Search This Blog

Monday, June 13, 2011

WAKATI SERIKALI INAPOTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO BILA KUWASHIRIKISHA WANANCHI: matokeo yake ndo haya.....

Hapa ni Hamuyebe - Ukerewe: 
Serikali imetekeleza mradi wa soko lakini kama unavyoona hakuna bidhaa ndani ya soko na jengo halitumiki kama soko. Pesa nyingi zimetumika lakini mradi hauwanufaishi wananchi maana hautumiki kwa shughuli za kuinua hali ya kiuchumi. Wakazi wa eneo hili wamelalamika kuwa jengo hili la soko ujenzi wake haukushirikishwa  wananchi na pia wananchi hawana bidhaa za kutosha kwenda kuuza humo sokoni:

Hebu angalia picha ya hapa chini uone kwa makini:
Kwa sababu ya uzalishaji kidogo wa mazao ya kilimo, pembeni kuna kibanda kidogo sana cha nyanya ambacho pia wateja ni wachache sana. Tunaiomba serikali iwashirikishe jamii wakati wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo pia kuwekeza sana katika shughuli za kilimo ili kuinua kiwango cha mazao na ndipo hilo soko litatumika.

No comments:

Post a Comment