Search This Blog

Friday, June 17, 2011

KAMBI YA UPINZANI YAIFUMUA BAJETI YA SERIKALI: wafuta posho, watangaza kima cha chini mshahara sh 315,000

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zito Kabwe

 Kambi ya Upinzani Bungeni imetangaza bajeti mbadala ya Sh14 trilioni na kubainisha upungufu mkubwa katika Bajeti ya Serikali, huku ikipendekeza kufutwa kwa misamaha ya kodi kwa kampuni za uchimbaji wa madini na mafuta na posho za vikao kwa watumishi wa umma, wakiwamo wabunge. Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni, mjini hapa jana, Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe alisema hatua hiyo imelenga kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Katika bajeti hiyo mbadala, kambi hiyo imesisitiza umuhimu wa ushiriki mkubwa zaidi wa umma na uchunguzaji wa utungaji na utekelezaji wa Bajeti, ili kuboresha uwajibikaji na kuziba mianya zaidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

Kambi ya Upinzani inapendekeza kupunguza misamaha ya kodi ikitaka isizidi asilimi...Soma zaidi http://www.kwanzajamii.com 

No comments:

Post a Comment