Search This Blog

Sunday, June 26, 2011

KWA MTINDO HUU POSHO IKATWE TU:

Wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI ni nyingi sana ukilinganisha hali ya umasikini nchini.
Kwa mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake ikipunguzwa tutakuwa tumeokoa kama 900 Billion fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea nyumba, kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta ya Afya, kama Taifa tutakuwa tumeinua kiwango cha maendeleo na tutamaliza tatizo kubwa sana tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi katika shughuli za maendeleo.

Wabunge nawaomba muitendee haki Nchi hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11 wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada. Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili la kukataa posho na kupunguza gharama za matumizi ili kuisaida Nchi

Wednesday, June 22, 2011

KAMA NOMA NA IWE NOMA::: Mhe. Mbowe ataka Posho zifutwe, Mashangingi yote yauzwe!!


KIONGOZI wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, ametaka yafanyike mabadiliko ya sera na sheria ili kuwezesha kuondolewa kwa posho kwa wabunge na watumishi wa umma na ununuzi wa magari ya kifahari ili fedha hizo ziwanufaishe Watanzania wote. Akizungumza bungeni  wakati akichangia hoja ya Bajeti ya Serikali, Mbowe alisema; "Tunachotaka Chadema sio kuwafutia wabunge posho, bali ni kufanya mabadiliko ya msingi katika sera zinazohusu posho," alisema Mbowe na kusisitiza:

 Hatuwezi kujenga taifa kwa kulipana posho kubwa namna hii. Kwa uhalisia ni kuwa posho, semina, ununuzi wa magari ya kifahari kwa viongozi wa serikali na wabunge na kusafiri kwa ndege kwenye madaraja ya juu vinachangia kuongeza umaskini wa nchi.

Mbowe alisisitiza kuwa vitu hivyo vinapaswa kufutwa haraka na fedha hizo zipelekwe kwenye maeneo ambayo yatakuwa ni ya manufaa kwa Watanzania walio wengi.Mbowe ameitaka serikali ifanye uamuzi wa haraka wa kuyapiga mnada mashangingi yote yaliyonunuliwa na serikali kwa  ajili ya vigogo serikalini.

Sunday, June 19, 2011

Mzee CHILUBA, AMEFARIKI DUNIA!!!

Rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 68. Bwana Chiluba amekuwa na ugonjwa moyo kwa miaka kadha.
Rais Chiluba aliiongoza Zambia kwa mwongo mzima katika miaka ya '90, na baada ya kustaafu alishtakiwa kwa sababu ya rushwa.

Frederick Chiluba alipata urais wa Zambia mwaka wa 1991, wakati Afrika inaanza kuingiia katika demokrasi ya vyama vingi. Kabla ya hapo alikuwa kiongozi wa wafanyakazi.

Aliahidi kuleta mabadiliko lakini alipochukua uongozi Zambia ilikuwa imeshafilisika, naye aliacha rushwa kustawi. Alipojaribu kujiongezea muhula wa tatu wa madaraka, alipingwa. Pia alilaumiwa kuwa akipenda maisha ya anasa.

Baada ya kuondoka madarakani mwaka wa 2001, mrithi wake, Levy Mwanawasa, alimshtaki kwa shutuma za rushwa. Baada ya kesi ya miaka 6 kuhusu ubadhirifu wa mali ya taifa, Frederick Chiluba aliambiwa hakuwa na makosa. .

Lakini katika kesi nyengine iliyofanywa katika mahakama makuu ya London, Chiluba alikutikana na hatia ya kuiba mamilioni ya dola ya fedha za serikali ya Zambia, kwa kutumia akaunti kwenye mabenki ya London.

Friday, June 17, 2011

KAMBI YA UPINZANI YAIFUMUA BAJETI YA SERIKALI: wafuta posho, watangaza kima cha chini mshahara sh 315,000

Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zito Kabwe

 Kambi ya Upinzani Bungeni imetangaza bajeti mbadala ya Sh14 trilioni na kubainisha upungufu mkubwa katika Bajeti ya Serikali, huku ikipendekeza kufutwa kwa misamaha ya kodi kwa kampuni za uchimbaji wa madini na mafuta na posho za vikao kwa watumishi wa umma, wakiwamo wabunge. Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni, mjini hapa jana, Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, Zitto Kabwe alisema hatua hiyo imelenga kuongeza mapato ya Serikali na kupunguza matumizi yasiyokuwa ya lazima.

Katika bajeti hiyo mbadala, kambi hiyo imesisitiza umuhimu wa ushiriki mkubwa zaidi wa umma na uchunguzaji wa utungaji na utekelezaji wa Bajeti, ili kuboresha uwajibikaji na kuziba mianya zaidi ya ufisadi na matumizi mabaya ya rasilimali za nchi.

