Search This Blog

Tuesday, November 30, 2010

BEI YA COCA COLA JUU !!!!!

Kampuni ya Coca cola Nyanza Bottling company limited (NBCL) leo imetangaza rasmi bei mpya za soda zake, akitangaza bei hizo Mkuu wa mauzo na masoko wa kampuni hiyo bw. Bhubhinder Singh amezitaja bei hizo ni kama ifuatavyo...
Bei ya soda za kampuni hiyo zimepanda kutoka shilingi 400 kwa ujazo wa chupa ya ml350 hadi shilingi 500 kwa ujazo huo huo. Coca cola inawasihi wateja wake wote kutolipa zaidi ya shilingi 500 katika ununuzi wa soda kama ilivyoainishwa kwenye jedwali hapo juu.
Bei hiyo halali itatambulishwa kwa nguvu zote kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mabango, vipeperushi kwenye sehemu za mauzo, kwenye friji za mauzo, kalenda zitakazotoka za mwaka 2011, t-shirts, kofia na promosheni za mitaani ili kutusaidia hata pale tunapokwenda sehemu za vijijini tusibamizwe na wauzaji, kwani kwa vijijini bei ni hiyo ya 500 hata kabla haijapanda kihalali. Bei ya kreti moja inapanda kutoka 8,100 hadi 9,600 huku faida ya muuzaji ikipanda kutoka asilimia 18 na kuwa asilimia 25.
Kampuni hiyo imetoa changamoto kwa wadau wake kwa kuwazawadia chupa 3 za vinywaji bure kwa kila kreti moja watakalonunua kuanzia tarehe 1 hadi 10 december 2010 na kuanzia december 11 hadi 20.2010 Nunua kreti moja upate chupa mbili za vinywaji.

Sunday, November 28, 2010

KIKWETE KUMWAMBIA DR. BILALI AKAFUNDISHE UDOM!!! IMEKAAJE???

Nimemsikia juzi Rais Kikwete akimwagiza Dr Bilal awe anaenda kutoa lecture pale UDOM. Kuna mambo ambayo wananchi ni bora tujiulize.  

1. Kufundisha chuo kikuu ni lazima taratibu zitumike, kwa mfano lazima awe mwajiriwa iwe full time au part time na lazima atasimamiwa kwamba kweli anafanya kazi hiyo na hatimaye atalipwa kwa kazi hiyo. Unadhani kama makamu wa rais ataweza kukidhi matakwa ya kazi hiyo? 

2. Inamaana tuamini kuwa U-Makamu wa Rais hauna majukumu makubwa kiasi cha kumruhusu mhusika kuendelea na majukumu mengine na tuamini kuwa U-Makamu wa Rais ni kazi rahisi saaaaaaaaaana!!!


3. Dr. Bilal kama Makamu wa Rais anapewa ulinzi na ndiyo maana anaandamana na walinzi muda wote katika majukumu yake. Je, atakuwa anaingia nao kwenye vyumba vya kufundishia? Au nje ya darasa ni lazima kuwe na askari wa kutosha kumlinda??, Je wanafunzi wote wafanyiwe screening kabla ya kuingia kwenye kipindi au kama walikuwepo watoke wawe screened then waingie, kipindi si kitakuwa kimeisha kabla ya kuanza jamani!!!??. Na hizo kelele za ving'ora kila siku si itakuwa kero?? 

Kauli za JK huwa zinabeba maana anayoijua yeye. Mbona Shein ni Dr lakini haikuwahi kutokea kuambiwa akashike chaki kufundisha?. Hii itakuwa ni zaidi ya udhalilishaji na ni tatizo la JK kutokuzingatia hotuba ndio maana anajikuta kila siku yuko off-point.

Nadhani washauri wake wawe makini ila tuna mshukuru kwa kutufahamisha kuwa Makamu wa Rais hana kazi kubwa za cheo hicho hata kama atakaa Dodoma kuendelea kufundisha mambo pale Ikulu yataendelea tu.

Nawasilishaaaaaaaa!

Wednesday, November 24, 2010

BREAKING NEWS !!!! BARAZA LA MAWAZIRI TZ HILI HAPA...


1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe
Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu:  Stephen Wassira
2.Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano)  Samia Suluhu
2. Ofisi ya  Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
NAibu: Pereira Ame Silima
7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
15. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu:Dr. Fenella Mukangara
24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge

Monday, November 22, 2010

SITASHANGAA HAYA KUTOKEA TANZANIA


Mimi sitashangaa yafuatayo kutokea:

Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kusikitishwa na uteuzi wa nafasi mbalimbali utakaofanywa na JK... utasikia wanasema du kawaweka maswahiba wake.
Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kulalamikia rushwa kushamiri Tanzania .. kama kwamba walikosa mbadala wa kumweka uongozini kupambana na rushwa kwa umakini zaidi ..
Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuanza kulalamikia hali ngumu ya maisha.. ngoja nitoe scenario moja: Chadema wana sera ya elimu bure hadi kidato cha sita (6) kama si chuo kikuu. lakini sitashangaa walioinyima kura Chadema kuanza kuja kwako kukupigia magoti kuomba msaada wa kifedha ili apate ada ya kumpeleka mtoto sekondari. Wakati walikataa kuichagua iondoe hiyo kero. Sitashangaa elimu ya namna hii ikiendelea kutolewa na CCM huku wanachi wakishangilia ati CCM oyeeeeee!!

Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM waliokuwa wanavaa sare na kucheza kama hawana akili nzuri wakati wa mikutano ya kampeni kuendelea kuwa katika hali zao duni............ why? kwa sababu serikali imeshindwa kuwa na dira endelevu.
Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuendelea kuishi katika nyumba za mbavu za mbwa  wakati wamekataa kumpigia kura Dr. Slaa aliyekuwa ameahidi kushusha bei ya saruji (cement) ili wananchi walio wengi waweze kujenga nyumba imara na bora

Sitashangaa wanachi mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia ukosefu wa dawa hospitalini..
Sitashangaa wananchi na mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia utendaji mbovu wa idara mbalimbali za serikali (kumbuka jinsi Clouds walivyokuwa wanachambua utendaji mbovu wa idara mbalimbali e.g. EWURA, DAWASCO, TANESCO lakini wakawa vuvuzela wa CCM wakati wa uchaguzi)
Sitashangaa wapenzi wa CCM kulalamikia mishahara wanayopata na wakati huo huo kulalamikia posho kubwa za viongozi wakati wao maisha ni magumu hata kushindwa kuendesha biashara zao na kuinua kipato

Sitashangaa watu hawa kuvaa ma- Tshirt, kofia na kanga 2015 kushangilia na kushabikia CCM wakati wa uchaguzi mwingine.

Kutokana na hili naomba tushirikiane pamoja kuzidi kutoa elimu ya uraia, ipo siku yatabadilika ... "MAFISADI YANA MWISHO" Dr Slaa.

Saturday, November 20, 2010

AJALI HAINA KINGA

Familia yangu tulipata ajali juzi maeneo ya Nundu-Buzuruga, Nyakato Mwanza, kijana wangu kamanda jr (7months) ndo alivunjika mguu wa kulia kama anavyoonekana hapo. Tulipata matibabu mazuri Bugando hospital kwa sasa hali zinaendelea poa. Tuombeane uzima na kupona kwa haraka. 
We surrender all to God.

Wednesday, November 17, 2010

EID MUBARAK

KWA WANABLOG WANGU....NINAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID.

EID MUBARAK

Tuesday, November 16, 2010

BREAKING NEWS !!!! MIZENGO PINDA NDIYE WAZIRI MKUU

Mhe. Mizengo Pinda "Mtoto wa Mkulima"
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO KAYANDA PINDA KUWA WAZIRI MKUU, KWA MUJIBU WA TANGAZO LILILOSOMWA BUNGENI SASA HIVI NA SPIKA WA BUNGE MH. ANNE ABDALLAH.

ZOEZI LINALOFUATA SASA NI WABUNGE KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUU KWA KURA YA PAPO KWA PAPO NA BAADAYE UTAFUATIA UCHAGUZI WA NAIBU SPIKA AMBAYE ATAJULIKANA LEO PIA.

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.

BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA

HAWA WANAFAA KUWA WAZIRI MKUU..LAKINI.....

Hawa waheshimiwa - Mwandosya, Magufuli, Tibaijuka na Pinda pia Edward Lowassa na Dr. Harrison Mwakyembe wanafaa kwa nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa kuwa wana ushawishi katika siasa za Tanzania.

Mwakyembe: 
Alionekana ana uwezo, msomi aliyebobea na ambaye CCM wapiga debe wake (kundi linalomtetea) wamekuwa wakishinikiza apewe nyundo kumaliza ufisadi maana wananchi walivutiwa sana na jinsi kamati yake ilivyokuwa mstari wa mbele kushughulikia issue ya UFISADI. Kwa bahati mbaya ameondolewa kwa kuhofia upinzani atakaoupata kutoka kwa wababe wa siasa za bongo  na wafanyabiashara wanaoisaidia CCM

Lowassa:
Anajulikana kwa makeke yake; haiba na mvuto kwa jamii. Ni swahiba wa JK na ana ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM. Kinachomkwaza JK kumchukua, japo anatamani sana kumrejesha tena ni ile kashfa ya Richmond! Inasemekana JK anataka kutumia kigezo cha idadi nyingi za kura alizopata jimboni kwake kuonyesha kwa watanzania kuwa bado Lowasa anakubalika. Kuna kundi linaloongozwa na viongozi wastaafau wanaopinga hili kutokea....JK anahofia kwamba akimchukua CCM itamomonyoka!

