Search This Blog

Friday, December 31, 2010

HIZI NI MILA????? AU NINI HAPA TANZANIA!!!!!???




Jamani au kuna kitu kinatafutwa maana nashindwa kuelewa kama kweli ni MILA za Kitanzania kweli. 

NINAWATAKIENI KHERI YA MWAKA MPYA 2011. THANKS FOR YOUR COMMENTS FROM ALL BLOG VIEWERS. 
STAY BLESSED NA TUJIPANGE KWA MWAKA UJAO.......CHEEEEERS.

KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA HII HAPA WAJAMENI


Vuguvugu la kudai katiba mpya limepamba moto nchini Tanzania. Sijui ni wangapi wanaoshiriki katika vuguvugu hili wameshawahi kuisoma katiba nzima na kutafakari mapungufu yake. Hapa chini ni katiba nzima kama ilivyowekwa katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Katiba. Hebu na tuisome kwa makini kabla hatujaamua ni mabadiliko gani tunayotaka kuyafanya. Mungu Ibariki Tanzania!!!

Friday, December 24, 2010

KWA WAFUATILIAJI WA BLOG HII...NINAWATAKIA XMAS NJEMA


THIS IS TO WISH YOU MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2011

MASH ATANGAZA KIKOZI CHA STARS CHA MICHUANO YA NILE

KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania (taifa stars) kwaniaba ya kocha mkuu wa timu hiyo Jan poulsen (aliye mapumzikoni kwao Sweden) amekitaja kikosi cha wachezaji 23 wa timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la Nile basin mashindano yanayotaraji kuanza kutimua vumbi rasmi tarehe 5 january 2011 nchini Misri.Tofauti na wengi tulivyozoea, Tukio hilo limefanyika leo katika eneo la wazi la uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza ambapo kocha huyo msaidizi yuko ziarani kwa ajili ya shughuli maalum huku likishuhudiwa na Viongozi mbalimbali wa soka waandishi wa habari na wapenzi wa soka wa jiji la miamba.

KIKOSI KAMILI NI KAMA IFUATAVYO

GOALKEEPERS:-
1.JUMA KASEJA - SIMBA SC
2.SHAHBAN KADO -MTIBWA FC
3.SAID MOHAMED - MAJIMAJI SC

DEFENDERS:-
4.SHADRACK NSAJIGWA - YOUNG AFRICAN
5.MWASIKA STEPHANO - YOUNG AFRICAN
6.AGREY MORRIS - AZAM FC
7.KELVIN YONDANI - SIMBA SC
8.JUMA NYOSSO - SIMBA SC
9.NADIR HAROUB - YOUNG AFRICAN

MIDFIELDELS:-
10.IDRISSA RAJABU - SOFAPAKA
11.NURDIN BAKARI - YOUNG AFRICAN
12.SHAHBAN NDITI - MTIBWA FC
13.HANRY JOSEPH - NORWAY
14.JABIR AZIZ - AZAM
15.ABDI KASSIM - YOUNG AFRICAN

FOWARD PLAYERS
16.SALUM MACHAKU - MTIBWA FC
17.MRISHO NGASA - AZAM
18.NIZAR KHALFAN - CANADA
19.GODFREY TAITA - KAGERA SUGAR
20.ATHUMAN MACHUPPA - SWEDEN
21.JERRY TEGETE - YOUNG AFRICAN
22.SAID MAULID - ANGOLA
23.ALI AHMED SHIBOLI - SIMBA SC

Kocha huyo msaidizi amesema kuwa mazoezi ya Stars yataanza rasmi siku ya jumatatu ambapo kambi itakuwa uwanja wa karume jijini dar .

Anauhakika na kikosi hicho alichokitaja kuwa cha ushindi akiwa na imani kubwa kuwa kila mchezaji atacheza kwa bidii na hatimaye kulipandisha soka la Tanzania katika viwango vya soka duniani.

