Search This Blog

Thursday, April 21, 2011

MAJAMBAZI YAKAMATWA JIJINI MWANZA

Jana majira ya saa kumi na dakika kadhaa jioni jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwatia nguvuni watu wanne wanaotuhumiwa kwa kufanya ujambazi wakiwa na bunduki moja aina ya smg na bastola mbili moja ikiwa na risasi 12 na na ya pili ikiwa na risasi 2. Kwa mujibu wa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza Simon Sirro amesema kuwa watu hao wamekematwa katika eneo la mtaa wa libert jirani na benki ya NMB wakiwa kwenye harakati za safari kuelekea Nyegezi ambako walipanga kwenda kufanya uvamizi kwenye duka moja. 
RISASI 14.
Raia wema ndiyo waliofanikisha kukamatwa kwa majambazi hao kwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi ambao nao bila ajizi walifuatilia nyendo za majambazi hao na hatimaye kufanikiwa kuwatia nguvuni.
BASTOLA ZILIZOKAMATWA.
Awali majambazi hayo yalivamia bar moja eneo la kilimahewa na kuwalaza watu chini kisha kupora mali zao na kuiba bastola ya mteja mmoja. Majambazi hayo yaliyokuwa katika gari dogo yalipostukia kuwa yanafuatiliwa yalianza kufyatua risasi hovyo hali iliyosababisha shughuli za biashara kwenye eneo la tukio kusimama kwa muda. 
Wawili kati ya majambazi hayo manne hali zao ni mbaya na wamepelekwa hospitali ya Rufaa Bugando, mmoja katwangwa risasi mguuni na takoni ile hali mwingine sugu anayetambulika kwa jina maarufu 'Askofu' akiwa amevunjika mguu kabisa kwa kutwangwa risasi wakati alipojaribu kuitoroka mikono ya polisi.
Jeshi la polisi mwanza linaendelea kufanya uchunguzi zaidi juu ya tukio zima ambamba na kuwahoji watuhumiwa wote wanne wa mkasa huo.

Wednesday, April 20, 2011

GAMBA LIMEVULIWA LAKINI SUMU IPO PALEPALE

Kitendo cha CCM kuja na kiini macho cha kujivua gamba na kubakia na sumu kimezua tafsiri mbalimbali. Nyoka akitaka kuvua gamba anatoa lote kuanzia kichwani hadi mkiani lakini gamba la CCM limetoka kidogodogo tena kifuani tu! Hivi ni gamba gani hili? la mjusi? ,kenge?, mamba? Tena wameweka na muda ndani ya siku 90. Hilo  ni gamba? Au ukurutu? Kwa nyoka gamba linamsaidia tu kujikimu bali sumu yake ndo silaha.

Watu walioonekana ni gamba la kuvuliwa kama akina Makamba bado ni kiini macho maana kama kweli CCM ina nia mathubuti basi haina haja ya kuweka muda wa siku 90. Hata kama tukiamini kuwa gamba litaondolewa, Je sumu je??? Sumu ya CCM iko katika muundo wa uongozi wa chama, sera zake zisizokidhi mahitaji ya jamii, uwezo mdogo wa viongozi, n.k. Na kama nyoka akivua gamba basi hilo gamba halina thamani tena linakanyangwa tu na kuoza ama kutupiliwa mbali na upepo. Kiini macho ni kuwa wale walioonekana kama gamba kwa CCM wakavuliwa cha kushangaz ani kuwa bado wana nyadhifa nyeti katika serikali ya CCM. Kama CCM wana nia ya dhati na falsafa ya KUJIVUA GAMBA  basi hiyo falsafa itumike serikalini ambako hayo magamba yapo.

Lakini pamoja na kiini macho hicho cha CCM hebu tujiulize maswali haya:
Je, gamba hili la CCM lililovuliwa hivi karibuni liliota lini au alizaliwa nalo? Au ni kipindi hiki cha awamu ya nne ndo gamba lilionekana?

Je gamba hili litachukua muda gani kuota tena?

Ok, CCM wauelezee umma athari ilizokuwa inapata jamii kwa gamba lake.

NAOMBA KUTOA HOJA.

