Search This Blog

Monday, November 22, 2010

SITASHANGAA HAYA KUTOKEA TANZANIA


Mimi sitashangaa yafuatayo kutokea:

Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kusikitishwa na uteuzi wa nafasi mbalimbali utakaofanywa na JK... utasikia wanasema du kawaweka maswahiba wake.
Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kulalamikia rushwa kushamiri Tanzania .. kama kwamba walikosa mbadala wa kumweka uongozini kupambana na rushwa kwa umakini zaidi ..
Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuanza kulalamikia hali ngumu ya maisha.. ngoja nitoe scenario moja: Chadema wana sera ya elimu bure hadi kidato cha sita (6) kama si chuo kikuu. lakini sitashangaa walioinyima kura Chadema kuanza kuja kwako kukupigia magoti kuomba msaada wa kifedha ili apate ada ya kumpeleka mtoto sekondari. Wakati walikataa kuichagua iondoe hiyo kero. Sitashangaa elimu ya namna hii ikiendelea kutolewa na CCM huku wanachi wakishangilia ati CCM oyeeeeee!!

Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM waliokuwa wanavaa sare na kucheza kama hawana akili nzuri wakati wa mikutano ya kampeni kuendelea kuwa katika hali zao duni............ why? kwa sababu serikali imeshindwa kuwa na dira endelevu.
Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuendelea kuishi katika nyumba za mbavu za mbwa  wakati wamekataa kumpigia kura Dr. Slaa aliyekuwa ameahidi kushusha bei ya saruji (cement) ili wananchi walio wengi waweze kujenga nyumba imara na bora

Sitashangaa wanachi mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia ukosefu wa dawa hospitalini..
Sitashangaa wananchi na mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia utendaji mbovu wa idara mbalimbali za serikali (kumbuka jinsi Clouds walivyokuwa wanachambua utendaji mbovu wa idara mbalimbali e.g. EWURA, DAWASCO, TANESCO lakini wakawa vuvuzela wa CCM wakati wa uchaguzi)
Sitashangaa wapenzi wa CCM kulalamikia mishahara wanayopata na wakati huo huo kulalamikia posho kubwa za viongozi wakati wao maisha ni magumu hata kushindwa kuendesha biashara zao na kuinua kipato

Sitashangaa watu hawa kuvaa ma- Tshirt, kofia na kanga 2015 kushangilia na kushabikia CCM wakati wa uchaguzi mwingine.

Kutokana na hili naomba tushirikiane pamoja kuzidi kutoa elimu ya uraia, ipo siku yatabadilika ... "MAFISADI YANA MWISHO" Dr Slaa.

Saturday, November 20, 2010

AJALI HAINA KINGA

Familia yangu tulipata ajali juzi maeneo ya Nundu-Buzuruga, Nyakato Mwanza, kijana wangu kamanda jr (7months) ndo alivunjika mguu wa kulia kama anavyoonekana hapo. Tulipata matibabu mazuri Bugando hospital kwa sasa hali zinaendelea poa. Tuombeane uzima na kupona kwa haraka. 
We surrender all to God.

Wednesday, November 17, 2010

EID MUBARAK

KWA WANABLOG WANGU....NINAWATAKIA SIKUKUU NJEMA YA EID.

EID MUBARAK

Tuesday, November 16, 2010

BREAKING NEWS !!!! MIZENGO PINDA NDIYE WAZIRI MKUU

Mhe. Mizengo Pinda "Mtoto wa Mkulima"
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK. JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEMTEUA MH. MIZENGO KAYANDA PINDA KUWA WAZIRI MKUU, KWA MUJIBU WA TANGAZO LILILOSOMWA BUNGENI SASA HIVI NA SPIKA WA BUNGE MH. ANNE ABDALLAH.

ZOEZI LINALOFUATA SASA NI WABUNGE KUMTHIBITISHA WAZIRI MKUU KWA KURA YA PAPO KWA PAPO NA BAADAYE UTAFUATIA UCHAGUZI WA NAIBU SPIKA AMBAYE ATAJULIKANA LEO PIA.

WAZIRI MKUU ANATARAJIWA KUAPISHWA KESHO IKULU NDOGO YA CHAMWINO, IKIWA NI HATUA YA KWANZA KABLA YA KUTANGAZWA KWA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI. HATUA HII INAKAMILIKA BAADA YA RAIS KUKAA NA KUSHAURIANA NA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.

BARAZA HILO JIPYA LINATARAJIWA KUTANGAZWA IJUMAA

HAWA WANAFAA KUWA WAZIRI MKUU..LAKINI.....