Sunday, December 19, 2010

NOTE MPYA ZA HAPA TZ HIZI HAPA





Noti za zamani bado ni fedha halali na zina thamani sawa na zile mpya. Zitaendelea kutumika na kuwepo katika mzunguko sambamba na hili toleo jipya la noti mpaka hapo hizo za zamani zitakapotoweka taratibu na hatimaye kwisha kabisa kwenye mzunguko. Hivyo basi, wananchi wanashauriwa kuendelea kuzipokea na kuzitumia noti za zamani bila shaka au wasiwasi wowote kuhusu uhalali wake hadi hapo zitakapokwisha na kutoweka kabisa katika mzunguko. Vilevile ieleweke kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa kupeleka noti za zamani benki na kutaka kupewa mpya.
Toleo hili la noti mpya lina taswira inayozingatia mandeleo ya uchumi na jamii. Tumefanya mabadiliko kidogo katika toleo jipya kwa kuweka picha za waasisi wa taifa letu. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anaonekana kwenye noti ya shilingi elfu moja na Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwenye noti ya shilingi mia tano. Noti tatu zilizosalia yaani elfu mbili, elfu tano na elfu kumi zitaendelea kuwa na picha za wanyama pori ambao wanapatikana kwa wingi kwenye hifadhi na mbuga zetu za wanyama. Hata hivyo, kutokana na kupunguza ukubwa wa noti hizi mpya tumeweka picha za vichwa vya wanyama hao badala ya wanyama wazima kama ilivyo kwenye noti za zamani.
Ili kupambana na uhalifu wa kughushi na kuongeza muda wa noti hizi kukaa katika mzunguko kwa muda mrefu kabla ya kuchakaa, toleo hili limeongezewa ubora kwa kuweka alama maalum mpya za usalama na kutumia taaluma mpya ya kuziimarisha. Alama mbali mbali za usalama zimeboreshwa na kwa mara ya kwanza kabisa alama ya “motion” ambayo ni rahisi sana kutambulika kwa macho imetumika katika noti hizi. Ili kuelimisha wananchi kuhusu alama za usalama zinazotambulisha uhalali wa noti zetu, tumetoa matangazo na vipeperushi ambavyo vitasambazwa sehemu mbali mbali za nchi. Taarifa ya alama za usalama za noti pia zipo kwenye tovuti ya Benki Kuu kwa anwani www.bot-tz.org
Ni muhimu kwa umma kufahamu alama za usalama ili uweze kutofautisha noti halali na bandia kwa urahisi. Hata hivyo Benki Kuu inapenda kutahadharisha watu wawe waangalifu na kuzichunguza noti zote wanazopokea hasa kwenye giza ili kuhakikisha kwamba ni noti halali. Uchunguzi ufanywe kwa noti zote zilizopo kwenye mzunguko pamoja na za zamani. Endapo wana mashaka warejee kwenye mabango na vipeperushi vilivyotolewa na Benki Kuu au tawi lolote la Benki Kuu.
Gavana
Benki Kuu ya Tanzania

Friday, December 17, 2010

MAREKANI INAHAHA KUBORESHA ELIMU YAKE....SISI WA-TZ TUMEJIPANGAJE?????

