Search This Blog

Friday, February 11, 2011

Habari zilizokatika- MUBARAK WA MISRI AACHIA NGAZI

Jeshi lashika madaraka Misri
 Field Marshal Mohammed Hussein Tantawi Soliman.
 Jeshi la Misri latwaa madaraka na mkuu wa Baraza la Juu la Kijeshi- Higher(Supreme) Military Council ni Field Marshal Mohamed Hussein Tantawi Soliman ndiye kiongozi wa serikali ya kijeshi nchni Misri:Mohamed Hussein Tantawi Soliman (Arabic: محمد حسين طنطاوى; alizaliwa 31 October 1935) 
 Jenerali Omar Suleiman aliyekuwa Makamu wa Raisi wa Hosni Mubarak:
 Kabla ya hapo alikuwa mkuu wa Idara ya Usalama wa taifa wa Misri:Omar Suleiman (Arabic: عمر سليمان, alizaliwa July 2, 1936) 
 Mkaruka huyu General Hosni Mubarak ambaye ameng'olewa na pipoz pawa, ana miaka 82
Mitaani watu weweeeeeeee!!!!!!!!!

HILI LINANIKERA SANA!!!!!!


WANAFUNZI WA VYUO VIKUU WALIANDAMANA KUPINGA MASUALA MBALIMBALI YA UTENDAJI WA SERIKALI YA CCM

 WALIANDAMANA KWA HASIRA SANA
 WAKAPIGWA MABOMU NA ASKARI 
 BAADAE SIKU CHACHE TU HATA VIDONDA HAVIJAPONA NA HATA SERIKALI HAIJATIMIZA MADAI YAO........EBU ANGALIA PICHA HAPO CHINI............
INAKERA SANA..........

Monday, February 7, 2011

MKAKATI WA MATOKEO YA FORM FOUR ULIANZIA AWAMU YA NNE

VIONGOZI wakuu wa nchi watuambie kwa nini Shule za sekondari zikachipua kama uyoga huku majengo yakiwa na nyufa, sakafu za vumbi na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikikosekana.
Shule hazina vitabu vya kutosha, maabara, maktaba, ofisi za walimu, viti, meza wala vyoo. Mbaya zaidi hakuna walimu wenye ujuzi na uwezo stahiki.
Baada ya kelele za ukosefu wa walimu, Mhe Kikwete na Lowassa wakabuni mbinu hii.... Wakaagiza shule zitafute ‘bora walimu’ vijana wa kidato cha nne na sita ili wawe wanafundisha na serikali iliteua walimu wa shule za msingi kuwa walimu wa sekondari. Lowassa akafuta kozi ya ualimu ya miaka miwili. Sasa ikawa ni kozi ya mwaka mmoja. Lakini kelele za uhaba wa walimu ziliendelea, wakatengeneza walimu wa fastafasta. Hawa ni vijana wakapewa mafunzo ya wiki nne ya ualimu kisha wakaanza kazi ya ualimu. Hapana shaka baadhi yao walikuwa wamefeli.
Matokeo yake sasa:
Matokeo wanafunzi wengi waliofanya mtihani wa kidato cha pili walifeli hivyo hawakuingia kidato cha tatu mwaka 2008.Mhe. Kikwete katika mkutano na maofisa elimu, walimu wakuu wa shule na vyuo, wataalamu wa elimu na wasomi uliofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam,  alipendekeza mitihani ya kidato cha pili na darasa la nne isiwe kikwazo katika juhudi za kuimarisha elimu. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe akatangaza bungeni mitihani hiyo miwili ‘imefutwa’. Wabunge wakashangilia na kupiga vigelegele.
Vijana walioingia kidato cha kwanza mwaka 2006 walipaswa kumaliza kidato cha nne mwaka 2009. Lakini waliofeli mtihani wa kidato cha pili mwaka 2007, walirudia darasa hilo mwaka 2008 wakawa pamoja na walioanza kidato cha kwanza 2007. Kwa kuwa, baada ya kufutwa mtihani wa kidato cha pili mwaka 2008 vilaza wote waliingia kidato cha tatu mwaka 2009 hadi kidato cha nne mwaka 2010, ni dhahiri JK na Lowassa wamefanikiwa katika Mkakati wa Matokeo ya  Elimu ya form four waliouanzisha toka  mwaka 2006.

