Search This Blog

Thursday, January 6, 2011

VIONGOZI WA CHADEMA WAKAMATWA KUTOKANA NA MAANDAMANO ARUSHA

Viongozi wa CHADEMA

Polisi wakizuia maandamano
Maeneo ya Unga Limited palikuwa hapatoshi

MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.

VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.

HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE.

AIDHA HABARI ZINADATISHA KWAMBA JIJI LA ARUSHA LINARINDIMA KWA MPAMBANO WA KUKIMBIZANA WA POLISI NA MAKUNDI YA WATU WANAODAIWA KUTAKA KWENDA KITUO CHA POLISI KUWATOA WALIOKAMATWA KWA NGUVU.

Kabla ya kukamatwa.............

Mh. Freeman Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.

Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.

"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe. 

No comments:

Post a Comment