  • Matokeo ya mtihani wa kimataifa yaliyotolewa hivi karibuni kwa wanafunzi wenye miaka 15 yamezua kizaazaa hapa Marekani. Katika matokeo hayo Marekani imeshika nafasi ya 17 katika kusoma, nafasi ya 31 katika hesabu na nafasi ya 23 katika sayansi. Alama ya jumla ya Marekani ikilinganishwa na nchi nyingi zilizoendelea ni "wastani" na kwa ujumla imefanya vibaya. Wanafunzi kutoka Korea ya Kusini, Finland, China, Singapore, Canada ndiyo wamefanya vizuri zaidi wakifuatiwa na nchi zinginezo. Wanafunzi kutoka mji wa Shanghai nchini China ndiyo wanaongoza kwa kupata alama za juu zaidi.
  • Kwa Wamarekani jambo hili halikubaliki kwani wanajua kwamba bila kuwa nambari wani katika elimu, haiwezekani kwao kuendelea kuwa nambari wani kiuchumi na kitekinolojia ulimwenguni; na tayari wameshajiwekea malengo ya kurudi kileleni tena katika masomo yote ifikapo mwaka 2020. Wakiweza kufanya hivi, mahesabu yao yanaonyesha kwamba uchumi wao utaweza kujiongezea dola zipatazo trilioni 41 katika miaka 20 ijayo!
  • Watawezaje kurudi kileleni? Hatua ya kwanza waliyoipendekeza ni kuimarisha taaluma ya ualimu na kuifanya iheshimiwe zaidi ili kuweza kuvutia wanafunzi wenye vipaji. Hii ni pamoja na kuwalipa walimu mishahara mizuri pamoja na marupurupu ya kutosha, kuwajengea mazingira mazuri ya kufanyia kazi na nafasi zinginezo za kujiendeleza. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba katika nchi zinazofanya vizuri katika elimu, ualimu si kazi ya kiholela tu. Katika nchi kama Singapore, Finland na Korea ya Kusini, kwa mfano, ni wanafunzi bora pekee ndiyo huruhusiwa kujiunga na ualimu (bofya hapa). Hata katika nchi za Kiarabu mkakati kama huu tayari umeanza kupendekezwa.
  • Nilishangaa kuona kwamba sisi tunafanya kinyume. Kimsingi wale wanaofeli ndiyo tunawabebesha jukumu la kuelimisha taifa huku tukiwalipa mishahara kidogo na kuwafanyisha kazi katika mazingira magumu sana hasa kule vijijini. Na hapa hatujawataja hawa wa"Voda Fasta!". Taaluma ya ualimu haiheshimiwi hata kidogo japo kusema kweli ndiyo mama wa kila taaluma na msingi wa kila taifa lililoelimika. Ndiyo maana kuna kipindi fulani walimu walitishia kugoma na waziri wa elimu wa wakati ule inasemekana alitoa tamko kwamba hata walimu wakigoma hakuna neno kwani anaweza kuokota watu mabarabarani na sokoni wakaingia madarasani kufundisha!Tutawezaje kuwa na elimu bora kama tunadharau taaluma ya ualimu namna hii? Ati, ni kwa nini hawa vijana wenye vipaji wanaopata divisheni wani tusiwape kila kitu ili wavutike na kwenda kusomea ualimu? Au tutakimbilia umasikini wetu na kusema kwamba hatuna pesa na kwamba programu ya aina hiyo haiwezekani?
  • Jambo jingine lilinivutia katika ripoti hii ni hili. Karibu nchi zote zilizofanya vizuri sana zinatumia lugha yake zenyewe kufundishia madarasani. Wachina wana Kichina chao, Wakorea na Kikorea chao, Wafin wana Kifini chao n.k. Na sisi je? Tumeng'ang'ania sera ya lugha ambayo ni kichekesho, sera ambayo kimsingi haiwasaidii watoto wetu kumudu lugha yo yote kitaalamu kati ya zile tunazotumia. Kutokana na kizingiti hiki cha lugha, elimu yetu imebutuka na kuwa zoezi la kukariri tu hata kama hatuelewi hicho tunachokikariri kina maana gani. Hii kweli ni elimu?
  • Kuna mengi ya kujifunza katika ripoti hii. Jambo la msingi ambalo inabidi tulitambue ni kwamba hatutaweza kuendelea bila kuwa na elimu bora inayowakaramsha vijana wetu na kuwafanya wawe tayari kwenda kupambana na dunia pale wanapomaliza masomo yao. Na kuboresha taaluma ya ualimu pamoja na kuwa na sera imara ya lugha ya kufundishia vinaweza kuwa mwanzo mzuri katika kuleta mabadiliko ya kweli katika mfumo wetu wa ualimu

Tuesday, December 14, 2010

ASERNAL HOI KWA MASHETANI WEKUNDU

JI-SUNG PARK.Bao safi kwa kichwa la Ji-Sung Park katika kipindi cha kwanza, lilitosha kuipatia ushindi Manchester United dhidi ya Arsenal na kuwawezesha kushikilia usukani wa ligi kutoka kwa mahasimu wao hao.

Nafasi nzuri kwa Arsenal ilikuwa ni ya Marouane Chamakh, ambaye alikosa kufunga baada ya mpira wa kichwa alioupiga kuzuiwa na Nemanja Vidic.

WAYNE ROONEY.Wayne Rooney angeweza kuongeza bao la pili, lakini mkwaju wake wa penalti baada ya Clichy kuunawa mpira, ukapaa juu ya lango la Arsenal.
Kwa matokeo hayo, Manchester United sasa wamefikisha pointi 34 wakiwa na mchezo mmoja mkononi, wakifuatiwa na Arsenal yenye pointi 32, sawa na Manchester City iliyo nafasi ya tatu na Chelsea watakaopambana na Manchester United siku ya Jumapili ijayo wapo nafasi ya nne na pointi 31.