MGOSI AIPAISHA SIMBA SC KILELENI


MSHAMBULIAJI Mussa Hassan Mgosi aliiongoza Simba kurudi kileleni mwa ligi kwa kufunga mabao mawili na kuiwezesha timu yake kushinda 2-0 dhidi ya wachezaji 10 wa Polisi Tanzania. Mgosi alifunga bao la kwanza katika ya dakika 53, kipindi cha pili kwa mpira wa adhabu wa umbali wa mita 35, baada ya Mbwana Samata kuangushwa.Mgosi alipiga faulo hiyo na mpira ulikwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Said Kombo asijue la kufanya. 

Awali katika dakika ya 44, pia Mgosi alifunga bao kwa mpira wa adhabu aliopiga nje ya eneo la 18 baada ya kuangushwa kwa Nyagawa, lakini mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza alilikataa kwa kusema mfungaji alishindwa kufuata kanuni za upigaji wa mpira huo ambao ulitakiwa uguswe na watu wawili kwanza jambo ambalo Mgosi hakufanya na timu hizo kwenda mapumziko kwa suluhu. 

Katika kipindi cha pili mshambuliaji Mussa Mgosi alifunga bao la pili katika dakika ya 84, akiunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Haruna Shamte kutoka upande wa kulia na kufikisha mabao sita katika msimu huu. 

Kwa matokeo hayo Simba imerudi kileleni baada ya kufikisha pointi  33 ikiwa na pointi moja zaidi ya Yanga iliyo na michezo zaidi ikiwa nafasi ya pili na pointi 32. 

Polisi walipata pigo katika dakika ya 63, baada ya mshambuliaji wao Semsue Juma kutolewa nje kwa kadi mbili za njano baada ya kuwachezea vibaya Amir Maftah na Kaseja katika wakati tofauti.

MATUMIZI YA MAJINA YA VIONGOZI NA WANASIASA KATIKA MASHULE YA SERIKALI NA BINAFSI LINI MWISHO WAKE?

Matumizi ya majina ya wanasiasa na viongozi kwenye mashule na taasisi mbalimbali yalianza kuwa makubwa pale Serikali ilipoanzisha kampeni kubwa ya ujenzi wa shule za sekondari ili ziweze kuchukua ongezeko kubwa la wanafunzi waliotarajiwa kuingia kidato cha kwanza. Wanasiasa na Viongozi waliona hapo ndipo mahali pa kuchukulia ujiko. Baadhi yao walishinikiza zipewe majina yao. Hata watu waliokuwa hawajatoa mchango wowote wa maana kwa jamii, walitaka shule ziitwe kwa majina yao. Ilikuwa rahisi kwao kudandia sifa kwenye shule kuliko zahanati, hospitali au barabara zilizojengwa kwa nguvu ya wananchi.

Matokeo yanaonyesha wanafunzi waliomaliza fomu four hawakufanya bidii kusoma na kupata alama nzuri kulingana na sifa za wenye majina ya shule wanazosoma. Au labda tuamini kuwa majina yaliyotumika pia yalichangia kufeli kwa wanafunzi???? Tafakari.
Shule ya Yusuf Makamba Dar es Salaam ina rekodi  ya DI=2, DII=4, DIII=19, DIV=113 na waliofeli 314; Shule ya Pius Msekwa (Mwanza) imetoa DI=1, DII=2, DIII=9, DIV=60 na waliofeli 58.  Ali Hassan Mwinyi (Tabora) DI=0, DII=3, DIII=2, DIV=38 na waliofeli 67. Cyril Chami (Kilimanjaro) DI=0, DII=0, DIII=1, DIV=22 na waliofeli 54; Mengine jaribu kuangalia NECTA. 

Viongozi ambao majina yao yametumika kwa heshima na kumbukumbu ya kazi waliyofanya, au kwa kushinikiza kwao waone wajibu wa kutoa ushauri na kusukuma mbele maendeleo ya elimu. Pia wanapaswa kuwa walezi wa shule husika.Wanasiasa hao wanapaswa kusaidia kutatua matatizo yanayokabili shule hizo ili ziwe na mazingira mazuri ya kuleta matokeo bora kila mwaka kulingana na heshima ya majina yao katika jamii.