Pinda:
Ndiye PM kwa sasa, kulingana na hali ya kisiasa ilivyop, jinsi CCM ilivyoaibishwa kwenye uchaguzi JK anaona Pinda si mtu wa aina anayoitaka pale. Anadhani Pinda ni muoga na mkimya sana, anataka mchapakazi, anayeogopewa na mwenye ushawishi katika siasa za Bongo! Kitendo cha PM kulia bungeni, kukili kwamba anawaogopa mafisadi nk vinamfanya JK akose imani na Pinda. Inasemekana pia kwamba wakati wa kampeni za urais Pinda yeye hakujishughulisha kukisaidia chama, aliamua kukaa pembeni kutokujihusisha na uchakachuaji, kitu ambacho JK anakiona kama ni usaliti! 

Mwandosya:
Vyanzo vyetu vinadai kwamba Mark Mwandonsya hana ushawishi kwa baadhi ya vigogo wa chama chake, na kwa wananchi. Washauri wa JK wameona kumpa nyundo huyo kutadhoofisha makali ya Serikali na kumuongezea mzigo JK....kitu ambacho kitaweka wazi mapungufu ya Rais.

Tibaijuka:
Hadi sasa anaongoza katika list, JK anataka kumpa nyundo mama huyu nguli amabaye ameonyesha ukomavu wa kisiasa na mwenye upeoo mkubwa sana katika anga za kimataifa! Kundi kubwa la vigogo wa Chama wanamtaka mama huyu amabaye anakubalika sana pia katika maeneo ya maziwa makuu. Inasemekana JK anatatizwa na kitu kimoja tu...tayari Dr. Asha Rose Migiiro ametajwa na ameshaombwa kuja kuomba urais kupitia CCM (2015) na tayari ameonyesha nia;sasa endapo PM akiwa Tibaijuka itakuwa vigumu kwa Rais na PM wake wote kuwa wanawake 2015!! Mbaya zaidi inasemekana pia Tibaijuka ana mpango wa kuomba kiti cha urais 2015!! Kwa taarifa tu ni kwamba uamauzi wa Dr Migiro ndiyo utaamua kama Tibaijuka apewe u-PM au la! Endapo atakuwa PM ina maana Dr. Migiro hatarejea kugombea 2015...ili kumpisha Tibaijuka abanjuke na upresidaa!!

Magufuli:
JK, washauri wake, CCM na wapinzani hawana hoja against huyu jamaa. Kila mmoja anajua kwamba ni mchapakazi, msomi na hana woga! Anakubalika sana na wananchi na upande wa wapinzani pia. JK anafahamu kwamba jamaa ni jembe na akimpa mpini basi chombo kitakaa mrama! TAtizo ni moja; JK anaogopa kufunikwa na Magufuli na inasemekana ana bifu naye binafsi.! Pia mafisadi wanahofia akipewa u-PM itakuwa mwisho wa wao kuichezea nchi hii, na mawaziri wanamuogopa, inasemekana kuna njama zinafanyika aondolewe hata kwenye baraza la mawaziri!! Tatizop wanajua wananchi watapiga kelele na itakuwa aibu kwao....Uwezekano wa yeye kupata u-PM ni endapo tu kama mama Migiro ataendeleza msimamo wake wa kuwania urais 2015.....

KWA MAONI YANGU NI KUWA MH. PINDA ATAEENDELEA KUWA WAZIRI MKUU KWA KUZINGATIA KUWA MABARIRIKO YA NAFASI YA SPIKA, THEN ETI JK ATEUE WAZIRI MKUU ITAKUWA SI NJEMA KISIASA. PIA KI-UCHUMI MABADIRIKO YA WAZIRI MKUU YATAIGARIMU NCHI MAANA WANATUNZWA KWA PESA ZETU HAO.

NAWASILISHA.

BARAZA JIPYA LA MAWAZILI ZANZIBAR HILI HAPA...

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame

2.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
Mhe. Omar Yussuf Mzee

3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Mhe. Haji Omar Kheri

4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.

5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

6. Wizara ya Katiba na Sheria

Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.

7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Hamad Masoud Hamad

8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban

9. Wizara ya Afya

Mhe. Juma Duni Haji

10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto

Mhe. Zainab Omar Mohammed

11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo

Mhe. Abdilahi Jihad Hassan

12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-

Mhe. Ali Juma Shamhuna

13. Wizara ya Kilimo na Maliasili

Mhe. Mansoor Yussuf Himid

14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Said Ali Mbarouk

16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika

Mhe. Haroun Ali Suleiman

17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Suleiman Othman Nyanga

18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Haji Faki Shaali

19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Machano Othman Said

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Issa Haji Ussi

2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Zahra Ali Hamad

3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya

Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya

4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,

Mhe. Bihindi Hamad Khamis

5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati

Mhe. Haji Mwadini Makame

6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,

Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi

Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa leo jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.