Hawa waheshimiwa - Mwandosya, Magufuli, Tibaijuka na Pinda pia Edward Lowassa na Dr. Harrison Mwakyembe wanafaa kwa nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa kuwa wana ushawishi katika siasa za Tanzania.

Mwakyembe: 
Alionekana ana uwezo, msomi aliyebobea na ambaye CCM wapiga debe wake (kundi linalomtetea) wamekuwa wakishinikiza apewe nyundo kumaliza ufisadi maana wananchi walivutiwa sana na jinsi kamati yake ilivyokuwa mstari wa mbele kushughulikia issue ya UFISADI. Kwa bahati mbaya ameondolewa kwa kuhofia upinzani atakaoupata kutoka kwa wababe wa siasa za bongo  na wafanyabiashara wanaoisaidia CCM

Lowassa:
Anajulikana kwa makeke yake; haiba na mvuto kwa jamii. Ni swahiba wa JK na ana ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM. Kinachomkwaza JK kumchukua, japo anatamani sana kumrejesha tena ni ile kashfa ya Richmond! Inasemekana JK anataka kutumia kigezo cha idadi nyingi za kura alizopata jimboni kwake kuonyesha kwa watanzania kuwa bado Lowasa anakubalika. Kuna kundi linaloongozwa na viongozi wastaafau wanaopinga hili kutokea....JK anahofia kwamba akimchukua CCM itamomonyoka!

Pinda:
Ndiye PM kwa sasa, kulingana na hali ya kisiasa ilivyop, jinsi CCM ilivyoaibishwa kwenye uchaguzi JK anaona Pinda si mtu wa aina anayoitaka pale. Anadhani Pinda ni muoga na mkimya sana, anataka mchapakazi, anayeogopewa na mwenye ushawishi katika siasa za Bongo! Kitendo cha PM kulia bungeni, kukili kwamba anawaogopa mafisadi nk vinamfanya JK akose imani na Pinda. Inasemekana pia kwamba wakati wa kampeni za urais Pinda yeye hakujishughulisha kukisaidia chama, aliamua kukaa pembeni kutokujihusisha na uchakachuaji, kitu ambacho JK anakiona kama ni usaliti! 

Mwandosya:
Vyanzo vyetu vinadai kwamba Mark Mwandonsya hana ushawishi kwa baadhi ya vigogo wa chama chake, na kwa wananchi. Washauri wa JK wameona kumpa nyundo huyo kutadhoofisha makali ya Serikali na kumuongezea mzigo JK....kitu ambacho kitaweka wazi mapungufu ya Rais.

Tibaijuka:
Hadi sasa anaongoza katika list, JK anataka kumpa nyundo mama huyu nguli amabaye ameonyesha ukomavu wa kisiasa na mwenye upeoo mkubwa sana katika anga za kimataifa! Kundi kubwa la vigogo wa Chama wanamtaka mama huyu amabaye anakubalika sana pia katika maeneo ya maziwa makuu. Inasemekana JK anatatizwa na kitu kimoja tu...tayari Dr. Asha Rose Migiiro ametajwa na ameshaombwa kuja kuomba urais kupitia CCM (2015) na tayari ameonyesha nia;sasa endapo PM akiwa Tibaijuka itakuwa vigumu kwa Rais na PM wake wote kuwa wanawake 2015!! Mbaya zaidi inasemekana pia Tibaijuka ana mpango wa kuomba kiti cha urais 2015!! Kwa taarifa tu ni kwamba uamauzi wa Dr Migiro ndiyo utaamua kama Tibaijuka apewe u-PM au la! Endapo atakuwa PM ina maana Dr. Migiro hatarejea kugombea 2015...ili kumpisha Tibaijuka abanjuke na upresidaa!!

Magufuli:
JK, washauri wake, CCM na wapinzani hawana hoja against huyu jamaa. Kila mmoja anajua kwamba ni mchapakazi, msomi na hana woga! Anakubalika sana na wananchi na upande wa wapinzani pia. JK anafahamu kwamba jamaa ni jembe na akimpa mpini basi chombo kitakaa mrama! TAtizo ni moja; JK anaogopa kufunikwa na Magufuli na inasemekana ana bifu naye binafsi.! Pia mafisadi wanahofia akipewa u-PM itakuwa mwisho wa wao kuichezea nchi hii, na mawaziri wanamuogopa, inasemekana kuna njama zinafanyika aondolewe hata kwenye baraza la mawaziri!! Tatizop wanajua wananchi watapiga kelele na itakuwa aibu kwao....Uwezekano wa yeye kupata u-PM ni endapo tu kama mama Migiro ataendeleza msimamo wake wa kuwania urais 2015.....

