Search This Blog

Thursday, January 6, 2011

KAMA TULIVYOTARAJIA NA WENGI: CHADEMA YACHUKUA UMEYA, NA UNAIBU MEYA JIJI LA MWANZA.

 Hatimaye jiji la Mwanza leo limepata Meya wake mpya baada ya kura za Madiwani wapatao 32 kupigwa nazo kuhesabiwa na hatimaye diwani wa kata ya Nyakato bw. Josephat Manyerere wa CHADEMA kutangazwa kuwa ndiye meya mpya wa jiji la Mwanza.

Akitangaza matokeo ya umeya Mwanza, msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mkurugenzi wa jiji bw. Wilson Kabwe amemtaja Bw. Stanslaus Mabula (CCM) kuwa amepata kura 15, na Bw. Josephat Manyerere (CHADEMA) akiibuka mshindi kwa kupata kura 17.
Mjengoni jiji la Mwanza
Huyu ndiye meya mpya wa jiji la Mwanza kupitia CHADEMA Bw.Josephat Manyerere(kulia) akipongezwa na mbunge wa Nyamagana Mh.Wenje, na kwa chati pembeni ni diwani wa Mwaloni Kirumba Bw.Novat Manoko.


Mhe. Wenje akipongezana na Mhe. Zito Kabwe

Mara baada ya mchakato wa kumpata Meya kumalizika na mshindi kutajwa, ungwe iliyofuata ikawa ni kumsaka Naibu Meya ambapo kulikuwa na wagombea wawili nayo matokeo yakataja kuwa diwani Charles Marwa Chichibela (pichani mwenye suti) kutoka CHADEMA ameibuka kidedea kwa kuzinyakua kura 17, dhidi ya 15 za Daudi Mkama wa CUF.

No comments:

Post a Comment