DR. REMMY ONGALA KAFARIKI DUNIA

HABARI ZIMETUFIKIA KWAMBA MWANAMUZIKI MAARUFU NA KIPENZI CHA WENGI RAMADHANI MTORO ONGARA MAARUFU KAMA 'DK. REMMY' AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO NYUMBANI KWAKE MBEZI.

HABARI ZINASEMA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE SINZA KWA REMMY JIJINI DAR. TAARIFA ZAIDI ZA MAZISHI TUTAWALETEA KADRI ZITAVYOPATIKANA.

DR REMMY ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WANAMUZIKI MAHIRI WALIOKUWA NYOTA KATIKA TASNIA HIYO KWA MUDA MREFU SANA. MIAKA YA KARIBUNI ALIACHANA NA MUZIKI WA KIDUNIA NA KUOKOKA AMBAPO ALIIMBA NYIMBO ZA INJILI KWA MAFANIKIO MAKUBWA.

DK. REMMY ATAKUMBUKWA PIA KWA KUWA MWANAMUZIKI WA KWANZA ALIYEIMBA HADHARANI FAIDA YA MATUMIZI YA KONDOM KATIKA WIMBO WAKE 'MAMBO KWA SOKSI' AMBAO HATA HIVYO ULIPIGWA VITA SANA KWA KILE KILICHOITWA ATI KUKIUKA MAADILI KIASI HATA UKAFIFIA KWA MSHANGAO WA WENGI.

MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI
-AMINA

KIKWETE AKABIDHIWA KOMBE LA CHALLENGE NA VIJANA WA KILIMANJARO STARS

JK akiwa katika picha ya pamoja na kikosi kizima cha Timu ya Kili Stars Ikulu jijini Dar es Salam

Nahodha wa Timu ya Taifa Tanzania Bara(Kili Stars) Shadrack Nsajigwa akimkabidhi JK Kombe la Chalenji Ikulu jijini Dar leo baada ya timu hiyo kuibuka Bingwa wa michuano ya Chalenji jana.Rais Kikwete aliialika timu hiyo Ikulu kuipongeza. Pembeni yake ni Mama Salma Kikwete na Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.

Wednesday, December 8, 2010

TRAFIK KAZINI

Akiwa anawasiliana na Radio call - lakini anaongoza magari

Akiwahimiza madereva kujali muda

Akipozi

Anawahi kuhamasisha zaidi,

SIKU YA UHURU - MWANZA

MSECHU AWASILI NYUMBANI-TZ




LICHA ya Mganda Davis Ntare kutwaa taji la Tusker Project Fame 2010, jopo la majaji kwa pamoja na uongozi wa chuo cha mafunzo cha shindano hilo wamekiri kwamba mshiriki wa Tanzania, Peter Msechu, ana kila sababu ya kuwa ndiye mshindi wa shindano.

Kila mtu kwa wakati wake, majaji Ian, Hermes Joachim na Juliana Kanyomozi, walimtaja Msechu kuwa ni mwanamuzikii maarufu anayejiamini sana na kujiweza jukwaani, na pia mbunifu.

Sifa hizo ndizo zinazotakiwa kwa mwanamuziki wa karne hii iliyojaa utandawazi, walieleza majaji.

Msechu ambaye kete yake ya mwisho aliitupa kwa kutumia kwa kibao cha Kilwa Jazz aliudhihirishia tena umma wa wengi katika Afrika Mashariki kwamba anaweza kuwainua kwenye viti na kuwaimbisha muda wowote anaotaka.

Msechu, huku akionyesha kujiamini kwamba muziki ni njia pekee ya kueleza hisia zake kwa jaji huyu kwani, angepata wapi nafasi nyingine ya kumwambia.

"Ningemuita nikamwambia nina maongezi naye angekuja?", alisema Msechu katika mkutano na waandishi wa habari mara baada ya onyesho hilo kwisha na washindi kutajwa katika maeneo ya Ruaraka, jijini Nairobi, eneo ambapopia yapo makao makuu ya East African Breweries, watengenezaji wa bia ya Tusker.