KWA MAONI YANGU NI KUWA MH. PINDA ATAEENDELEA KUWA WAZIRI MKUU KWA KUZINGATIA KUWA MABARIRIKO YA NAFASI YA SPIKA, THEN ETI JK ATEUE WAZIRI MKUU ITAKUWA SI NJEMA KISIASA. PIA KI-UCHUMI MABADIRIKO YA WAZIRI MKUU YATAIGARIMU NCHI MAANA WANATUNZWA KWA PESA ZETU HAO.

NAWASILISHA.

BARAZA JIPYA LA MAWAZILI ZANZIBAR HILI HAPA...

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya Vifungu 42 (1) na (2), 43 (1) na (2) na 47 vya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein ameunda Wizara 16 na kuwateua Wajumbe wa Baraza la Mapinduzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Ikulu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi-
Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame

2.Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Fedha, Uchumi, na Mipango ya Maendeleo)
Mhe. Omar Yussuf Mzee

3. Ofisi ya Rais, (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora)
Mhe. Haji Omar Kheri

4. Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais
Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji.

5. Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais-

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mhe. Mohammed Aboud Mohammed

6. Wizara ya Katiba na Sheria

Mhe. Aboubakar Khamis Bakary.

7. Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Hamad Masoud Hamad

8. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Ramadhan Abdulla Shaaban

9. Wizara ya Afya

Mhe. Juma Duni Haji

10. Wizara ya Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Wanawake na Watoto

Mhe. Zainab Omar Mohammed

11. Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo

Mhe. Abdilahi Jihad Hassan

12. Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati-

Mhe. Ali Juma Shamhuna

13. Wizara ya Kilimo na Maliasili

Mhe. Mansoor Yussuf Himid

14. Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko

Mhe. Nassor Ahmed Mazrui

15. Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mhe. Said Ali Mbarouk

16. Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika

Mhe. Haroun Ali Suleiman

17. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Suleiman Othman Nyanga

18. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Haji Faki Shaali

19. Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri Asiekuwa na Wizara Maalum

Mhe. Machano Othman Said

Aidha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohammed Shein ameteua Naibu Mawaziri kama ifuatavyo:

1. Naibu Waziri, Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano

Mhe. Issa Haji Ussi

2. Naibu Waziri, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali

Mhe. Zahra Ali Hamad

3. Naibu Waziri, Wizara ya Afya

Mhe. Dr. Sira Ubwa Mamboya

4. Naibu Waziri, Wizra ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo,

Mhe. Bihindi Hamad Khamis

5. Naibu Waziri, Wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati

Mhe. Haji Mwadini Makame

6. Naibu Waziri, Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko,

Mhe. Thuwaiba Edington Kissasi

Waheshimiwa wote waliotajwa wanatarajiwa kuapishwa leo jioni katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.

Monday, November 15, 2010

JE KUNA SALIO?????????????

"Aisee baba angu. Kumbe salio kidogo hiviiii!! Aisee Spika Makinda hajanipa pesa yangu ya vikao" Mrema

Sunday, November 14, 2010

MCHUMU MCHUMU TENAA MMWAAAAAAAA....

Kazi ipoooooo!!!!!!!!! kwa wapendanao.

50 CENT MFUASI WA FREEMASONS???

Cutris James Jackson III aka 50 Cent msanii mkali toka kwa Obama,amezua utata baada ya kuonekana ametupia kapelo yenye nembo inayofanana na dini ambayo inahusishwa na imani ya kishetani duniani,Fremasons. Nembo ya freemasons ni pembetatu na jicho moja na 50 Cent inasemekana alikua mstari wa mbele kuipinga dini hiyo hivi karibuni...ngoja tuone inakua vp,kama mwana ndio hivo tena au ni swagga tu!!!

Saturday, November 13, 2010

Friday, November 12, 2010

CUF, TLP, UDP na NCCR Mageuzi vyakataa kuungana na CHADEMA bungeni!!!! Kwa nini?? Sababu hizi hapa!!!!!!

Baada ya Chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni kuwa ni Mhe. Mbowe, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI- source TBC1( MUKTASARI WA HABARI). 


