KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ametaka yafanyike mabadiliko ya sera na sheria ili kuwezesha kuondolewa kwa posho kwa wabunge na watumishi wa umma na ununuzi wa magari ya kifahari ili fedha hizo ziwanufaishe Watanzania wote. Akizungumza bungeni wakati akichangia hoja ya Bajeti ya Serikali, Mbowe alisema; "Tunachotaka Chadema sio kuwafutia wabunge posho, bali ni kufanya mabadiliko ya msingi katika sera zinazohusu posho," alisema Mbowe na kusisitiza:
Hatuwezi kujenga taifa kwa kulipana posho kubwa namna hii. Kwa uhalisia ni kuwa posho, semina, ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali na wabunge na kusafiri kwa ndege kwenye madaraja ya juu vinachangia kuongeza umaskini wa nchi.
Mbowe alisisitiza kuwa vitu hivyo vinapaswa kufutwa haraka na fedha hizo zipelekwe kwenye maeneo ambayo yatakuwa ni ya manufaa kwa Watanzania walio wengi.Mbowe ameitaka serikali ifanye uamuzi wa haraka wa kuyapiga mnada mashangingi yote yaliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya vigogo serikalini.
No comments:
Post a Comment