Search This Blog

Monday, February 7, 2011

MKAKATI WA MATOKEO YA FORM FOUR ULIANZIA AWAMU YA NNE

VIONGOZI wakuu wa nchi watuambie kwa nini Shule za sekondari zikachipua kama uyoga huku majengo yakiwa na nyufa, sakafu za vumbi na vifaa vya kujifunzia na kufundishia vikikosekana.
Shule hazina vitabu vya kutosha, maabara, maktaba, ofisi za walimu, viti, meza wala vyoo. Mbaya zaidi hakuna walimu wenye ujuzi na uwezo stahiki.
Baada ya kelele za ukosefu wa walimu, Mhe Kikwete na Lowassa wakabuni mbinu hii.... Wakaagiza shule zitafute ‘bora walimu’ vijana wa kidato cha nne na sita ili wawe wanafundisha na serikali iliteua walimu wa shule za msingi kuwa walimu wa sekondari. Lowassa akafuta kozi ya ualimu ya miaka miwili. Sasa ikawa ni kozi ya mwaka mmoja. Lakini kelele za uhaba wa walimu ziliendelea, wakatengeneza walimu wa fastafasta. Hawa ni vijana wakapewa mafunzo ya wiki nne ya ualimu kisha wakaanza kazi ya ualimu. Hapana shaka baadhi yao walikuwa wamefeli.
Matokeo yake sasa:
Matokeo wanafunzi wengi waliofanya mtihani wa kidato cha pili walifeli hivyo hawakuingia kidato cha tatu mwaka 2008.Mhe. Kikwete katika mkutano na maofisa elimu, walimu wakuu wa shule na vyuo, wataalamu wa elimu na wasomi uliofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza, Dar es Salaam,  alipendekeza mitihani ya kidato cha pili na darasa la nne isiwe kikwazo katika juhudi za kuimarisha elimu. Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe akatangaza bungeni mitihani hiyo miwili ‘imefutwa’. Wabunge wakashangilia na kupiga vigelegele.
Vijana walioingia kidato cha kwanza mwaka 2006 walipaswa kumaliza kidato cha nne mwaka 2009. Lakini waliofeli mtihani wa kidato cha pili mwaka 2007, walirudia darasa hilo mwaka 2008 wakawa pamoja na walioanza kidato cha kwanza 2007. Kwa kuwa, baada ya kufutwa mtihani wa kidato cha pili mwaka 2008 vilaza wote waliingia kidato cha tatu mwaka 2009 hadi kidato cha nne mwaka 2010, ni dhahiri JK na Lowassa wamefanikiwa katika Mkakati wa Matokeo ya  Elimu ya form four waliouanzisha toka  mwaka 2006.

No comments:

Post a Comment