Lakini kama hakutakuwepo na nia njema ya kuangalia maendeleo ya shule zetu ambazo zina majina ya viongozi basi SIFA hii ya kushinikiza matumizi ya majina ya viongozi na wanasiasa haitaishia hapo, itafikia hatua hata makanisa na misikiti yataitwa kwa majina yao. Usije shangaa ukaja kusikia Alli Hassan Mwinyi SDA Church, au Msikiti wa Edward Lowasa, sehemu nyingine utaweza kusikia Salima Kikwete Full Gospel Fellowship Church. 

Tunachoomba si kutoa tu majina bali kuangalia namna gani ya kuinua maendeleo ya jamii ili kuleta maisha bora kwa jamii husika. Kitu kingine hivi tabia hii ya kuita taasisi kama shule majina ya watu hata wengine ambao hawajatoa mchango wowote katika jamii itaisha lini???. Maana kila siku kuna viongozi na wanasiasa wapya wanaibuka na kila mtu atataka jina lake litumike kwenye shule ama taasisi fulani ili tu ajipatie ujiko!!!!
Nawasilisha!!!!!

Sunday, February 6, 2011

SAKATA LA DOWANS: Utetezi wa Mhe. Kikwete kwa wananchi huu hapa.


Hebu tafakari hizi nukuu za RAIS Jakaya Kikwete siku ya maadhimisho ya miaka 34 ya CCM huko Dodoma ambazo mimi nachukulia ni utetezi wake katika sakata la DOWANS.

"..Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe..,"

“Wapo wanaosema niko kimya au nashindwa kuchukua hatua, kwa sababu marafiki zangu wamehusika. Nawalinda. Kwa sababu hiyo, nikaona nami nisema angalau watu wanisikie, lakini sina la ziada ni yale yale yaliyokwishasemwa”.

 “Sikuona umuhimu wa kufanya hivyo kwa sababu viongozi wenzangu wameelezea kwa ufasaha uamuzi wa Kamati Kuu na ule wa kikao cha pamoja cha Wabunge wa CCM,”

“ Wapo waliosema lazima tulipe, wapo waliosema tusilipe, wapo waliosema tusiharakishe kulipa kwani kuna uwezekano wa kutokulipa kwa kutumia sheria,”

“ Uamuzi wangu ukawa tusiharakishe kulipa, tutafute njia za kuepuka katika kulipa. Ndiyo maana ya taarifa ya Chiligati na ile ya Waziri Mkuu,”

“ Tumewataka wanasheria wetu wasaidiane na wale wa Tanesco kuhakikisha hilo halitokei.  Nataka kuwahakikishia kuwa na mie ni miongoni mwa wale wasiotaka Tanesco ilipe,"

"Kauli za mimi kuhusika na Dowans inanishangaza, maana nisingeamua hivyo katika Kamati Kuu(CC) na Kamati ya Wabunge wa CCM.  Ama kweli akutukanae hakuchagulii tusi”

“ Sina hisa zozote wala manufaa yoyote yale, Pia sina ajizi wala kigugumizi cha kuchukua hatua kwa sababu ya rafiki yangu au hata kama angekuwa ndugu yangu kahusika.  Maamuzi yaliyofanywa na Kamati Kuu na Kamati ya Chama ya Wabunge wa CCM yalifanywa chini ya uongozi wangu,”

Ukifuatilia kauli hizo kuna kauli nyingi za Mhe Kikwete ambazo kama Rais hakustahili kuzisema, mojawapo ya ,ni kauli yake ya kwamba pamoja na kumsifu sana Nyerere lakini alishindwa kutatua changamoto nyingi katika utawala wake na hivyo hivyo kwa marais wengine waliomtangulia, sembuse mimi (Kikwete). Alisema hayo akijitetea kwamba yeye sio wa kwanza kushindwa kuondoa matatizo ya watanzania.

