Search This Blog

Wednesday, April 20, 2011

GAMBA LIMEVULIWA LAKINI SUMU IPO PALEPALE

Kitendo cha CCM kuja na kiini macho cha kujivua gamba na kubakia na sumu kimezua tafsiri mbalimbali. Nyoka akitaka kuvua gamba anatoa lote kuanzia kichwani hadi mkiani lakini gamba la CCM limetoka kidogodogo tena kifuani tu! Hivi ni gamba gani hili? la mjusi? ,kenge?, mamba? Tena wameweka na muda ndani ya siku 90. Hilo  ni gamba? Au ukurutu? Kwa nyoka gamba linamsaidia tu kujikimu bali sumu yake ndo silaha.

Watu walioonekana ni gamba la kuvuliwa kama akina Makamba bado ni kiini macho maana kama kweli CCM ina nia mathubuti basi haina haja ya kuweka muda wa siku 90. Hata kama tukiamini kuwa gamba litaondolewa, Je sumu je??? Sumu ya CCM iko katika muundo wa uongozi wa chama, sera zake zisizokidhi mahitaji ya jamii, uwezo mdogo wa viongozi, n.k. Na kama nyoka akivua gamba basi hilo gamba halina thamani tena linakanyangwa tu na kuoza ama kutupiliwa mbali na upepo. Kiini macho ni kuwa wale walioonekana kama gamba kwa CCM wakavuliwa cha kushangaz ani kuwa bado wana nyadhifa nyeti katika serikali ya CCM. Kama CCM wana nia ya dhati na falsafa ya KUJIVUA GAMBA  basi hiyo falsafa itumike serikalini ambako hayo magamba yapo.

Lakini pamoja na kiini macho hicho cha CCM hebu tujiulize maswali haya:
Je, gamba hili la CCM lililovuliwa hivi karibuni liliota lini au alizaliwa nalo? Au ni kipindi hiki cha awamu ya nne ndo gamba lilionekana?

Je gamba hili litachukua muda gani kuota tena?

Ok, CCM wauelezee umma athari ilizokuwa inapata jamii kwa gamba lake.

NAOMBA KUTOA HOJA.

No comments:

Post a Comment