Search This Blog

Tuesday, November 2, 2010

MAKAMANDA WA CHADEMA WAZIDI KUONGEZEKA MJENGONI

MHE.MNYIKA MBUNGE WA UBUNGO- Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana hivi sasa ni kwamba Mgombea Ubunge kwa jimbo la Ubungo na Naibu katibu mkuu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. John Mnyika ametangazwa rasmi kuwa ndiye Mbunge mteule wa jimbo hilo kwa kuibuka na kura 66,743 huku mpinzani wake ambaye ni mgombea wa chama cha CCM Hawa Ngumbi ambaye amepata idadi ya kura 50,554.

Mh. Zitto Zubeir Kabwe,Jimbo la Kigoma Kaskazini - CHADEMA

Mh. Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu anyakua Jimbo la Mbeya Mjini - CHADEMA.
Msimamizi wa kituo cha Chuo cha Uhasibu Bw. Samweli Lazaro jimbo la Mbeya Mjini amemtangaza Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Joseph Mbilinyi a.k.a Mr II a.k.a Sugu kupitia chama cha CHADEMA kwa kuibuka na kura 46,411 na kumbwaga mpizani wake CCM Bw. Benson Mpesya kwa kupata idadi ya kura 24,327.

Mh. Freeman Mbowe,Jimbo la Hai - CHADEMA
Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe
ameshinda uchaguzi Jimbo la Hai na kurejea bungeni tena
kama mbunge baada ya kuwa nje kwa miaka mitano

No comments:

Post a Comment