Huu ni utetezi RAHISI mno kwa jinsi alivyoshindwa kutatua matatizo ya watanzania. Sio tu Mhe.Kikwete ameshindwa kutatua matatizo bali ameyaongeza na kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu zaidi. Mwl.Nyerere alijenga umoja wa kitaifa na alijenga uwajibikaji kwa watumishi wa umma kitu ambacho Kikwete ameshindwa. Mzee Ruksa aliruhusu uchumi wa soko ambao ulisaidi kufanya upatikanaji wa bidhaa muhimu ambazo mwanzo zilionekana kama anasa. Mzee Mkapa akajitahidi kujenga uchumi imara bila kusahau miundo mbinu na kurudisha heshima ya wafanyakazi. Pamoja na mapungufu yao viongozi waliopita wanayo ya kujivunia.

Kipindi hiki hakina umoja wa kitaifa, kuna makundi ndani ya CCM, matumizi makubwa serikalini, kuendekeza ununuaji wa magari ya kifahari yasiyo na tija, gharama za maisha zimepanda mno, thamani ya shilingi imeshuka sana, mfumuko wa bei hauelezeki, mitandao ya wizi mfano wizi wa EPA, mfumo wa elimu ni mbovu kwa kuanzisha kisiasa shule za kata zisizo na walimu wala vifaa nya kutosha hasa vya sayansi,

Mhe Kikwete amekiri na ameweka bayana Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni au Richmond in kampuni hewa. MASWALI: Kama hii ni kweli anatuambiaje kuhusu matokeo ya TAKUKURU waliosema kuwa Richmond haikuwa na shida? Kama ilikuwa kampuni hewa kwa nini aliruhusu ikauza mkataba na DOWANS na mkataba uleule ukatumika na Tanesco?
Je watendaji wenzake wa Serikali na CCM waliosema deni la Dowans halikwepeki walikuwa na maana gani kama yeye hataki deni lilipwe?
Je kama hakuona umuhimu wa kutoa tamko wakati watendaji wake wanatofautiana kauli, je ni nani aliyekuwa na kauli ya mwisho katika sakata hili?

Mimi ninaona nchi hii inahitaji sana mabadiriko ya namna ya kushughulikia masuala ya jamii.

Saturday, February 5, 2011

HIZI NOTI MPYA NI NOTI KWELI? AU NI BATIKI?

BoT yatetea noti zake mpya zilizotolewa za 'batiki'
Maswali ya kujiuliza:
1. Hivi kwa nini hadi zisuguliwe ndo tujue uhalali wa noti??
2. Je watasugua wangapi maana kama noti ikisuguliwa sana ndo itachanika mapema?
3. Hebu angalia noti hizo hapo chini. Mbona zikisuguliwa hazitoi rangi?? Au nazo hazikuwa halali?

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa ufafanuzi kuhusu kuchuja rangi  katika
noti mpya zilizotolewa hivi karibuni na kusema kuwa hali hiyo ni ya kawaida kwa noti zilizochapwa kwa teknolojia maaluum ijukanayo kama 'Intaglio Printing'

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu, alisema aina hiyo ya uchapishaji unafanya noti kuwa na hali ya mparuzo zinapopapaswa na imetumika ili kuimarisha kingo za noti kwa lengo la kupunguza uwezekano wa kuchanika na kuchakaa kwa haraka.

Prof. Ndulu alisema miparuzo hiyo huacha rangi noti inaposuguliwa kwa nguvu kwenye karatasi nyeupe kitendo ambacho kinathibitisha kuwa noti hiyo ni halali.

"Kutoa rangi ni moja ya alama ya usalama inayothibitisha kuwa noti siyo bandia, noti hizi hazichuji zikilowekwa kwenye maji kama inavyodaiwa kwa kuwa wino uliotumika hauyeyuki kwenye maji,"alisema Prof.Ndulu

Prof.Ndulu alisema kuwa utowaji rangi huo upo hata katika noti za nje kama dola pale zinaposuguliwa ambapo teknolojia iliyotumika kutengezewewa inalingana.

Alisema kuwa noti hizo zimetengenezwa kwa teknolojia ya kuwekewa kinga dhidi ya uchafu ili kupunguza uwezekano kunasa uchafu inapokuwa katika mzunguko.

Aliongeza kuwa noti za zamani bado ni halali na zitaendelea kutumika pamoja na zile mpya mpaka zitakapopotea katika mzunguko kwa sababu ya uchakavu wake.

