Thanks, asanteni kwa maombi yenu!!!!
Search This Blog
Saturday, April 16, 2011
Monday, April 11, 2011
BREAKING NEWS !!!! GBAGBO AKAMATWA!!
Hatimaye,Laurent Gbagbo amekamatwa kama Saddam Hussein akiwa amejificha shimoni huku jasho likimchuruzika. Ameondoka kwa aibu, pingu mikononi huku akipewa taulo ajifute jasho. Aliloa kuanzia kichwani hadi unyao. Alionekana kuchanganyikiwa akijifuta jasho hata kwenye makwapa bila aibu. Ni furaha iliyoje imla mwingine kuangukwa kwa kila aina ya aibu!Kwa habari zaidi, Bonyeza hapa.
Sunday, April 10, 2011
MBOZI WAJA NA STAILI MPYA YA TIBA: Huko ni MATONE ya Uponyaji
Nabii Joshua Mwantyala akiwanyunyuzia maji ya tiba wananchi waliokusanyika katika mkutano wake wa Neno la Mungu la uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wenye magonjwa sugu kama vile Ukimwi, Kansa na mengineyo. Nabii Joshua juzi alianzisha huduma ya tiba yake inayojulikana kama majibu ya tiba ya maajabu ya Loliondo ambapo yeye hutoa matone ya maji ya uponyaji.ambayo huwanyunyuzia wagonjwa vinywani.
BREAKING NEWS !!!! MUKAMA KATIBU MKUU CCM, Makamba na unabii wake chali
Katibu Mkuu mpya CCM (kulia) Bw. Wilson Mukama
Nape Nauye "Uenezi unaanzia hapa hapa"
Habari tulizopokea ni kwamba, hatimaye, CCM imeamua kumpiga kibuti katibu wake Mkuu Yusuf Makamba. Nafasi yake imechukuliwa na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa jiji la Dar Es Salaam, Wilson Mukama. Naye Nape Nnauye amechukua nafasi ya itikadi na uenezi ilikuwa ikishikiliwa na John Chiligati. Inaonekana zamu hii ni ya watoto wa wakongwe wa CCM. Maana Rehema Nchimbi mtoto wa John Nchimbi baba yake Emanuel Nchimbi,kama Nape, amechukua nafasi ya katibu wa organizesheni.Swahiba mwingine wa Kikwete, Zakhia Meghji aliyetupwa nje kwa kashfa ya EPA benki kuu na anayedaiwa kushiriki ufisadi wa kutisha kwenye wizara ya utalii amerejea kwa kishindo kwa kunyakua nafasi ya katibu wa fedha na uchumi iliyokuwa chini ya Amos Makala.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa CCM imeamua kujivua gamba kwa kuwatimua vinara na watetezi wa ufisadi hasa Makamba. Hatimaye Kikwete amelitupa jini na jinamizi la Makamba ambaye kimsingi alikuwa akimtawala Kikwete pamoja na uenyekiti wake. Bila shaka akina Tambwe Hiza sasa wanajinonihii kwenye suruali kutokana na muungu wao Makamba kupigwa buti. Je imejivua gamba au ni gamba lile lile la kujuana, kulindana, kufisidi, kuganga njaa, usanii na upuuzi mwingine? Time will tell.
......sijui nitoroke hata hiki kikao!!!! watu hawa hawana hata huruma- Makamba naye katimuliwa U-katibu mkuu aliyejifanya Nabii ndani ya CCM iliyooza.
"Poa tu"--Makala - .......Ndo wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa
Wednesday, April 6, 2011
Msaada kwenye tuta...Eti hili gari lipo kiofisi??
Jamani gari la serikali (pesa za walalahoi) limepakia mkaa na mazagazaga kibao, nadhani linatoka shopping kwa ajili ya kigogo fulani. Ninachojiuliza ni kuwa lipo kikazi zaidi??? au ndo kasi mpya????
Monday, April 4, 2011
UNA MIAKA 30??? OMBA UONGOZI BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA)
Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika
Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) ngazi ya taifa, linatarajia kufanya uchaguzi mwezi ujao.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa Bavicha kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu la chama.
