Pichani anaonekana Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere akiwa amepanga foleni kusubiri kupiga kura yake wakati wa chaguzi mbalimbali zilizokuwa zinafanyika nchini enzi za uhai wake. Ninachojiuliza ni hivi???? Mbona viongozi wetu siku hizi hawapangi foleni?????????? Au huwa wamechoka????????? Au ni kutokuona umuhimu wa kujali utu wawatu au mtu mwingine??????
Katika uchaguzi wa mwaka huu sikuweza kuona Kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa Serikali na Chama akiwa amepanga foleni kusubiri kupiga kura badala yake walikuwa wanakuja na Msafara wa watu kibao. Je ni kwa vipi tulimuenzi Mwl. Nyerere wakati wa kupiga kura? Nawauliza nyie viongozi!!!!!!!!!
Swali jingine la nyongeza...Naomba kwa wale walio na kumbukumbu mnipe majina ya hao wengine waliopo kwenye foleni na baba wa Taifa tafadhali.... hasa huyo mwenye kofia hapo mbele na hao wawili walio nyuma ya Mwalimu.
No comments:
Post a Comment