Ukiangalia ndoa ya CUF na CCM kule Zanzibar ni vigumu sana kuamini kuwa CUF inaweza kushirikiana na Chadema kwenye kambi ya upinzani. Sikushawishika kwa mara ya kwanza niliposikia kuwa eti CUF na Chadema watashirikiana. Labda kama CUF ni mbili. Lakini ikiwa CUF ni moja siamini kuwa CUF ile ile inaweza kuwa na muungano na  Chadema. 

CUF vile vile kwenye Bunge la Muungano wanajiona kama wamepotea kwani wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party. Wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party kwa Chadema si CCM. Kwa hiyo CUF haiwezi kumpenda Chadema. Hata ukiangalia kwenye uchaguzi, inaelekea mikakati ya CUF na CCM ilikuwa inafanana na wameshinda wote maeneo ya pwani. Kwa hiyo baadae ukiangalia vizuri kwenye tafakari yako, CUF wanajiona kuwa hawako tofauti sana na CCM.

Hata kampeni zao unaweza kuona kuwa CUF hawakuwa against CCM kihivyo. 

Jingine ni kuwa CCM wanauona wingi wa Chadema kama TISHIO kwao. Hivyo wako tayari kurefusha mkono kwa chama kingine. NCCR alikuwa ni direct ally wa CCM. Kampeni za Kawe zilithibitisha kuwa NCCR ilikuwa adui wa Chadema kuliko kuipnga CCM. Hili ni la muda kidogo. NCCR kina MPs wanne tu. Kwa hiyo CCM kumvutia CUF upande wake ni kupunguza nguvu ya upinzani kwani wabunge 45 wa Chadema ukijumlisha na 30 wa CUF, upande wa wapinzani ilikuwa inakuja na wabunge 75. Hiyo si nguvu ya kupuuza kwa CCM hivyo kwao itakuwa vizuri Chadema wakibaki peke yao.

Kwa ujumla ni kuwa katika Bunge lijalo UPINZANI itakuwa ni Chadema peke yao. Na hilo litawajenga zaidi. Hawa wengine kina UDP, TLP, NCCR na CUF obviously watahamia kwa CCM. Pepo zote za kisiasa zinaonesha hivyo.

BEAKING NEWS.......MARANDO KURA HAZIKUTOSHA ZA USPIKA

HESHIMIWA ANNE MAKINDA NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE BAADA YA KUMSHINDA MH. MGOMBEA MABERE NYAUCHO MARANDU KATIKA UCHAGUZI WA KUMPATA SPIKA MPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
HIVI SASA SPIKA HUYO MPYA ANASIMAMIA ZOEZI LA KUAPA LA WABUNGE WAPYA WA BUNGE HILI, ZOEZI AMBALO LINATARAJIWA KUCHUKUA SIKU 2



Kura zilizopigwa jumla ni 327
Zilizoharibika ni kura 9

Anna...kura 265....SPIKA 74.2%

Marando.....kura 53


Zoezi la upigaji kura za kumchagua Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilienda vizuri huku Anne Makinda (CCM) alimteua mbunge wa Ludewa Mh. Deo Haule Filikunjombe kusimamia kura zake na mgombea wa Chadema Mh. Mabere Marando alimteua Mh. Halima Mdea kwenda kusimamia kura zake.

KWA KAULI HII YA MAKAMBA...BASI KATIBU MKUU WA CCM ANAFAA KUWA MWANAMKE.

Nimevutiwa na hoja ya Mzee Yusuf Makamba kwamba safari hii Kamati Kuu ya CCM iliona ni vyema kupitisha mwanamke kwenye nafasi ya Uspika sababu ni wakati wao na kwa kuwa tangu uhuru hatujawahi kuwa na Spika wa kike.

Kwa maoni yangu ni kuwa chama kama kinawathamini wanawake kingeanzia nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM kwani nayo haijawahi shikwa na mwanamke tangu uhuru  kuliko kukimbilia kwenye uspika ambao chama hakina uhakika wa kushinda moja kwa moja, ''charity begins at home''. Vinginevyo itakuwa siyo KUWAWEZESHA wanawake bali KUWAWEZA.


Hii statement inanikumbusha kauli aliyotoa Chiligati kuhusu kutoswa kwa Seleli kuwa aliachwa sababu hana mvuto, eti sababu alikuwa anatetea nafasi yake hakupaswa kupata idadi ndogo ya kura. Haijachkua muda tumegundua kuwa hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Kikwete naye hana mvuto. Toka ushindi wa 82% (2005) hadi kushindwa kwa 61% (2010) akiwa madarakani. Ama kweli nyani haoni kundule, na wanawake WAKIWEZWA, WANAWEZESHWA!

