Search This Blog

Friday, October 7, 2011

Kwa matokeo ya Igunga tutegemee "VUA GAMBA PART 2"

Pamoja na maneno mengi ya kuonyesha kuwa kuna umakini na mvuto wa kisiasa katika jamii, lakini kwa watu wanaojua kutafakari na kupambanua mabo ni dhahiri kuwa Chadema imeweza kuleta mabadiriko ya kisiasa Tanzania. 

Ebu turejee matokeo ya Igunga kidogo:
Mwaka 2010 CCM walipata kura 36,000: Uchaguzi mdogo wa juzi wakaambulia kura 26,484 ambazo zimepatikana katika mazingira yanayolalamikiwa na wadau wa maendeleo ya kijamii.
Mwaka 2010 CHADEMA hawakupata kura: Uchaguzi mdogo wakapata kura 23,286 hii inaonekana wamepanda chati na kukubalika katika jamii.
Mwaka 2010 CUF walipata kura 11,000: Uchaguzi mdogo wakaambulia kura 2,014.

Hebu tutafakari haya:
Je kwa takwimu hizo ni chama gani chenye mvuto katika jamii??Kutokana na mwenendo wa kisiasa?

Tukirejea kwenye gharama zilizotumika, CCM ilitumia Tshs 3biln, CHADEMA Tshs 400Mln na CUF Tshs 150Mln. CCM wamepata kura 26,484, CHADEMA kura 23,286, CUF kura 2,104, kwa hesabu za haraka ukigawanya idadi ya pesa na kura walizopata hali itakuwa hii: CCM:3,000,000,000/26,484=113,275/=
CHADEMA:400,000,000/23,286=17177/=
CUF:150,000,000/2,104=71,292/= hivyo basi
CCM imetumia Tsh 113,275/= kupata kura moja.
CDM imetumia Tsh 17,177/= kupata kura moja
CUF imetumia Tsh 71,292/= kupata kura moja
Kwa uchambuzi huo utaona kuwa CHADEMA inakubalika kwa jamii bila hata ya kutumia gharama kubwa ya kipesa. Ikiwa na maana kuwa sera na hoja zinakubalika zaidi kwa jamii na kimeleta imani katika jamii zaidi kuliko wale wanaotumia hela nyingi kutafuta imani na umaaufu kwa jamii. Kwa hiyo CCM walitumia pesa nyingi sana kutafuta kura moja uliko vyama vingine na hii inaonyesha kuwa imepoteza imani kwa jamii ndo maana inawagharimu kupata idadi ya kura.

Ukiona chama chako kinaporomoka kwa idadi ya kura basi sioni sababu ya kushangilia eti umeshinda kwa kishindo wakati kila kukicha wananchi wako wanakuchoka. Chama chenye takwimu ambayo inapanda kila siku kinadhiirisha kuwa wapo focused na kina uongozi madhubuti na kinakubalika kwa wananchi. 

Nadhani ile falsafa ya kujivua gamba tafakari yake siyo kwa viongozi tu ila hata wanachama wake nao wanajivua gamba na ku-support chama kingine kilicho na msimamo makini. Nadhani kwa matokeo ya Igunga tutegemee "vua gamba part 2" baada ya part 1 kuonekana imewashindwa.

Mungu ibariki Tanzania


1 comment:

  1. Pamoja na vitisho vya CCM, kugawa pesa na wali lakini nguvu ya CHADEMA ilikuwa kali sana. Na bado tunawasubiri 2015 tuchukue nchi. Ngoja tu wajivue magamba

    ReplyDelete