Search This Blog

Sunday, June 26, 2011

KWA MTINDO HUU POSHO IKATWE TU:

Wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI ni nyingi sana ukilinganisha hali ya umasikini nchini.
Kwa mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake ikipunguzwa tutakuwa tumeokoa kama 900 Billion fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea nyumba, kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta ya Afya, kama Taifa tutakuwa tumeinua kiwango cha maendeleo na tutamaliza tatizo kubwa sana tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi katika shughuli za maendeleo.

Wabunge nawaomba muitendee haki Nchi hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11 wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada. Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili la kukataa posho na kupunguza gharama za matumizi ili kuisaida Nchi

No comments:

Post a Comment