Mwanamke awe Katibu Mkuu CCM.

NAOMBA KUTOA HOJA

Thursday, November 11, 2010

WABUNGE WAANZA KUTINGA MJENGONI

Mhe. Mr. II akiwa mjengoni. Du amebadirika ghafra wajameni!!!!!!!!

Mhe. Sita na Mhe. Anne Malecela wakisalimiana

Kidume...Dr. Slaa akisalimiana na wabunge Dodoma.

Hebu mcheki Mhe. Vick Kamata mguuni ...ametinga kikuku jamani...mweeeee!!!!! Bunge la mwaka huu ni balaa...Biashara ni matangazo.

Mhe. Halima Mdee na Mhe. Sitta wakisalimiana.

Wednesday, November 10, 2010

MAPINDUZI MAKUBWA CCM HAYA HAPA......SITTA, CHENGE NJE USPIKA

ANNA MAKINDA

ANNA ABDALAH

KATE KAMBA
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.

Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.

SITTA USO KWA USO NA CHENGE
SIKU ZOTE WANGEKUWA HIVI.....TUSINGEYASIKIA YA UNAFIKI.


CHADEMA YAMTEUA MARANDO KUGOMBEA USPIKA

Mh. Mabere Nyaucho Marando


HABARI ZILIZOTUFIKIA PUNDE KUTOKA DODOMA ZINASEMA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KIMEMTEUA MWANASIASA MKONGWE MH. MABERE NYAUCHO MARANDO KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WABUNGE WATEULE VITI MAALUMU WA CCM NA CHADEMA

Tume ya Uchaguzi imetangaza nafasi 104 ya wabunge wa viti maalumu kwa mgawanyo wake wa kuweza kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge. Hivyo baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo CCM imejizolea viti 65, CHADEMA kimepata viti 23 na CUF kimepewa viti 10.

Katika bunge lililopita kulikuwa na Viti maalumu 75 ambapo CCM ilikuwa ina viti 58, CUF viti 11 na CHADEMA viti 6. Viti vingine 6 vimeachwa wazi vikisubiri matokeo ya majimbo 7 ambayo uchaguzi wake haukufanyika.

Yafuatayo ni majina ya wanaopewa nafasi kutajwa kuwa wabunge wateule kutoka CCM na CHADEMA. Chama Cha Wananchi CUF bado hakijapeleka orodha ya majina waliyopendekeza kuchukua nafasi zao 10.

MAJINA YA WABUNGE WATEULE
WA VITI MAALUMU WA CCM NI:

Wabunge 65 wateule wa Viti Maalumu toka CCM waliotajwa ni Sophia Simba, Gaudentia Kabaka, Ummi Mwalimu, Agness Hokororo, Martha Umbulla, Lucy Mayenga, Faida Mohamed Bakari, Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh na Stella Manyanya.
Wengine ni Lediana Mng’ong’o, Sarah Msafiri Ally, Catherine Magige, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa na Al-Shaymaa Kwegir.

Wengine ni Maria Hewa, Hilda Ngoye, Josephine Genzabuke, Esther Midimu, Maida Hamad Abdalla, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Sokoine, Munde Abdallah na Benardetha Mushashu.
Pia wamo Margreth Mkanga, Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Said, Riziki Lulida, Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta na Subira Mgalu.

Wengine ni Vicky Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Getrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Nyabakari na Pudenciana Kikwembe.

Wengine ni Rita Kabati, Martha Mlata, Dk Maua Daftari, Elizabeth Batenga, Azza Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Abeid, Kiumbwa Mbaraka na Roweete Kasikila, Anastazia Wambura, Mary Chatanda, Rosemary Kirigini, Mariam Kisangi na Kemilembe Lwota
-------------------------------

MAJINA YA WABUNGE WATEULE 23
WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NI:

Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza, Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.

Wengine ni Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha na Rachel Mashishanga.

Tuesday, November 9, 2010

Wembe ni ule ule!!!!!!!!!!!!!