Kambi ya Upinzani inapendekeza kupunguza misamaha ya kodi ikitaka isizidi asilimi...Soma zaidi http://www.kwanzajamii.com 

Tuesday, June 14, 2011

UKITAKA MTU ASIJUE PASSWORD YAKO: Tumia hii mbinu

Ukiona vipi tumia hii hapa....
Ukiona wadau wanazidi kupiga chambo......kazi ni kwakooooooooo!!!!!!

NONDOZ ZINATAFUTWA KWA KASI: hapa ni CBE Mwanza

Hapa ni CBE Mwanza, wanachuo wa kozi mbalimbali wakijiandaa na mitihani ya kumaliza mwaka na wengine kumaliza kabisa chuo. Mijadala ya vikundi imekuwa ikisaidia kujengeana uwezo miongoni mwa wanachuo.

Hebu fikiria ndo umetoka kwa discussion chuoni ama shuleni ama ukiwa na mitikasi yako, unaamua kwenda kwenye ATM na akili imechoka, ile kingiza kadi tu unakutana na hii hali..............
Mwana blogu wenu anawatakia wanachuo wote CBE Mwanza, CBE Dodoma, CBE DSM, SAUT, UDOM, UDSM na vyuo vyote tanzania mafanikio mema katika mitihani yote!

Monday, June 13, 2011

WAKATI SERIKALI INAPOTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO BILA KUWASHIRIKISHA WANANCHI: matokeo yake ndo haya.....

Hapa ni Hamuyebe - Ukerewe: 
Serikali imetekeleza mradi wa soko lakini kama unavyoona hakuna bidhaa ndani ya soko na jengo halitumiki kama soko. Pesa nyingi zimetumika lakini mradi hauwanufaishi wananchi maana hautumiki kwa shughuli za kuinua hali ya kiuchumi. Wakazi wa eneo hili wamelalamika kuwa jengo hili la soko ujenzi wake haukushirikishwa  wananchi na pia wananchi hawana bidhaa za kutosha kwenda kuuza humo sokoni:

Hebu angalia picha ya hapa chini uone kwa makini:
Kwa sababu ya uzalishaji kidogo wa mazao ya kilimo, pembeni kuna kibanda kidogo sana cha nyanya ambacho pia wateja ni wachache sana. Tunaiomba serikali iwashirikishe jamii wakati wa utekelezaji wa shughuli za maendeleo pia kuwekeza sana katika shughuli za kilimo ili kuinua kiwango cha mazao na ndipo hilo soko litatumika.

Friday, June 3, 2011

Sababu ya kuchelewa kuvua gamba ni lugha iliyotumika... hapo chini

Ni OPERATION???? AU OPARATION?????

UWAJIBIKAJI KWA UMMA: nyuma ya pazia hali ipo hivi.....


Watumishi wa umma ambao hawautumikii umma, bali wanajitumikia wao wenyewe.
 Wanasiasa wanaozungumza, lakini hawasemi lolote.
 Wapigaji kura ambao wanapiga kura, lakini hawamchagui mtu yeyote.
 Walimu wanaofundisha ujinga.
 Mahakimu ambao wanawahukumu watu na wanachukua mlungula.
 Wanajeshi ambao kila wakati wako katika mapambano na watu ambao inabidi wawalinde.
 Maaskari ambao hawawezi kuzuia uhalifu kwa sababu wako “busy” na mikakati ya kufanya uhalifu.
 Watu ambao wanazitumikia pesa.
 Wacha Mungu ambao badala ya kumhubiri Mungu kwa ajili ya mbingu wanamhubiri Mungu kwa ajili ya tamaa zao .
Madaktari ambao badala ya kuokoa maisha, wanayamalizia.
 Makandarasi ambao wanatengeneza majumba yanayoporomoka na barabara zenye mashimo.
 Wafanyabiashara wanaouza takataka.
 Watu wafundishao maadili lakini wao wakiwa hawana maadili.

Wednesday, June 1, 2011

KAZI NI KWAKOOOOOO!

Hii ndiyo mikakati ya serikali hii ya kuinua kiwango cha elimu nchini...Kumbuka leo ni Siku ya Watoto duniani. Je huu ni uungwana???
 Kipindi cha mitihani wengine hutumia mbinu hizi. Ili mradi kufaulu!!!!
 Ukiona wezi na vibaka wamezidi ....tumia hii mbinu hapa chini!!
 Kazi ni kazi ............ ni ubunifu na uwezo wako tu.
 Tunaikumbukaje siku ya WATOTO DUNIANI?1/6/2011