Monday, April 11, 2011

BREAKING NEWS !!!! GBAGBO AKAMATWA!!

Hatimaye,Laurent Gbagbo amekamatwa kama Saddam Hussein akiwa amejificha shimoni huku jasho likimchuruzika. Ameondoka kwa aibu, pingu mikononi huku akipewa taulo ajifute jasho. Aliloa kuanzia kichwani hadi unyao. Alionekana kuchanganyikiwa akijifuta jasho hata kwenye makwapa bila aibu. Ni furaha iliyoje imla mwingine kuangukwa kwa kila aina ya aibu!Kwa habari zaidi, Bonyeza hapa.

Sunday, April 10, 2011

MBOZI WAJA NA STAILI MPYA YA TIBA: Huko ni MATONE ya Uponyaji

Nabii Joshua Mwantyala akiwanyunyuzia maji ya tiba wananchi waliokusanyika katika mkutano wake wa Neno la Mungu la uponyaji na kuwaombea wagonjwa wote wenye magonjwa sugu kama vile Ukimwi, Kansa na mengineyo. Nabii Joshua juzi alianzisha huduma ya tiba yake inayojulikana kama majibu ya tiba ya maajabu ya Loliondo ambapo yeye hutoa matone ya maji ya uponyaji.ambayo huwanyunyuzia wagonjwa vinywani.

BREAKING NEWS !!!! MUKAMA KATIBU MKUU CCM, Makamba na unabii wake chali

Katibu Mkuu mpya CCM (kulia) Bw. Wilson Mukama


Nape Nauye "Uenezi unaanzia hapa hapa"
 Habari tulizopokea ni kwamba, hatimaye, CCM imeamua kumpiga kibuti katibu wake Mkuu Yusuf Makamba. Nafasi yake imechukuliwa na aliyewahi kuwa mkurugenzi wa jiji la Dar Es Salaam, Wilson Mukama.  Naye Nape Nnauye amechukua nafasi ya itikadi na uenezi ilikuwa ikishikiliwa na John Chiligati. Inaonekana zamu hii ni ya watoto wa wakongwe wa CCM. Maana Rehema Nchimbi mtoto wa John Nchimbi baba yake Emanuel Nchimbi,kama Nape, amechukua nafasi ya katibu wa organizesheni.

Swahiba mwingine wa Kikwete, Zakhia Meghji aliyetupwa nje kwa kashfa ya EPA benki kuu na anayedaiwa kushiriki ufisadi wa kutisha kwenye wizara ya utalii amerejea kwa kishindo kwa kunyakua nafasi ya katibu wa fedha na uchumi iliyokuwa chini ya Amos Makala.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa CCM imeamua kujivua gamba kwa kuwatimua vinara na watetezi wa ufisadi hasa Makamba. Hatimaye Kikwete amelitupa jini na jinamizi la Makamba ambaye kimsingi alikuwa akimtawala Kikwete pamoja na uenyekiti wake. Bila shaka akina Tambwe Hiza sasa wanajinonihii kwenye suruali kutokana na muungu wao Makamba kupigwa buti. Je imejivua gamba au ni gamba lile lile la kujuana, kulindana, kufisidi, kuganga njaa, usanii na upuuzi mwingine? Time will tell.

......sijui nitoroke hata hiki kikao!!!! watu hawa hawana hata huruma- Makamba naye katimuliwa U-katibu mkuu aliyejifanya Nabii ndani ya CCM iliyooza.
"Poa tu"--Makala -  .......Ndo wale wale waliokunywa uji wa mgonjwa

Monday, April 4, 2011

UNA MIAKA 30??? OMBA UONGOZI BARAZA LA VIJANA CHADEMA(BAVICHA)

Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, John Mnyika

Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) ngazi ya taifa, linatarajia kufanya uchaguzi mwezi ujao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya chama hicho, John Mnyika, nafasi zitakazogombewa ni pamoja na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji, Mweka Hazina, Wawakilishi wa Bavicha kwenye Mkutano Mkuu wa chama na wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu la chama.

