Search This Blog

Monday, November 1, 2010

MAKAMANDA WAANZA KUJITOKEZA KWA KUSHINDA KWA KISHINDO

Mh. John Magale Shibuda (pichani) na Silvester Kasurumbai wametangazwa rasmi na wasimamizi wa uchaguzi kuwa wabunge wa maswa magharibi na mashariki kwa tiketi ya CHADEMA baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi mkuu. Shibuda kakomba kura 17,456 Maswa Magharibi wakati Kasurumbai kazoa kura 17,075

Mbunge mtarajiwa wa Musoma Mjini Mh. Vicent Nyerere.
Taarifa rasmi iliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa Musoma Mjini leo imethibitisha ushindi wa Vincent Nyerere wa CHADEMA kuwa mbunge mpya baada ya kumshinda aliyekuwa mbunge, Vedasto Mathayo Manyinyi wa CCM. 

MATOKEO RASMIVincent Nyerere (CHADEMA) 21,335 (50.71%)
Vedasto Mathayo Manyinyi (CCM) 14,072 (39.38%)
Mustapha Juma Wandwi (Civic United Front) 253 (0.71%)
Chrisant Ndege Nyakitita (Democratic Party) 53 (0.15%)
Tabu Saidi Machibya (NCCR - Mageuzi) 19 (0.05%)

MGOMBEA wa CHADEMA jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa ameshinda kiti hicho baada ya kujizolea kura 17742 dhidi ya kura 16916 alizopata mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Monica Mbega ambaye ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

LEMA - Mbunge mteule wa jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya CHADEMA Godbless Lema akiwa anaondoka katika ofisi ya halmashauri ya jiji la Arusha mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge akiwa anasindikizwa na wanachi pamoja na wapambe wake. Mh. Lema amepata kura 56, 569 dhidi ya Dk. Batilda Burian wa CCM aliepata kura 37,460.

No comments:

Post a Comment