Akizungumzia hoja ya kuwepo noti mmoja iliyo na thamani kubwa zaidi ya ile ya sasa ya sh.10,000/-, Prof. Ndulu  alisema BoT haikuona haja ya kufanya hivyo kwakuwa malipo makubwa yanahimizwa kufanywa kupitia njia nyingine za kibenki kama njia ya mitandao.

Katika siku za karibuni wananchi mbalimbali wamekuwa wakilalamika na kuhofia teknolojia iliyotumika kutengeza noti mpya zilizotolewa hivi karibuni.

Noti hizo ambazo ni ya 10,000/-, 5,000/-, 2000/-, na  1,000/- zilipokelewa kwa shingo upande baada ya kuingizwa kwenye mzunguko na BoT huku wengine wakidai zimetengenezwa kwa teknolojia dhaifu na kulinganisha na upikaji vitenge aina ya batiki.

Hali hiyo imesababisha watu wengi kutokuwa na imani nazo huku yakiwepo matukio ya msuguano katika maeneo mbalimbali ya biashara ka baadhi ya watu kuzikataa pale wanaporudishiwa chenji hususani muda wa usiku.

Hata wale wanaozipokea saa za mchana wamekuwa na mashaka nazo na kuziangalia mara mbili mbili huku wengine wakilalamika kwamba zimetengenezwakwa teknolojia ya chini inayopunguza hadhi ya noti hizo. 

HILI NDILO JESHI LETU LINAVYOLINDA RAIA

CHANZO CHA MATOKEO MABAYA YA FOMU FOO HIKI HAPA

WANAFUNZI WENGI HUTOROKA VIPINDI VYA MASOMO.

OFFICE ZOTE ZINGEKUWA HIVI....

Hii imekaaje???

Hata kama shughuli haijamalizika , lakini akigeuka kuangalia nyuma shughuli itamalizika mapeeeeeemaaa!!!!

MDAU WANGU KAKOSWAKOSWA KULIWA NA NYOKA!!!!

Nyoka aliingia ndani.....sijui alitokea wapi!!!!!!!!

Hapo palipotuna tayari ameshameza panya kadhaa ila bado anamnyemelea mdau wangu Mr. Steve huko Igoma Mwanza
Mpambano ukawa mkali ikabidi mdau wangu Mr. Steve amchome na moto kuepusha balaa

HII INAASHIRIA NINI? JE UENEZI WA SIASA?


Tuesday, February 1, 2011

CHADEMA YAWEKA WAZI SABABU ZA KUTOUNGANA NA CUF

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kuwa hakiwezi kushirikiana na vyama vingine vya upinzani bungeni kwa kuwa vyama hivyo vimeungana na CUF ambayo 'imefunga ndoa' na CCM na kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dk Slaa alisema Kamati Kuu ya Chadema imeona kuwa chama hicho hakiwezi kuwa na ushirikiano wenye tija na vyama hivyo bungeni, hivyo imemwagiza kiongozi wa kambi ya upinzani kuunda baraza kivuli la mawaziri kwa kuwahusisha wabunge wa Chadema pekee. "Kamati Kuu imeendelea kuzingatia umuhimu wa vyama vya siasa kushirikiana katika kuimarisha nguvu ya upinzani hapa nchini. Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa CUF na CCM wamejiunga kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na kwa kuwa sheria inayoruhusu uwepo wa vyama vya siasa inahusu pande zote za Muungano, inaamini kuwa CCM na CUF ni wamoja hata huko, (Bara),"alisema Dk Slaa.

Dk Slaa alisema hayo alipokuwa akieleza maazimio ya Kamati ya Chadema iliyokutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

MCHAKATO WA KATIBA MPYA
Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya, Dk Slaa alisema kamati hiyo ilipinga utaratibu uliotangzwa na Rais Jakaya Kikwete wa kuunda tume kwa kuwa hiyo siyo njia sahihi ya kutungwa kwa katiba mpya.

Alisema njia sahihi ambayo kamati hiyo iliona ni ile itakayowashirikisha wananchi kikamilifu na kwa dhati bila kujali tofauti zao za kisiasa, dini, kabila, umri, elimu,wala jinsia.

