Search This Blog

Friday, January 7, 2011

CCM NA UNYANYASAJI WA KIJINSIA


Josephine Mushumbushi.

Matumizi ya nguvu yaliyofanywa na Serikali ya CCM mjini Arusha yamedhihilisha unyanyasi wa kijinsia wa hali ya juu sana. Pichani anaonekana mwanamke (Mchumba wa Dr. Slaa) aliyepigwa sana na Polisi hadi kupasuka kichwa na kuvuja damu kama anavyoonekana. Hebu iangalie picha kwa umakini uone ni kiasi gani cha damu iliyomwagika. 
Sidhani kama kweli akina mama wa aina hii hapa Tanzania wanaweza kuwa na vurugu hadi kusababisha askari kuwapiga kwa kutumia silaha za moto. Wanawake wengi walianguka mitaroni, kupigwa na risasi za moto, kupigwa mabomu ya machozi,  kumwagiwa maji ya pilipili ikiwa ni kuwadhalilisha na kuwanyanyasa. Baada ya kujeruhiwa vibaya, Mushumbushi na wanawake wengine walienda Polisi kuchukua PF3 kama haki ya kila mtanzania - matokeo yake wakawekwa rumande na kuendelea kuteseka kwa maumivu makali. 
Mhe.Lucy Owenya baada ya kipigo alizirai na kuokolewa na wananchi ambao walikuwa wanakimbia kuokoa roho zao. Gari la Mbunge wa Viti maalumu Mjini Moshi, Mhe Grace Kihweru liliharibiwa na Askari. Akina mama waliokuwepo kwenye maandamao hawakuwa na silaha za kuwatishia polisi. Kitendo cha polisi kutumia nguvu kubwa kupita kiasi ni ukiukwaji wa haki za binadamu na kinasikitisha.

Blog hii inawapa pole wanawake wote walioathirika na ukatiri wa serikali ya CCM.

No comments:

Post a Comment