Search This Blog

Monday, February 7, 2011

MGOSI AIPAISHA SIMBA SC KILELENI


MSHAMBULIAJI Mussa Hassan Mgosi aliiongoza Simba kurudi kileleni mwa ligi kwa kufunga mabao mawili na kuiwezesha timu yake kushinda 2-0 dhidi ya wachezaji 10 wa Polisi Tanzania. Mgosi alifunga bao la kwanza katika ya dakika 53, kipindi cha pili kwa mpira wa adhabu wa umbali wa mita 35, baada ya Mbwana Samata kuangushwa.Mgosi alipiga faulo hiyo na mpira ulikwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha kipa Said Kombo asijue la kufanya. 

Awali katika dakika ya 44, pia Mgosi alifunga bao kwa mpira wa adhabu aliopiga nje ya eneo la 18 baada ya kuangushwa kwa Nyagawa, lakini mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza alilikataa kwa kusema mfungaji alishindwa kufuata kanuni za upigaji wa mpira huo ambao ulitakiwa uguswe na watu wawili kwanza jambo ambalo Mgosi hakufanya na timu hizo kwenda mapumziko kwa suluhu. 

Katika kipindi cha pili mshambuliaji Mussa Mgosi alifunga bao la pili katika dakika ya 84, akiunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Haruna Shamte kutoka upande wa kulia na kufikisha mabao sita katika msimu huu. 

Kwa matokeo hayo Simba imerudi kileleni baada ya kufikisha pointi  33 ikiwa na pointi moja zaidi ya Yanga iliyo na michezo zaidi ikiwa nafasi ya pili na pointi 32. 

Polisi walipata pigo katika dakika ya 63, baada ya mshambuliaji wao Semsue Juma kutolewa nje kwa kadi mbili za njano baada ya kuwachezea vibaya Amir Maftah na Kaseja katika wakati tofauti.

No comments:

Post a Comment