"Kamati Kuu imejadili na kutafakari kwa kina maoni ya wadau mbalimbali juu ya mchakato unaofaa katika kupata katiba mpya na kuzingatia kuwa njia sahihi ni ile itakayowashirikisha wananchi,"alisema Dk Slaa na kuongeza:
 
"Aidha, Kamati Kuu imezingatia kwamba kuunda tume ya rais siyo njia sahihi itakayowezesha upatikanaji wa katiba mpya yenye kuzingatia utashi, matakwa na mahitaji ya wananchi wa Tanzania."

Alisema kutokana na hali hiyo, kamati hiyo iliunga mkono utaratibu wa kutumia Bunge katika kutengeneza na kusimamia mchakato wa upatikanaji wa katiba hiyo huku ikipongeza uamuzi wa sekretariati yake kwa kumuagiza Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika kuwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu katiba.

Dk Slaa alitoa wito kwa wabunge wote kuunga mkono hoja hiyo ili iweze kupita na kuruhusu mabadiliko yatakayowezesha kulifikisha taifa kwenye katiba mpya na bora kwa maslahi ya umma.

 VURUGU ZA ARUSHA
Akizungumzia suala la vurugu za Arusha, Dk Slaa alisema Kamati Kuu ilipokea kwa masikitiko vifo vya raia watatu waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi katika juhudi za kuzuia maandamano halali yaliyoandaliwa na chama hicho.

Alisema kamati ilimtupia lawama Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha kwa kuvuruga uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha na inaamini mkurugenzi huyo alifanya hivyo kwa maelekezo ya CCM. Dk Slaa alisema kamati iliwapa pole familia za wafiwa wote na kumpongeza mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha, Godbles Lema kushiriki na wafiwa wakati wote wa maombolezo ya msiba huo.

Alisema kamati hiyo imewaagiza madiwani wa Chadema wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kuendelea kuhudhuria vikao vya baraza la madiwani na kuwawakilisha wananchi waliowachagua na pia kuhakikisha wanatumia nafasi yao kufanikisha uchaguzi wa meya unafanyika.

MAANDAMANO YA KUPINGA MALIPO YA DOWANS
Kuhusu Dowans, Dk Slaa alisema kamati ilielezea masikitiko yake ya kupanda kwa gharama za umeme na nishati za gesi nchini na kusisitiza kuwa maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho nchi nzima yako paleple na yataanza Februari 24 katika Jiji la Mwanza.  Alisema pamoja na mambo mengine, maandamano hayo yanapinga malipo ya fidia kwa kampuni ya Dowans ambayo tayari CCM imeridhia.

"Kamati Kuu imesikitishwa na kufadhaishwa na uamuzi wa CCM na Serikali yake wa kuridhia kuilipa Kampuni hewa ya Dowans fedha za walipa kodi Sh94 bilioni pamoja na kwamba kampuni hii Ilishaharamishwa na Bunge kwa niaba ya Watanzania.

Kamati Kuu imetambua kuwa sakata la Dowans ni mwenendelezo wa vitendo vya kifisadi ndani ya CCM na Serikali yake ambavyo vimelighalimu taifa,"alisema Dk Slaa.

Alisema kamati hiyo iliwahimiza wabunge wa Chadema na wananchi wote kuendelea kupinga malipo ya Dowans na kuwataka wabunge hao kuendelea kuwahamisha wananchi kupinga malipo hayo kwa njia ya kisiasa na kisheria.

Aidha, Dk Slaa alitaka Serikali ya CCM kuchota sera nzuri za Chadema zinazohusu uboreshaji wa nishati ya umeme na kuzitumia kwa masilahi ya Taifa.

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NI JANGA LA KITAIFA
Katika hatua nyingine, Chadema imetangaza matokeo ya kidato cha nne kuwa ni janga la kitaifa. "Kamati Kuu imezingatia na kusikitishwa kuona kuwa ni asilimia 11.5 tu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa Kidato cha Nne ndio waliofauli. Ndio kusema karibu asilimia 90 ya vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2010 hawawezi kuendelea na masomo ya elimu ya juu na itakuwa vigumu kwa vijana hawa kupata ajira yoyote ya uhakika,"alisema.

