Search This Blog

Wednesday, March 16, 2011

Sasa CCM ni Bora Liende: Kila siku utasikia hili na lile.

UVCCM wamtaka Makamba ang'oke

*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?



Kuna kila dalili kuwa chama tawala CCM sasa kinajiendesha kwa mtindo wa bora liende. Asubuhi utasikia huyu karopoka hili,mchana utamsikia mwingine karopoka lile,alimradi ni vurugu mechi kila siku.
 UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.
Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita..
“Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai,” alisema Bw Ulega.
Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.
Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.
Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.
“Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.
Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.
“Hawa watu ni mawaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama,” alisema.
Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.
 KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

 Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema,"

Naye Mhe. Lowassa  naye alisema “Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imepanda hilo nalo tusubiri vikao? “

No comments:

Post a Comment