Alitaja umri unaoruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35.
" Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama," alisema Mnyika.
Alisema kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia shilingi elfu thelathini.
Alisema waliogombea uchaguzi wa awali uliofutwa watajaza na kulipia upya hata kama waliogombea nafasi hizo hizo wanazogombea sasa kwa mujibu wa kanuni za chama.
Alisema Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama.
Saturday, April 2, 2011
HII INAASHIRIA NINI? USHINDI?? KIPIGO???
Upande huu wachezaji wa Simba Sports Club wakifanya mazoezi kwa ajili ya kuikabili TP Mazembe kesho.
Upande ule timu ya TP Mazembe wakikata mauno baada tu ya kuwasili uwanja wa ndege DSM.
Hii inaashiria nini?? Ushindi?? au Kipigo? Tusubiri kesho jumapili tarehe 3/4/2011
WEST HAM 2 MANCHESTER 4...........premier league
Wayne Rooney kapiga hat-trick na kuiwezesha Manchester United kuikong'oli West Ham United 4-2.
Kosa la Patrice Evra kuunawa mkono eneo la penati na faulo ya Nemanja Vidic kwa Carlton Cole kulisababisha Mark Noble wa West Ham kushindilia magoli 2 kwa njia ya penati.Lakini Manu ilipata goli la nne kupitia kwa Javier Hernandez Chicharito na kuondoka na ushindi wa goli 4-2.
Friday, April 1, 2011
TANZANIA YAWEKA REKODI YA NOTI.....kati ya noti hizo hapo chini ni ipi noti mpya?
Kwa mara ya kwanza Tanzania imeweka rekodi ya pesa/Noti kama ifuatavyo:
1. Kuwepo kwa noti mbili (2) zenye kiwango sawa na zipo katika mzunguko kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu sasa.
2. Noti mpya inazeeka na kuchakaa mapema kuliko noti ya zamani. Ukiangalia picha hiyo hapo juu utadhani noti ya upande wa chini ndio ya zamani,, kumbe ni mpyaaaaaa ina umri wa miezi minne(4) tu.
Sielewi kwa nini BoT inapata kigugumizi kushughulikia tatizo la hizo noti ambazo wanaziita mpya na zinatoa rangi kama batiki......kumbe hamna lolote!! Jamani serikali hii imeshindwa kabisa kuwajibika maana ni maajabu sana noti ndani ya miezi minne tu noti imeshazeeka, je ikimaliza miaka 5 si tutabaki na sarafu tu?????
Nawasilisha.
Thursday, March 31, 2011
LUKE 21:10-11
Sept. 11 (NY) Jan 11 (Haiti) March 11 (Japan)...Luke 21:10-11 Then Jesus said unto them,?
Nation shall rise against nation, and kingdom against kingdom. And great earthquakes shall be in divers places, and famines and pestilences, and fearful sights, and great signs shall there be from heaven. Jesus says for behold I come quickly, so ask yourself, are U ready?
MWAKA WA VIKOMBEEEEEEE!!!!!!!!!!!
BABU WA LOLIONDO
MAGRETH MUTALEMWA WA TABORA
FATUMA SENGO WA DODOMA
Kilianza kikombe cha Babu kule Loliondo (KKKT)….kisha kikombe cha brazameni kule Rombo (Mkatoliki); Bibi kule Tabora (Mkatoliki) na kule Mbeya Babu dogo (yawezekana akawa mMoravian huyu …lol). Sasa Fatuma Sengo (Muislam). Baada ya muda tutarajie Wasabato na Waanglikana, Wa Full Gospel, na wengine nao kuja na vikombe vyao…andaeni makoo yenu kupitisha hayo madawa!
Swali langu ni kuwa kwa nini hawa "Wataalamu" wanatumia vikombe?????
Friday, March 18, 2011
Wednesday, March 16, 2011
Sasa CCM ni Bora Liende: Kila siku utasikia hili na lile.
UVCCM wamtaka Makamba ang'oke
*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?
Kuna kila dalili kuwa chama tawala CCM sasa kinajiendesha kwa mtindo wa bora liende. Asubuhi utasikia huyu karopoka hili,mchana utamsikia mwingine karopoka lile,alimradi ni vurugu mechi kila siku.
Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita..
“Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai,” alisema Bw Ulega.
Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.
Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.
Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.
“Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.
Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.
“Hawa watu ni mawaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama,” alisema.
Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.
Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.
"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.
Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema,"
Naye Mhe. Lowassa naye alisema “Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imepanda hilo nalo tusubiri vikao? “
Thursday, March 10, 2011
HAPPY BIRTHDAY, CATHY
Mdau wangu Cathy yupo UDOM, ametimiza miaka kadhaa leo. Let God leads your ways. This Blog wishes you Happy Birthday
Wednesday, March 9, 2011
DAWA YA LOLIONDO HII HAPA INAITWA "MUGARIGA"
Mmea unaojulikana kama "Murigariga".
Babu anasema alioteshwa kuwa mti huo wa porini na Mungu na kuwa unatibu magoniwa yote sugu, sharti ni kuwa ni lazima yeye ndo akupe kikombe hicho cha "uzima" ndo unapona, ukienda kujitengezea mwenyewe haifanyi kazi, bila shaka ndo sababu ya umati mkubwa kujazana katika kijiji kidogo cha Samunge huko Loliondo.
FOLENI ya magari kwenda Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile
Dawa ikiwa jikoni ikichemshwa
MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambukile Mwasapile (78), wa kijiji cha Samunge-Loliondo, wilayani Ngorongoro, Arusha akitibu wagonjwa.
Monday, March 7, 2011
SERIKALI YA CCM INAVYOCHEMKA...Mhe Pinda Kamkataza Mgufuri kubomoa nyumba
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Dk.John Magufuli, kusitisha mara moja operesheni bomoabomoa inayoendelea nchini hadi serikali itakapotafakari upya suala hilo. Alitoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chato, mkoani Kagera.
Waziri Mkuu alisema uamuzi huo unatokana na malalamiko mengi yanayotolewa na wananchi ikiwemo kutopewa elimu ya kutosha juu ya operesheni hiyo.
"Magufuli akishaagiza, meneja wa TANROADS jasho linamtoka na kuanza kubomoa... hatuendi hivyo. Ukitizama X wanalolibandika linakera," alisema Waziri Mkuu.
Hii serikali bwana!!!!!!!!!! . Maagizo yanatolewa barabarani. Kwanini asimuite ofisini kwake akampa maagizo ya kusitisha zoezi hilo? Halafu amwachie yeye mwenyewe atangaze?
Hapo Magufuli kesha vunjwa moyo na kwa kifupi amedhalilishwa mbele ya Tanroads na mbele ya wapiga kura wake na mbele ya watanzania kwa ujumla. Unadhani hata mbeleni atakapotoa maagizo, si wananchi watamwambia subiri kwanza Waziri Mkuu akubali. Hii ndiyo CCM bana!!!!
Hii tabia ya kila kiongozi wa serikali kutoa tamko namna anavyoona yeye tena vikao vya barabarani inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la uongozi (leadership) kwenye serikali kwa sasa.
Kibaya zaidi ili tatizo litaigharimu sana nchi na wananchi wake kwa sababu kila kiongozi atafanya lile ambalo anaona linafaa kwake yeye binafsi na hii ni hasara kubwa kwa taifa.
Leadership ni kitu muhimu sana mahali popote pale panapokuwa na watu au viumbe zaidi wa mmoja. Hata wanyama, wadudu, ndege wa angani, samaki wa baharini wana kiongozi wao na wanafuata kila kile kiongozi anacho fanya. Kiongozi si jina tu bali ni matendo. Kiongozi lazima kweli aonekane ni kiongozi na wale wanafuata watambue kuwa kuna kiongozi na watufuate njia zake.
Hii tabia ya viongozi wa serikali tena Mawaziri kila mmoja kuja na kauli tofauti kwenye jambo moja kwa kweli inakera na kuchanganya sana wananchi.
HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!!
Sunday, March 6, 2011
Friday, March 4, 2011
UKOSEFU WA MVUA...Mamlaka ya hali ya hewa mbona imekaa kimya????
Baadhi ya maeneo yanavyoonekana sasa kwa ukame.
HALI ya nchi yetu kiuchumi inaendelea kudorora kutokana na sababu nyingi, kubwa ikiwa ni ukosefu wa mvua. Kwa muda mrefu sasa Tanzania inapata mvua kidogo ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hivyo kukwamisha maendeleo ya kilimo na kuliweka taifa katika hali tete ya chakula, ingawa Serikali inasema hali si mbaya sana.
Ukweli ni kwamba, hali si nzuri kiuchumi na chakula kutokana na kukosekana mvua za kutosha. Hata mvua za masika ambazo kwa kawaida zinaanza kunyesha mwezi Machi sehemu mbalimbali nchini, hazionyeshi dalili ya kuwepo kiasi cha kutosha mwaka huu.
Kinachotushangaza, Malamaka ya Hali ya Hewa imekaa kimya bila kutoa taarifa juu ya matarajio ya kuwepo kwa mvua za kutosha au la. Tunachojua ni kwamba, moja ya kazi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa ni kufuatilia mwenendo wa hali ya hewa nchini na kutoa taarifa kwa taifa ili kuiandaa Serikali na wananchi kuchukuhua tahadhari juu ya matukio yanayoweza kutokea kulingana na hali itakavyo kuwa.
Kwa mfano, kama kutakuwa na mvua kidogo Serikali na taasisi nyingine za maendeleo ziandae mazingira ya kuwahamasisha wananchi kulima na kupanda mazao mapema na yale yanayostahimili ukame. Kama mvua zikiwa nyingi ambazo zinatarajiwa kuleta madhara kama vile mafuriko, wananchi waweze kuandaliwa kuhamishia makazi yao sehemu za miinuko ili wasikumbwe maafa.
Kilimo cha Tanzania kinategemea mvua kwa aslimia 100 hivyo wananchi wanatakiwa kupewa taarifa za kuwepo kwa mvua au la, ili waweze kuandaa mashamba na kupanda mazao, au wasifanye hivyo.
Kutokana ukimya wa mamlaka hiyo wakati huu tunapokabiliwa na matatizo mengi na hasa ya kukosekana kwa umme ambao kwa asilimia kubwa hutegemea mvua, tunajiuliza juu ya uwezo Mamlaka wa kufanya kazi yake ipasavyo. Mashaka yetu ni je, ina wataalumu wa kutosha na waliobobea katika fani hiyo? Kama wapo je, wanavifaa vya kutosha na vya kisasa kuweza kupata taarifa sahihi kama ilivyo katika nchi zilizoendelea? Kama havipo, Serikali imefanya nini, au haioni umuhimu wa mamlaka hii?
Katika nchi zilizoendelea idara, au mamlaka ya hali ya hewa inapewa umhumimu wa hali ya juu kwa sababu hakuna jambo linalofanyika katika sekta za kilimo, usafirishaji, biashara na maisha ya jamii bila kuwa na taarifa sahihi hali ya hewa.
Umuhimu wa mvua katika nchi yetu unatambulika kwa sababu mfumo wetu wote wa uzalishaji unategemea maji ya mvua. Kwa mfano, umeme unaohitajika katika sekta za uzalishahi na huduma za jamii kama viwanda, miradi ya maendeleo, ujasiriamali, elimu, hospitali unategema nguvu ya maji ambayo chanzo chake ni kikuu ni mvua, ndiyo maana sasa hivi tuko gizani na huduma zote zimekwama.
Kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu kiko shakani, hivyo kuiweka nchi katika uwezekano wa kukumbwa na njaa kutokana na upungufu wa chakula ambao tayari umeanza kujitokeza katika maeneo kadhaa.
Tunasisitiza na kuimbusha Mamlaka ya Hali Hewa kufanya kazi yake ipasavyo na kulijulisha taifa juu matarijio ya mvua kuanzia sasa. Hofu yetu ni kwamba, kukaa kimya kwao kunaweza kuliingiza taifa katika matatizo makubwa ya kuanza kuchukua hatua za dharua badala ya kuandaa mikakati ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na kuwepo, au kutokuwepo kwa mvua.
Subscribe to:
Posts (Atom)