UDINI
Kuhusu suala la udini,  katibu huyo alisema Kamati Kuu Ilipokea taarifa hiyo kwa masikitiko na kwamba hoja hiyo ya propaganda Iliyolenga kuwarubuni Watanzania na kuwaonda kwenye mchakato wa kuajdili hoja za msingi za kitaifa.

"Kamati Kuu imezingatia kuwa viongozi wa juu wa CCM wameamua kuficha udhaifu wao wa kioungozi kwenye kivuli chini ya zulia la udini ili wananchi waache kujadili mambo yamsingi ya Taifa ikiwemo kushindwa kwa CCM kutekeleza ahadi ilizoahaidi kwa wananchi wake,"alisema Slaa.


Sunday, January 23, 2011

CHADEMA NA MCHAKATO WA KATIBA MPYA: Mkutano wa hadhara DSM

Katibu Mkuu Dr. Slaa akisalimiana na wananchi

 Mwanzilishi wa Mageuzi Nchini Tanzania Mabere Marando ambaye kwa sasa ni mwanachama wa Chadema akiwasalimia mamia ya wananchini waliofurika kwenye mkutano wa hadhara viwanja vya mtaa wa mwongozo Makuburi-Mabibo  Dar es Salaam
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye pia ni naibu katibu mkuu wa chadema Zitto Kabwe akimwaga cheche kwenye mkutano huo na ulioudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mbalimbali na Mamia ya  wananchi
 Wananchi wakirudisha kadi za CCM na kujiunga CHADEMA
 Sehemu ya umati wa watu
"Narudisha kadi ya CCM najiunga CHADEMA leo"

Friday, January 21, 2011

MIKIKI MIKIKI!!!!!!!!!! NINAWATAKIA WIKENDI NJEMA!!!!!!!

IKO WAPI INTELIJENSIA YA POLISI??


MFUMO wa Polisi, vyombo vingine vya ulinzi na usalama na serikali,wa kukusanyia na kusafirishia taarifa, hasa za “usalama,” ujulikanao kama intelijensia una walakini.
Said Mwema, inspekta jenerali wa polisi (IGP), alisema alikuwa na “taarifa za kiintelijensia” kuwa kutatokea vurugu iwapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kitafanya maandamano mjini Arusha.
Iko wapi intelijensia ya polisi isiyoweza kuona Mafisadi na kuwakamata wanaounda makampuni na kuiba mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu na Hazina?
Iko wapi Intelijensia ya IGP Mwema isiyoweza kujua mmiliki wa Dowans na ndugu yake Richmond? Kwa nini inteligensia ya Mwema isizuie malipo ya mabilioni ya shilingi kufidia kisichoeleweka wakati wahusika wapo?
Au hii Intelijensia ni kwa Chadema tu????????????????

Friday, January 7, 2011

CCM NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA


Josephine Mushumbushi.

Matumizi ya nguvu yaliyofanywa na Serikali ya CCM mjini Arusha yamedhihilisha unyanyasi wa kijinsia wa hali ya juu sana. Pichani anaonekana mwanamke (Mchumba wa Dr. Slaa) aliyepigwa sana na Polisi hadi kupasuka kichwa na kuvuja damu kama anavyoonekana. Hebu iangalie picha kwa umakini uone ni kiasi gani cha damu iliyomwagika. 
Sidhani kama kweli akina mama wa aina hii hapa Tanzania wanaweza kuwa na vurugu hadi kusababisha askari kuwapiga kwa kutumia silaha za moto. Wanawake wengi walianguka mitaroni, kupigwa na risasi za moto, kupigwa mabomu ya machozi,  kumwagiwa maji ya pilipili ikiwa ni kuwadhalilisha na kuwanyanyasa. Baada ya kujeruhiwa vibaya, Mushumbushi na wanawake wengine walienda Polisi kuchukua PF3 kama haki ya kila mtanzania - matokeo yake wakawekwa rumande na kuendelea kuteseka kwa maumivu makali. 
Mhe.Lucy Owenya baada ya kipigo alizirai na kuokolewa na wananchi ambao walikuwa wanakimbia kuokoa roho zao. Gari la Mbunge wa Viti maalumu Mjini Moshi, Mhe Grace Kihweru liliharibiwa na Askari. Akina mama waliokuwepo kwenye maandamao hawakuwa na silaha za kuwatishia polisi. Kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kinasikitisha.