Alitaja umri unaoruhusiwa kugombea kwa mujibu wa Katiba umri wa ujana ni kati ya Miaka 18 na 35.
 Alisema mgombea anatakiwa kugombea kwenye umri unaomruhusu kumaliza kipindi chake cha uongozi akiwa bado na umri wa Ujana; hivyo wagombea wenye umri wa zaidi ya miaka 30 hawataruhusiwa kugombea ili kufanya viongozi wa vijana wasiwe zaidi ya miaka 35 katika kipindi chao chote cha utumishi katika Bavicha.

" Wagombea watachukua na Kurudisha Fomu kuanzia tarehe 4 Aprili hadi tarehe 26 Aprili. Fomu zitatolewa kuanzia ngazi ya Mkoa, Makao Makuu ya chama," alisema Mnyika.

Alisema kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watalipia shilingi elfu thelathini.

Alisema waliogombea uchaguzi wa awali uliofutwa watajaza na kulipia upya hata kama waliogombea nafasi hizo hizo wanazogombea sasa kwa mujibu wa kanuni za chama.
 Alisema mikutano ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wawakilishi wa Bavicha kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Bavicha kwa mujibu wa katiba, kanuni na taratibu.

Alisema Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, Mratibu wa Uhamasishaji na Mwekahazina watapendekezwa na Kamati ya Utendaji ya Bavicha na uteuzi wao utathibitishwa na Kamati Kuu ya chama.
 Kuhusu kampeni, Mnyika alisema kampeni za uchaguzi zitafanywa kwa kuzingatia kanuni za chama, maadili ya uongozi/viongozi pamoja na muongozo juu ya uendeshaji wa uchaguzi ndani ya chama uliopitishwa na Baraza Kuu la Chama unafafanua mambo yanayopaswa kufanywa na yasiyopaswa kufanywa wakati wa kampeni na uchaguzi ndani ya chama kwa lengo la kujenga mshikamano na umoja ndani ya chama na kufanya uchaguzi uwe huru na wa haki.

Saturday, April 2, 2011

HII INAASHIRIA NINI? USHINDI?? KIPIGO???

Upande huu wachezaji wa Simba Sports Club wakifanya mazoezi kwa ajili ya kuikabili TP Mazembe kesho.

Upande ule timu ya TP Mazembe wakikata mauno baada tu ya kuwasili uwanja wa ndege DSM.

Hii inaashiria nini?? Ushindi?? au Kipigo? Tusubiri kesho jumapili tarehe 3/4/2011

WEST HAM 2 MANCHESTER 4...........premier league

Wayne Rooney kapiga hat-trick na kuiwezesha Manchester United kuikong'oli  West Ham United 4-2.
Kosa la Patrice Evra kuunawa mkono eneo la penati na faulo ya Nemanja Vidic kwa Carlton Cole kulisababisha  Mark Noble wa West Ham kushindilia magoli 2 kwa njia ya penati.Lakini Manu ilipata goli la nne kupitia kwa Javier Hernandez Chicharito na kuondoka na ushindi wa goli 4-2.

Friday, April 1, 2011

TANZANIA YAWEKA REKODI YA NOTI.....kati ya noti hizo hapo chini ni ipi noti mpya?

Kwa mara ya kwanza Tanzania imeweka rekodi ya pesa/Noti kama ifuatavyo:
1. Kuwepo kwa noti mbili (2) zenye kiwango sawa na zipo katika mzunguko kwa wakati mmoja na kwa muda mrefu sasa.
2. Noti mpya inazeeka na kuchakaa mapema kuliko noti ya zamani. Ukiangalia picha hiyo hapo juu utadhani noti ya upande wa chini ndio ya zamani,, kumbe ni mpyaaaaaa ina umri wa miezi minne(4) tu.

Sielewi kwa nini BoT inapata kigugumizi kushughulikia tatizo la hizo noti ambazo wanaziita mpya na zinatoa rangi kama batiki......kumbe hamna lolote!! Jamani serikali hii imeshindwa kabisa kuwajibika maana ni maajabu sana noti ndani ya miezi minne tu noti imeshazeeka, je ikimaliza miaka 5 si tutabaki na sarafu tu?????
Nawasilisha.