HALMASHAURI NANE KUONGOZWA NA UPINZANI


Halmashauri nane nchini zitaongozwa na vyama vya upinzani baada ya kupata viti vingi vya udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa wiki iliyopita.
Halmashauri hizo ni Karatu, Manispaa ya Moshi, Kigoma Mjini, Moshi Vijijini, Ukerewe, Jiji la Mwanza, Kasulu na Mbulu.
MWANZA
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitaliongoza Jiji la Mwanza linaloundwa na majimbo ya Ilemela na Nyamagana kufuatia kushinda kata 11 dhidi ya kata nane zilizochukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uchaguzi katika kata za Mirongo na Mkuyuni uliahirishwa hadi baadaye. Hata hivyo, matokeo yake hayawezi kusababisha athari yoyote kwa kuwa hata kama CCM itashinda itakuwa na viti 10 na isitoshe kata hizo inasemekana ni ngome za Chadema.
KARATU
Katika matokeo ya udiwani Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilishinda halmashauri ya Karatu kwa kupata kata 10 na kata nne kuchukuliwa na Chama Cha mapinduzi (CCM).
UKEREWE
Katika Jimbo la Ukerewe, Chadema imefanikiwa kupata viti 13 kati ya 24 vya udiwani hali inayokiwezesha kuongoza halmashauri hiyo, CCM imepata viti 10 huku CUF ikiwa na kiti kimoja.
KiGOMA MJINI
Chadema imeshinda katika kata 10 wakati CCM imeshinda katika kata tisa.
JIMBO LA MOSHI MJINI
Chadema italiongoza jimbo la Moshi Mjini baada ya kupata kata 17 kati ya kata 21. CCM imepata kata nne.
MOSHI VIJIJINI
Halmashauri ya Moshi Vijijini inayoundwa na majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo, itaongozwa na Chadema kwa kushirikiana na TLP baada ya kupata viti 16 dhidi ya 15 za CCM.
Katika Jimbo la Moshi Vijijini CCM ilipata kata tisa, Chadema kata saba na TLP sifuri wakati katika Jimbo la Vunjo TLP ilipata kata saba, Chadema kata mbili na CCM kata sita.
KASULU
Halmashauri ya Kasulu pia imekwenda kwa upinzani uliopata madiwani 14 dhidi ya madiwani 11 wa CCM. Halmashauri hiyo itaongozwa kwa pamoja kati ya Chadema kilichopata viti madiwani wane na NCCR-Mageuzi kilichopata madiwani 10.
MBULU
Halmashauri ya Mbulu itaongozwa na Chadema baada ya kushinda kata 17 dhidi ya kata 15 zilizochukuliwa na CCM.
ARUSHA
Hata hivyo, katika Jimbo la Arusha Mjini huenda likaongozwa kwa mseto baada ya Chadema kupata madiwani 8, TLP 1 na CCM 10. Kwa kuwa Chadema kilishinda ubunge na mbunge ni sehemu ya madiwani, hivyo chama hicho na TLP vitakuwa na madiwani 10 sawa na CCM hivyo kuongoza kwa mseto.
Hata hivyo, idadi ya madiwani wa viti maalum inaweza kuamua ni chama kipi kiongoze halmashauri hiyo. Chadema kimepata madiwani 8, TLP 1 na CCM 10.

UCHUMI UNAKUA????!!!! EBU CHECK BEI YA MADAFU YETU


KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS KWA AJILI YA TASKER CUP HIKI HAPA


Kocha mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen akitangaza kikosi ya timu ya Kilimanjaro Stars leo katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka nchini (TFF).Wachezaji waliotajwa na kocha ni Akitangaza kikosi hicho kocha mkuu wa timu ya taifa Jean Paulsen amewataja wachezaji Juma Kaseja wa Simba, Shaban Kado na Said Muhando ambao ni magolikipa.Amewataja wachezaji wengine kuwa ni Shadrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasyika, Haruna Shamte, Idrisa Rajab na Juma Nyoso ambao ni mabeki.
Viungo ni Shaaban Nditi, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Jabir Azizi, Nizar Khalfan, Meshack Abel, Mohamed Banka na Kigi Makasi.Amewataja washabuliaji kuwa ni Danny Mrwanda,Mrisho Ngasa, John Bocco, Thomas Ulimwengu, na Mshabuliaji Gaudence Mwaikimba.Kikosi hicho ndicho kitakacho shiriki katika mashindano ya Cecafa Tusker Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 27 mpaka Desemba 10,2010.katikati ni Meneja wa bia ya Tusker,Nandi Mwiyombella na kushoto ni Afisa Uhusiano wa SBL,Imani Lwinga

MPANGILIO WA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KWANZA WA BUNGE

TAREHE 8 - 17 NOVEMBA 2010

JUMATATU
08 Novemba, 2010
Tangazo la Rais Kuitisha Bunge
JUMANNE
09 Novemba, 2010
* Wabunge kuelekea Dodoma
* Kusajili Wabunge Wateule Dodoma
JUMATANO
10 Novemba, 2010
Usajili kuendelea Dodoma - Katibu wa Bunge

ALHAMISI
11 Novemba, 2010
Saa 4.00 Asubuhi
* Mikutano ya Kamati za Vyama vya Siasa
* Kikao cha Briefing UKUMBI WA BUNGE

Saa 10.00 Jioni
Kupokea majina ya wagombea Uspika (Nomination day)

IJUMAA
12 Novemba, 2010

* Mkutano wa Bunge wa Kwanza.
* Kikao cha Kwanza kuanza kwa kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
* Uchaguzi wa Spika.
* Kiapo cha Spika.
* Wimbo wa Taifa na Dua
* Kiapo cha Utii kwa Wabunge Wote.