Blog hii inawapa pole wanawake wote walioathirika na ukatiri wa serikali ya CCM.

Thursday, January 6, 2011

KAMA TULIVYOTARAJIA NA WENGI: CHADEMA YACHUKUA UMEYA, NA UNAIBU MEYA JIJI LA MWANZA.

 Hatimaye jiji la Mwanza leo limepata Meya wake mpya baada ya kura za Madiwani wapatao 32 kupigwa nazo kuhesabiwa na hatimaye diwani wa kata ya Nyakato bw. Josephat Manyerere wa CHADEMA kutangazwa kuwa ndiye meya mpya wa jiji la Mwanza.

Akitangaza matokeo ya umeya Mwanza, msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mkurugenzi wa jiji bw. Wilson Kabwe amemtaja Bw. Stanslaus Mabula (CCM) kuwa amepata kura 15, na Bw. Josephat Manyerere (CHADEMA) akiibuka mshindi kwa kupata kura 17.
Mjengoni jiji la Mwanza
Huyu ndiye meya mpya wa jiji la Mwanza kupitia CHADEMA Bw.Josephat Manyerere(kulia) akipongezwa na mbunge wa Nyamagana Mh.Wenje, na kwa chati pembeni ni diwani wa Mwaloni Kirumba Bw.Novat Manoko.


Mhe. Wenje akipongezana na Mhe. Zito Kabwe

Mara baada ya mchakato wa kumpata Meya kumalizika na mshindi kutajwa, ungwe iliyofuata ikawa ni kumsaka Naibu Meya ambapo kulikuwa na wagombea wawili nayo matokeo yakataja kuwa diwani Charles Marwa Chichibela (pichani mwenye suti) kutoka CHADEMA ameibuka kidedea kwa kuzinyakua kura 17, dhidi ya 15 za Daudi Mkama wa CUF.

KIKWETE KUHUDHURIA MAZISHI YA WAIOUAWA ARUSHA????

Inasemekana watu takribani kumi (10) wameuawa katika maandamano yaliyofanyika jana terehe 5/1/2011 Arusha. Katika maandamano hayo ambayo inasemekana CHADEMA walikuwa na barua ya kuwaruhusu toka kwa Msajili wa vyama vya siasa ambaye aribariki maandamano hayo. hata hivyo kisheria IGP alitakiwa aandikie barua CHADEMA kubatilisha ile ya awali then wangeandamana ingekuwa ukaidi. 


Demokrasia ni ghali na ina gharama yake, HAKI SAWA KWA WOTE, Vyama vya Siasa vimeandikishwa kisheria na vina wanachama waadilifu , Na ni hiari yao kuwa wanakutana bila kuvunja sheria. Ni kosa wanapoonewa bila sababu ya Msingi.Huwezi kuwazuia kuandamana kama wana kibali, hii ni kuleta Siasa za CHUKI, CHUKI Haina Nafasi.


Kitendo cha polisi kujiingiza katika siasa na kukataza mara kwa mara mikutano na maandamano ya Chadema, ni moja ya ukiukwaji wa haki za binadamu.Polisi wamemwaga damu, wamekamata hadi wabunge akiwemo kiongozi wa upinzani bungeni (Freeman Mbowe).


JE, Kikwete atahudhulia mazishi ya hawa wapendwa wetu waliouawa Arusha na Polisi wake?????.

VIONGOZI WA CHADEMA WAKAMATWA KUTOKANA NA MAANDAMANO ARUSHA

Viongozi wa CHADEMA

Polisi wakizuia maandamano
Maeneo ya Unga Limited palikuwa hapatoshi

MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.

VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.

HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE.

AIDHA HABARI ZINADATISHA KWAMBA JIJI LA ARUSHA LINARINDIMA KWA MPAMBANO WA KUKIMBIZANA WA POLISI NA MAKUNDI YA WATU WANAODAIWA KUTAKA KWENDA KITUO CHA POLISI KUWATOA WALIOKAMATWA KWA NGUVU.

Kabla ya kukamatwa.............

Mh. Freeman Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.

Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.

"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe.