Watumishi wa umma ambao hawautumikii umma, bali wanajitumikia wao wenyewe.
Wanasiasa wanaozungumza, lakini hawasemi lolote.
Wapigaji kura ambao wanapiga kura, lakini hawamchagui mtu yeyote.
Walimu wanaofundisha ujinga.
Mahakimu ambao wanawahukumu watu na wanachukua mlungula.
Wanajeshi ambao kila wakati wako katika mapambano na watu ambao inabidi wawalinde.
Maaskari ambao hawawezi kuzuia uhalifu kwa sababu wako “busy” na mikakati ya kufanya uhalifu.
Watu ambao wanazitumikia pesa.
Wacha Mungu ambao badala ya kumhubiri Mungu kwa ajili ya mbingu wanamhubiri Mungu kwa ajili ya tamaa zao .
Madaktari ambao badala ya kuokoa maisha, wanayamalizia.
Makandarasi ambao wanatengeneza majumba yanayoporomoka na barabara zenye mashimo.
Wafanyabiashara wanaouza takataka.
Watu wafundishao maadili lakini wao wakiwa hawana maadili.
No comments:
Post a Comment