JUMAMOSI ASUBUHI
13 Novemba, 2010
Wabunge kuendelea Kuapishwa

JUMATATU
15 Novemba, 2010
Wabunge kuendelea Kuapishwa

JUMANNE
16 Novemba, 2010 Asubuhi
Wabunge kuendelea Kuapishwa

Mchana
* Kuthibitisha Jina la Waziri Mkuu
* Waziri Mkuu kutoa Neno la Shukrani
* Uchaguzi wa NAIBU SPIKA

JUMATANO
17 Novemba, 2010
Asubuhi
Waziri Mkuu Kuapishwa IKULU -CHAMWINO

10. Saa 10.00 Jioni
RAIS KULIHUTUBIA BUNGE UKUMBI WA BUNGE

NENO LA SHUKRANI - WAZIRI MKUU

HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE

USIKU Tafrija ya Rais kwa Wabunge wote Viwanja vya Bunge

* ENDAPO ITAKUWA SIKUKUU TAREHE 15 AU 16 NOVEMBA, 2010 BUNGE LITASITISHA SHUGHULI ZAKE HADI SIKU INAYOFUATA. OFISI YA BUNGE

Monday, November 8, 2010

CHENGE KUGOMBEA USPIKA!! Aaaaaah!!!

Pichani Mh.Andrew Chenge Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki na Mwanasheria mkuu wa Zamani wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga SeaView leo ambapo amesema ana nia ya kugombea Uspika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Amesema ameamua kugombea Uspika wa ili aweze kusimamia na kutibu majeraha ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita kwa wengine.

Mswali ya kujiuliza ni haya:
1. Chenge ana kesi ya kifisadi Mahakamani, atawezaje kutibu majeraha ya kiutendaji wakati yeye ni mahututi?
2. Chenge ana kesi ya mauaji ya raia kwa kugonga na gari, je atawezaje kuwatetea walioathirika bungeni wakati ameshindwa kuwasaidia ndugu na jamaa wa wale aliwaua?



Saturday, November 6, 2010

MADAI YA DR. SLAA YASIPUUZWE HATA KIDOGO, YANA MSINGI.

Ndugu zangu wazalendo wa nchi hii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini mkubwa mwenendo wa matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo mbalimbali hususan kwa nafasi ya urais. Kwa wale wenzangu walioanza kufuatilia mapema kabisa, lazima watakuwa wameshtuka sana na namna "trend" ya matokeo ya urais ilivyobadilika ghafla. Matokeo ya awali kutoka mikoani yalianza kuonyesha tofauti ndogo ya kura kati ya Dr. Slaa na Jakaya Kikwete. Hali hiyo iliendelea kwa kipindi kirefu na kwenye baadhi ya majimbo kama Iringa, Mbeya, Moshi na Arusha Dr. Slaa alikuwa anaongoza kwa mbali kabisa. Baadaye nilishtuka nilipoambiwa kwamba matokeo ya urais yatakuwa yanatangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) na siyo wasimamizi wa uchaguzi kutoka kwenye majimbo. Kama suala la uchaguzi ni la wazi na huru, kwa nini wasimamizi wa uchaguzi wasitangaze tu matokeo ya urais sambamba na matokeo ya ubunge na udiwani. Ni nini kilichozuia????? Uhuru wa kutoa matokeo ulikuwa wapi???? Au wasimamizi wa kwenye majimbo hawakuwa na haki ya kutangaza matokeo ya uraisi????? 

