Search This Blog

Thursday, March 31, 2011

LUKE 21:10-11

Sept. 11 (NY) Jan 11 (Haiti) March 11 (Japan)...Luke 21:10-11 Then Jesus said unto them,?

Nation shall rise against nation, and kingdom against kingdom. And great earthquakes shall be in divers places, and famines and pestilences, and fearful sights, and great signs shall there be from heaven. Jesus says for behold I come quickly, so ask yourself, are U  ready?

jamani eee KAZI NI KAZI...




NANI ZAIDI KATI YA HAWA JAMAA???

MWAKA WA VIKOMBEEEEEEE!!!!!!!!!!!

BABU WA LOLIONDO

MAGRETH MUTALEMWA WA TABORA

FATUMA SENGO WA DODOMA

Kilianza kikombe cha Babu kule Loliondo (KKKT)….kisha kikombe cha brazameni kule Rombo (Mkatoliki); Bibi kule Tabora (Mkatoliki) na kule Mbeya Babu dogo (yawezekana akawa mMoravian huyu …lol). Sasa Fatuma Sengo (Muislam). Baada ya muda tutarajie Wasabato na Waanglikana, Wa Full Gospel, na wengine nao kuja na vikombe vyao…andaeni makoo yenu kupitisha hayo madawa!


Swali langu ni kuwa kwa nini hawa "Wataalamu" wanatumia vikombe?????

Wednesday, March 16, 2011

MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA

Sasa CCM ni Bora Liende: Kila siku utasikia hili na lile.

UVCCM wamtaka Makamba ang'oke

*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?



Kuna kila dalili kuwa chama tawala CCM sasa kinajiendesha kwa mtindo wa bora liende. Asubuhi utasikia huyu karopoka hili,mchana utamsikia mwingine karopoka lile,alimradi ni vurugu mechi kila siku.
 UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.
Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita..
“Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61 ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai,” alisema Bw Ulega.
Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.
Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.
Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.
Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.
“Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.
Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.
“Hawa watu ni mawaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama,” alisema.
Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.
 KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

 Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema,"

Naye Mhe. Lowassa  naye alisema “Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imepanda hilo nalo tusubiri vikao? “

Thursday, March 10, 2011

HAPPY BIRTHDAY, CATHY

Mdau wangu Cathy yupo UDOM, ametimiza miaka kadhaa leo. Let God leads your ways. This Blog wishes you Happy Birthday

Wednesday, March 9, 2011

DAWA YA LOLIONDO HII HAPA INAITWA "MUGARIGA"

Mmea unaojulikana kama "Murigariga".
Babu anasema alioteshwa kuwa mti huo wa porini na Mungu na kuwa unatibu magoniwa yote sugu, sharti ni kuwa ni lazima yeye ndo akupe kikombe hicho cha "uzima" ndo unapona, ukienda kujitengezea mwenyewe haifanyi kazi, bila shaka ndo sababu ya umati mkubwa kujazana katika kijiji kidogo cha Samunge huko Loliondo.
FOLENI ya magari kwenda Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu, Ambilikile Mwasapile
Dawa ikiwa jikoni ikichemshwa
MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambukile Mwasapile (78), wa kijiji cha Samunge-Loliondo, wilayani Ngorongoro, Arusha akitibu wagonjwa. 




Monday, March 7, 2011

SERIKALI YA CCM INAVYOCHEMKA...Mhe Pinda Kamkataza Mgufuri kubomoa nyumba



WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemwagiza Waziri wa Ujenzi, Dk.John Magufuli, kusitisha mara moja operesheni bomoabomoa inayoendelea nchini hadi serikali itakapotafakari upya suala hilo. Alitoa agizo hilo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Chato, mkoani Kagera.
Waziri Mkuu alisema uamuzi huo unatokana na malalamiko mengi yanayotolewa na wananchi ikiwemo kutopewa elimu ya kutosha juu ya operesheni hiyo.
"Magufuli akishaagiza, meneja wa TANROADS jasho linamtoka na kuanza kubomoa... hatuendi hivyo. Ukitizama X wanalolibandika linakera," alisema Waziri Mkuu.

Hii serikali bwana!!!!!!!!!! . Maagizo yanatolewa barabarani. Kwanini asimuite ofisini kwake akampa maagizo ya kusitisha zoezi hilo? Halafu amwachie yeye mwenyewe atangaze?
Hapo Magufuli kesha vunjwa moyo na kwa kifupi amedhalilishwa mbele ya Tanroads na mbele ya wapiga kura wake na mbele ya watanzania kwa ujumla. Unadhani hata mbeleni atakapotoa maagizo, si wananchi  watamwambia subiri kwanza Waziri Mkuu akubali. Hii ndiyo CCM bana!!!!

Hii tabia ya kila kiongozi wa serikali kutoa tamko namna anavyoona yeye tena vikao vya barabarani inaonyesha kuwa kuna tatizo kubwa la uongozi (leadership) kwenye serikali kwa sasa.

Kibaya zaidi ili tatizo litaigharimu sana nchi na wananchi wake kwa sababu kila kiongozi atafanya lile ambalo anaona linafaa kwake yeye binafsi na hii ni hasara kubwa kwa taifa.

Leadership ni kitu muhimu sana mahali popote pale panapokuwa na watu au viumbe zaidi wa mmoja. Hata wanyama, wadudu, ndege wa angani, samaki wa baharini wana kiongozi wao na wanafuata kila kile kiongozi anacho fanya. Kiongozi si jina tu bali ni matendo. Kiongozi lazima kweli aonekane ni kiongozi na wale wanafuata watambue kuwa kuna kiongozi na watufuate njia zake.

Hii tabia ya viongozi wa serikali tena Mawaziri kila mmoja kuja na kauli tofauti kwenye jambo moja kwa kweli inakera na kuchanganya sana wananchi.
HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!!

Friday, March 4, 2011

UKOSEFU WA MVUA...Mamlaka ya hali ya hewa mbona imekaa kimya????

Baadhi ya maeneo yanavyoonekana sasa kwa ukame.

HALI ya nchi yetu kiuchumi inaendelea kudorora kutokana na sababu nyingi, kubwa ikiwa ni ukosefu wa mvua. Kwa muda mrefu sasa Tanzania inapata mvua kidogo ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hivyo kukwamisha maendeleo ya kilimo na kuliweka taifa katika hali tete ya chakula, ingawa Serikali inasema hali si mbaya sana.

Ukweli ni kwamba, hali si nzuri kiuchumi na chakula kutokana na kukosekana mvua za kutosha. Hata mvua za masika ambazo kwa kawaida zinaanza kunyesha mwezi Machi sehemu mbalimbali nchini, hazionyeshi dalili ya kuwepo kiasi cha kutosha mwaka huu.


Kinachotushangaza, Malamaka ya Hali ya Hewa imekaa kimya bila kutoa taarifa juu ya matarajio ya kuwepo kwa mvua za kutosha au la. Tunachojua ni kwamba, moja ya kazi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa ni kufuatilia mwenendo wa hali ya hewa nchini na kutoa taarifa kwa taifa ili kuiandaa Serikali na wananchi kuchukuhua tahadhari juu ya matukio yanayoweza kutokea kulingana na hali itakavyo kuwa.  

Kwa mfano, kama kutakuwa na mvua kidogo Serikali na taasisi nyingine za maendeleo ziandae mazingira ya kuwahamasisha wananchi kulima na kupanda mazao mapema na yale yanayostahimili ukame.  Kama mvua zikiwa nyingi ambazo zinatarajiwa kuleta madhara kama vile mafuriko, wananchi waweze kuandaliwa kuhamishia makazi yao sehemu za miinuko ili wasikumbwe maafa.

Kilimo cha Tanzania kinategemea mvua kwa aslimia 100 hivyo wananchi wanatakiwa kupewa taarifa za kuwepo kwa mvua au la, ili waweze kuandaa mashamba na kupanda mazao, au wasifanye hivyo. 


Kutokana ukimya wa mamlaka hiyo wakati huu tunapokabiliwa na matatizo mengi na hasa ya kukosekana kwa umme ambao kwa asilimia kubwa hutegemea mvua, tunajiuliza juu ya uwezo Mamlaka  wa kufanya kazi yake ipasavyo.  Mashaka yetu ni je, ina wataalumu wa kutosha na waliobobea katika fani hiyo? Kama wapo je, wanavifaa vya kutosha na vya kisasa kuweza kupata taarifa sahihi kama ilivyo katika nchi zilizoendelea? Kama havipo, Serikali imefanya nini, au haioni umuhimu wa mamlaka hii?

Katika nchi zilizoendelea idara, au mamlaka ya hali ya hewa inapewa umhumimu wa hali ya juu kwa sababu hakuna jambo linalofanyika katika sekta za kilimo, usafirishaji, biashara na maisha ya jamii bila kuwa na taarifa sahihi hali ya hewa. 
Umuhimu wa mvua katika nchi yetu unatambulika kwa sababu mfumo wetu wote wa uzalishaji unategemea maji ya mvua. Kwa mfano, umeme unaohitajika katika sekta za uzalishahi na huduma za jamii kama viwanda, miradi ya maendeleo, ujasiriamali, elimu, hospitali unategema nguvu ya maji ambayo chanzo chake ni kikuu ni mvua, ndiyo maana sasa hivi tuko gizani na huduma zote zimekwama.

Kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa nchi yetu kiko shakani, hivyo kuiweka nchi katika uwezekano wa kukumbwa na njaa kutokana na upungufu wa chakula ambao tayari umeanza kujitokeza katika maeneo kadhaa.

Tunasisitiza na kuimbusha Mamlaka ya Hali Hewa kufanya kazi yake ipasavyo na kulijulisha taifa juu matarijio ya mvua kuanzia sasa. Hofu yetu ni kwamba, kukaa kimya kwao kunaweza kuliingiza taifa katika matatizo makubwa ya kuanza kuchukua hatua za dharua badala ya kuandaa mikakati ya kukabiliana na majanga yanayoweza kusababishwa na kuwepo, au kutokuwepo kwa mvua.

Friday, February 25, 2011

TAARIFA YA MSIBA

Ukoo wa Mukama, wa Majita  Musoma, wanasikitika kutangaza kifo cha Ndugu yetu mpendwa Japhet Muura Mukama kilichotokea jana 24/2/2011 hospitali ya Muhimbili. Mazishi yatafanyika Jumapili tarehe 27/2/2011 Dar es Salaam. Marehemu ameacha Mke na watoto watano - Joyce, Mukama, Mercy,Kabuche na Kainda. Mwana blog hii (Baraka Mukama) ni miongoni mwa wadogo zake na marehemu. Tunaomba sana kwa kipindi hiki cha masikitiko na majonzi Bwana Mungu awe pamoja nasi. Atupe faraja ya pekee na sisi tuliobaki tuwe na umoja, amani na upendo. Tunashukuru kwa wote waliotutumia salaamu za rambirambi.
Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina na Bwana libarikiwe. Amen

Thursday, February 24, 2011

CHADEMA YARINDIMA JIJI LA MWANZA.

Viongozi wa CHADEMA WAKIWA KWENYE MAANDAMANO JIJINI MWANZA 

Viunga vyote vilijaa nguvu ya umma.

Mhe. Dk Silaa akiwahutubia umatu wa watu viwanja vya furahisha jijini mwanza

                   Pipooooozzzzz 

“Tumekuja kwenu kuomba kibali cha kuhakikisha mnatuunga mkono ili kuiondosha serikali ya CCM pamoja na Kikwete na hivyo tunaanzia Mwanza kuzindua mkakati huu wa kupita kufanya kazi hiyo mkoa hadi mkoa pamoja na kuwashukuru baada ya kuwachaguwa wabunge wa chadema”alisema Mbowe .

Sunday, February 20, 2011

MAAMUZI YA JK NA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA HAYA HAPA:


TUMETOA BAADHI TU YA MAAMUZI YA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA.......


5. Aidha, Kamati ya Maafa ya Mkoa imeelekezwa kutengeneza taratibu nzuri zitakazohakikisha kuwa mapema iwezekanavyo, wananchi hao wanarejea makwao ili waendelee na shughuli zao za kawaida hasa sasa ambapo hatari ya milipuko katika maghala ya Gongolamboto haipo tena.
JAMANI HEBU ANGALIA HIYO PICHA. JE KUNA UWEZEKANO WA MTU KURUDI KUISHI HUMO NA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE??? SOMA NAMBA 5 HAPO JUU. NILIDHANI BARAZA LINGEAMUA KUWEPO NA UTARATIBU WA KUTOA MAHEMA (TENTS) KWA WAATHIRIKA, AMA KUWAPELEKA KATIKA BAADHI YA NYUMBA ZA SERIKALI KWA MUDA. MAANA MIUNDOMBINU IMEHARIBIKA SANA. HUWEZI KUENDELEA NA SHUGHULI WAKATI NYUMBA HAIPO NI MAJIVU TU. HAWA JAMAA VIPI??

2. Kuhusu waliopoteza maisha, tumeamua kuwa, Serikali igharamie mazishi ya marehemu wetu hao popote ndugu watakapoamua wakazikwe. Baadae ndugu wa marehemu wapewe kifuta machozi.
WASIWASI WETU NI KUWA HADI MUDA HUU TAKWIMU SAHIHI ZINATIA UTATA MAANA INASEMEKAMA WALIOFARIKI NI WENGI. TUKIO LA MBAGALA HADI SASA MALIPO HAYAJAKAMILIKA, IWEJE LA GONGOLAMBOTO?? WAWAJIBIKE!!!!

8. Baraza la Usalama la Taifa, limeagiza Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Dar es Salaam na Kitengo cha Maafa cha Taifa wazitambue mapema iwezekanavyo nyumba zilizoharibiwa, wenye nyumba na kuhakikisha kuwa matayarisho husika yanafanyika ikiwa ni pamoja na uthamini ili walipwe fidia wanayostahili bila kuchelewa.
TUNAOMBA KAMATI HII IANGALIWE UPYA MAANA MBAGALA WALIPROVE FAILURE.
14. Mwisho, Baraza la Usalama wa Taifa linawaomba wananchi waliohama warejee kwenye makazo yao kwani kipindi cha hatari ya mabomu kulipuka kimekwishapita. Tunaomba na kusisitiza wajiepushe kuchezea mabomu yaliyodondoka katika maeneo yao ambayo bado hayajaondolewa
KIPINDI CHA HATARI BADO HAKIJAPITA MAANA MABOMU NDO HASA YAPO URAIANI AMBAPO JK NA BARAZA LA USALAMA LA TAIFA LINAWATAKA WANANCHI WAKAISHI NAYO HUKO AMBAPO MABOMU YAMEDONDOKA. JE NI NAMNA GANI UTAWAZUIA MIFUGO INAYOCHUNGA MAENEO YA WAZI WASIYAGUSE HAYO MABOMU??? NADHANI KWA KIPINDI HIKI SERIKALI INGEWAHIFADHI WANANCHI SEHEMU SALAMA ZAIDI MAANA MABOMU YAMESAMBAA GONGOLAMBOTO NA MAENEO YA JIRANI.
KUNA DALILI YA HUZUNI HAPO?????




Thursday, February 17, 2011

BREAKING NEWS !!!! GONGOLAMBOTO YALIPULIWA NA MABOMU!!

Maeneo ya Gongolamboto Dar, yakilipuka na mabomu!!! Hali inatisha

Jiji zima la Dar maeneo mengi yalihathirika na mabomu

Majeruhi wakipata matibabu hospital ya Amama

Vijana na watoto walipata majeraha na wengine kupoteza maisha.

Watu kadhaa wamekufa kwa kupigwa na mabomu na kugongwa na magari baada ya kusikika kwa mlipuko wa mabomu maeneo ya Gongolamboto. Hali hadi muda huu inasikitisha sana. HIVI KWA NINI SERIKALI ISIWAJIBIKE??

Maeneo mengi yaliyopo ndani ya mji wa Dar es salaam inashangaza kumilikiwa na Jeshi la Wananchi mfano:Kigamboni(mwanzoni)i,Masaki,Mwenge (Lugalo),Mikocheni,Msasani,Kawe n.k haya ni maeneo yalipaswa kuwa makazi rasmi ya Wananchi. Tofauti yake ni kuwa Wananchi wanaishi nje ya Mji na jeshi linamiliki katikati maeneo ya jiji la DSM huku maeneo yake mengi yakiwa wazi eti mara Range,mara mess.Hili jeshi la ajabu huwezi kulinda Wananchi ukiwa katikati yao,hapo ni kuwa jeshi ndilo linalindwa na Wananchi. Kutokana na ukuaji wa Mji,na kwa usalama wa raia na shughuli za kijeshi na kazi zao Wanajeshi walipaswa KUHAMA na kuelekea nje ya Mji. Mbona Tanzania tumebahatika kuwa na maeneo mengi tu ya wazi nje ya miji. Kwa nini jeshi linang'ang'ania kuishi na mabomu yao mijini? Hii ni hatari.

