nchini wafuatilie mlingano wa matokeo (yaliyoidhinishwa na mawakala wa vyama husika) kutoka kwenye majimbo na matokeo yanayotangazwa na NEC. Sina hakika kama jambo hili linaweza kuruhusiwa lakini ninaona kuwa ni jambo la msingi sana. Lazima wananchi tujiridhishe kwamba kilichotangazwa na NEC kwamba ndiyo jumla ya kura za urais kwa mgombea fulani kutoka jimbo fulani lazima iwe kweli ndiyo jumla ya matokeo ya vituo vyote vya jimbo husika. Ninawaomba sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati mlifuatilie jambo hili kwa ukaribu sana kwani inawezekana hapa ndipo ujanja mkubwa uliofanyika ili kuwezesha chama tawala kuendelea kuongoza nchi hii.

Ndugu zangu, ninaandika haya kwa uchungu mkubwa sana baada ya kusoma maoni ya wananchi ninaokutana nao mitaani na hata ninaposoma kwenye mitandao. Ukweli ni kwamba watanzania wengi hivi sasa wameichoka CCM na wanataka mabadiliko. Hali hii imeonekana dhahiri wakati wa mikutano ya Chadema kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.  Tafadhali viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati tusiwakatishe tamaa wananchi lazima tuthamini na kuenzi harakati za wananchi kutaka mabadiliko. 

HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM . MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO SURA YA MTU. MIFANO:

JIMBO:                        CHAMA:-----------UBUNGE:------RAIS:

ARUSHA MJINI - CHADEMA...................56,208..... .......54,208
                       CCM................... ....36,107..................39,107

MBEYA-MJINI:CHADEMA..................46,411.... ..............42,917
                     CCM............... .........24,236...................32,249

NYAMAGANA: CHADEMA...............38,171....................30,991
                     CCM.....................27,883......................32,320
 ILEMERA :CHADEMA................31,256......... .............29,701
                 CCM......................26,870........................9,143
 MASWA MAGH: CHADEMA......17,456............ ..........11,742
                    CCM..................12,824........................17,104
 MASWA MASH: CHADEMA......17,075.......................12,203
                        CCM.............. 17,014.......................21,150

 Kali zaidi ni hii ya JIMBO LA Musoma mjini: Kutoka KURA 14,723 za Mbunge wa CCM na kuongezwa kufikia KURA 49,858 za KIKWETE.

MUSOMA MJINI CHADEMA......21,335................23,211
CCM.....................................14,723................49,858???
Tutafakari hili.


Hebu angalia hali halisi. Na hili pia halihitaji elimu ya juu kulielewa na kulichambua. Wapiga Kura Waliojiandikisha ni: 20,137,303.
 Na Waliojitokeza Kupiga Kura Ni: 8,626,283 sawa na asilimia 42.84%.
Hii ina maana waliojiandikisha lakini hawajapiga kura ni: 11,511,020 sawa na asilimia 57.16%.
Ni jukumu letu pia kuangalia ni kwa nini wapiga kura wengi hawakujitokeza. Tusaidiane kuangalia sababu hizi nami nitaanza kwa chache ambazo nimezifanyia utafiti kwa kuwauliza wale ambao walijiandikisha lakini hawakuweza kupiga kura:

1. Hawakuona majina yao ingawa walijiandikisha
2. Walikuwa safarini nje ya Wilaya, Mkoa au Nchi
3. Walikuwa sehemu tofauti na waliojiandikisha
4. Walikuwa wagonjwa
5. Kuna ambao wamefariki katika kipindi cha uboreshaji wa daftari na kipindi cha kupiga kura
6. Kuna walioondolewa kwa madai kuwa wamekufa lakini wako hai.
Mie nadhani tayari kulikuwa na mazingira ya kuchakachua kura ndiyo maana idadi ilikuwa kubwa sana. haiwezekani kweli zaidi ya nusu ya wapiga kura wasiende kupiga kura wakati hamasa ilikuwa kubwa sana. Haiwezekani. Kuna namna.
Je, kwa maoni au utafiti wako ni sababu gani nyingine zilizowafanya watu wasijitokeze kupiga kura?



Jambo lingine lililodhihilisha kuwa CCM hawana sera ni pale  Prof. Lipumba kumpa JK ilani ya CUF eti iwasaidie kuchukua mambo! Wao CCM wanayo ya kwao na Lipumba anajua hilo ila Prof kwa ujanja aliitoa ili kuonyesha kuwa CCM hawana sera za maana wajifunze kuweka sera za kunufaisha taifa. That was a smart move. Nadhani pia CCM wanatafuta ya Chadema iweze kuwasaidia kwa siku za usoni.

1 comment:

  1. Mi nadhani kitu kingine kilichochangia wapiga kura wengi kutoshiriki zoezi la upigaji ni kura ni kwa sababu ya kukata tamaa na mazoea kwamba hata wakipiga kura bado CCM wanaweza kuiba na kupata ushindi hivyo ni sawa na kujisumbua tu kupiga kura lakini pia kwa wengine sababu ni usumbufu ambao waliupata baada ya kukuta majina yao yamehamishiwa katika vituo vingine.

    ReplyDelete