Ndugu zangu ninachokiona hapa, ni kama kuna ujanja ulifanywa,  pia sisi watanzania wazalendo hatutakuwa hata mara moja kukaa kimya na kuridhika na matokeo ya urais yaliyotangazwa na NEC. Ninawaomba sana tena sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati wote nchini wafuatilie mlingano wa matokeo (yaliyoidhinishwa na mawakala wa vyama husika) kutoka kwenye majimbo na matokeo yanayotangazwa na NEC. Sina hakika kama jambo hili linaweza kuruhusiwa lakini ninaona kuwa ni jambo la msingi sana. Lazima wananchi tujiridhishe kwamba kilichotangazwa na NEC kwamba ndiyo jumla ya kura za urais kwa mgombea fulani kutoka jimbo fulani lazima iwe kweli ndiyo jumla ya matokeo ya vituo vyote vya jimbo husika. Ninawaomba sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati mlifuatilie jambo hili kwa ukaribu sana kwani inawezekana hapa ndipo ujanja mkubwa uliofanyika ili kuwezesha chama tawala kuendelea kuongoza nchi hii.

Ndugu zangu, ninaandika haya kwa uchungu mkubwa sana baada ya kusoma maoni ya wananchi ninaokutana nao mitaani na hata ninaposoma kwenye mitandao. Ukweli ni kwamba watanzania wengi hivi sasa wameichoka CCM na wanataka mabadiliko. Hali hii imeonekana dhahiri wakati wa mikutano ya Chadema kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.  Tafadhali viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati tusiwakatishe tamaa wananchi lazima tuthamini na kuenzi harakati za wananchi kutaka mabadiliko. 

HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM . MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO SURA YA MTU. MIFANO:

JIMBO:                        CHAMA:-----------UBUNGE:------RAIS:

ARUSHA MJINI - CHADEMA...................56,208..... .......54,208
                       CCM................... ....36,107..................39,107

MBEYA-MJINI:CHADEMA..................46,411.... ..............42,917
                     CCM............... .........24,236...................32,249

NYAMAGANA: CHADEMA...............38,171....................30,991
                     CCM.....................27,883......................32,320
 ILEMERA :CHADEMA................31,256......... .............29,701
                 CCM......................26,870........................9,143
 MASWA MAGH: CHADEMA......17,456............ ..........11,742
                    CCM..................12,824........................17,104
 MASWA MASH: CHADEMA......17,075.......................12,203
                        CCM.............. 17,014.......................21,150

 Kali zaidi ni hii ya JIMBO LA Musoma mjini: Kutoka KURA 14,723 za Mbunge wa CCM na kuongezwa kufikia KURA 49,858 za KIKWETE.

MUSOMA MJINI CHADEMA......21,335................23,211
CCM.....................................14,723................49,858???
Tutafakari hili.


Hebu angalia hali halisi. Na hili pia halihitaji elimu ya juu kulielewa na kulichambua. Wapiga Kura Waliojiandikisha ni: 20,137,303.
 Na Waliojitokeza Kupiga Kura Ni: 8,626,283 sawa na asilimia 42.84%.
Hii ina maana waliojiandikisha lakini hawajapiga kura ni: 11,511,020 sawa na asilimia 57.16%.
Ni jukumu letu pia kuangalia ni kwa nini wapiga kura wengi hawakujitokeza. Tusaidiane kuangalia sababu hizi nami nitaanza kwa chache ambazo nimezifanyia utafiti kwa kuwauliza wale ambao walijiandikisha lakini hawakuweza kupiga kura:

1. Hawakuona majina yao ingawa walijiandikisha
2. Walikuwa safarini nje ya Wilaya, Mkoa au Nchi
3. Walikuwa sehemu tofauti na waliojiandikisha
4. Walikuwa wagonjwa
5. Kuna ambao wamefariki katika kipindi cha uboreshaji wa daftari na kipindi cha kupiga kura
6. Kuna walioondolewa kwa madai kuwa wamekufa lakini wako hai.
Mie nadhani tayari kulikuwa na mazingira ya kuchakachua kura ndiyo maana idadi ilikuwa kubwa sana. haiwezekani kweli zaidi ya nusu ya wapiga kura wasiende kupiga kura wakati hamasa ilikuwa kubwa sana. Haiwezekani. Kuna namna.
Je, kwa maoni au utafiti wako ni sababu gani nyingine zilizowafanya watu wasijitokeze kupiga kura?



Jambo lingine lililodhihilisha kuwa CCM hawana sera ni pale  Prof. Lipumba kumpa JK ilani ya CUF eti iwasaidie kuchukua mambo! Wao CCM wanayo ya kwao na Lipumba anajua hilo ila Prof kwa ujanja aliitoa ili kuonyesha kuwa CCM hawana sera za maana wajifunze kuweka sera za kunufaisha taifa. That was a smart move. Nadhani pia CCM wanatafuta ya Chadema iweze kuwasaidia kwa siku za usoni.