Leo hii tunapoteza watu wengi kwa uzembe wa serikali,kusababisha ulemavu wa Maisha na kuongeza umasikini, kupoteza rasilimali kidogo za wananchi kwa uzembe usiohitaji usiohitaji hata kuunda tume. Serikali mara ngapi itatoa fidia na kutumia gharama nyingi za kimaafa.

Ebu tuache "SIASA" ni wakati sasa kwa JWTZ kuhama maeneo ya Raia na kuelekea nje kabisa ya mji,huko mtakuwa mmetunusuru jamani.
BLOG HII INATOA POLE NA RAMBIRAMBI KWA WOTE WALIOATHIRIKA NA MABOMU YA GONGOLAMBOTO. 




Tuesday, February 15, 2011

BARAZA LA MAWAZILI KIVULI HILI HAPA

KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe jana alitangaza Baraza la Mawaziri Kivuli likiwa na mawaziri 29 wote kutoka Chadema. Katika Baraza hilo, Mbowe amewateua Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kuwa Waziri Kivuli wa Fedha, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kuwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Kwa upande wa Mdee, atakuwa ana kwa ana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ambaye alianza kutekeleza wajibu wake katika wizara hiyo kwa kasi baada ya kuteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Mbowe akitangaza Baraza lake Kivuli jana alisema, anaweza kulifanyia mabadiliko na kuhusisha wabunge wa
vyama vingine vya upinzani wakati wowote na kwamba mabadiliko yatafanyika baada ya wao (wapinzani) kuzungumza na kufikia muafaka. Katika baraza hilo lililotangazwa baada kipindi cha maswali na majibu, Mbowe mwenyewe anakuwa Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi huku naibu wake akiwa Silinde David Ernest.

Idadi ya Mawaziri Kivuli
Mbowe alisema baraza lake halina mawaziri wengi ili kuonyesha mfano wa kukwepa matumizi yasiyokuwa ya lazima kwa vitendo."Pamoja na idadi ya mawaziri na naibu mawaziri wa Serikali kuwa 50, uteuzi wangu umeteua wasemaji wakuu na manaibu wasiozidi 29 ili kuonyesha kwa kivitendo, kilio chetu cha muda mrefu cha kuwa na baraza dogo la mawaziri.

Mawaziri wengine kivuli
Kwa mujibu wa Mbowe, Waziri Kivuli katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), amekuwa Raya Ibrahim Khamis, Waziri wa Uwekezaji na Uwezeshaji amekuwa Esther Matiko huku naibu wake akiwa Vicent Nyerere.

Mbowe alimteua Said Amour Arfi kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Mchungaji Israel Natse kuwa Waziri wa Mahusiano na Uratibu, huku Susan Lyimo akiteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Pauline Gekul ameteuliwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Leticia Nyerere Waziri wa Ofisi hiyo akishughulikia mazingira ambapo Zitto Kabwe amekuwa Waziri wa Fedha huku naibu wake akiwa Christina Mughwai.

Godbless Lema amekuwa Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Tundu Lissu, Katiba na Sheria, Ezekia Wenje akienda Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Joseph Selasini alipewa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Silvester Kasulumbai akiteuliwa kuongoza Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

Wengine walioteuliwa na wizara zao katika mabano ni Profesa Kulikoyela Kahigi (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Halima Mdee (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Mchungaji Peter Msigwa (Maliasili na Utalii).

Mhandisi Salvatory Machemuli ataongoza Wizara ya Ujenzi, Mhonga Ruhwanya (Wizara ya Uchukuzi), Lucy Owenya (Viwanda na Biashara), Christowaja Mtinda (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Dk Gervas Mbasa (Afya na Ustawi wa Jamii).

Pia wamo Regia Mtema (Kazi na Ajira), Naomi Kaihula (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto), Joseph Mbilinyi (Habari,Vijana na Michezo), Mustapha Akunaay (Ushirikiano wa Afrika Mashariki), Meshack Opulukwa (Kilimo, Chakula na Ushirika) na Highness Kiwia amekuwa Waziri Kivuli wa Maji.