Akizungumza na Mwananchi, Msechu ambaye ameshinda mkataba wa mwaka mmoja wa wa kurekodi na Kampuni ya Africa Sound yenye makao makuu nchini Kenya alisema anaamini kuwa yeye ni mshindi, ila zawadi kubwa amechukua Davis, na atalithibitisha hilo atakapoanza rasmi kazi yake ya muziki, mashabiki wataendelea kufurahi kumsikiliza na kumuona jukwaani.

Friday, December 3, 2010

URUSI KUANDAA KOMBE LA DUNIA 2018

Shirikisho la soka duniani, Fifa, limetangaza Urusi kuandaa Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kuzishinda nchi za England, Ureno na Uhispania, na Uholanzi na Ubelgiji.
Aidha Qatar nayo imechaguliwa kuandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Nchi nyingine zilizokuwa zikiwania nafasi hiyo ni Australia, Marekani, Japan na Korea Kusini.
Kwa mara ya kwanza katika historia, mashindano hayo ya kombe la dunia yanakwenda kufanyika nchini Urusi, Captain wa timu ya taifa hilo Andrey Arshavin ambaye pia hukiputa katika timu ya Arsenal, huku akishangilia, aliruka kwa furaha toka katika kiti alichokuwa amekaa akimpa mkono kila aliyekutana naye kuonyesha furaha yake ambayo ilikuja kama zali la mentali.
"Nina furaha kubwa, kwasababu hili ni tukio kubwa kwetu. Hakuna anayeelewa tukio hili lina maana gani kwa nchi yangu. Lakini ninaamini mara baada ya 2018 watu watatuelewa nini tunamaanisha." Kauli yake Arshavin.

Tuesday, November 30, 2010

BEI YA COCA COLA JUU !!!!!

Kampuni ya Coca cola Nyanza Bottling company limited (NBCL) leo imetangaza rasmi bei mpya za soda zake, akitangaza bei hizo Mkuu wa mauzo na masoko wa kampuni hiyo bw. Bhubhinder Singh amezitaja bei hizo ni kama ifuatavyo...
Bei ya soda za kampuni hiyo zimepanda kutoka shilingi 400 kwa ujazo wa chupa ya ml350 hadi shilingi 500 kwa ujazo huo huo. Coca cola inawasihi wateja wake wote kutolipa zaidi ya shilingi 500 katika ununuzi wa soda kama ilivyoainishwa kwenye jedwali hapo juu.
Bei hiyo halali itatambulishwa kwa nguvu zote kupitia vyombo mbalimbali vya habari, mabango, vipeperushi kwenye sehemu za mauzo, kwenye friji za mauzo, kalenda zitakazotoka za mwaka 2011, t-shirts, kofia na promosheni za mitaani ili kutusaidia hata pale tunapokwenda sehemu za vijijini tusibamizwe na wauzaji, kwani kwa vijijini bei ni hiyo ya 500 hata kabla haijapanda kihalali. Bei ya kreti moja inapanda kutoka 8,100 hadi 9,600 huku faida ya muuzaji ikipanda kutoka asilimia 18 na kuwa asilimia 25.
Kampuni hiyo imetoa changamoto kwa wadau wake kwa kuwazawadia chupa 3 za vinywaji bure kwa kila kreti moja watakalonunua kuanzia tarehe 1 hadi 10 december 2010 na kuanzia december 11 hadi 20.2010 Nunua kreti moja upate chupa mbili za vinywaji.

Sunday, November 28, 2010

KIKWETE KUMWAMBIA DR. BILALI AKAFUNDISHE UDOM!!! IMEKAAJE???

Nimemsikia juzi Rais Kikwete akimwagiza Dr Bilal awe anaenda kutoa lecture pale UDOM. Kuna mambo ambayo wananchi ni bora tujiulize.  

1. Kufundisha chuo kikuu ni lazima taratibu zitumike, kwa mfano lazima awe mwajiriwa iwe full time au part time na lazima atasimamiwa kwamba kweli anafanya kazi hiyo na hatimaye atalipwa kwa kazi hiyo. Unadhani kama makamu wa rais ataweza kukidhi matakwa ya kazi hiyo? 

2. Inamaana tuamini kuwa U-Makamu wa Rais hauna majukumu makubwa kiasi cha kumruhusu mhusika kuendelea na majukumu mengine na tuamini kuwa U-Makamu wa Rais ni kazi rahisi saaaaaaaaaana!!!


3. Dr. Bilal kama Makamu wa Rais anapewa ulinzi na ndiyo maana anaandamana na walinzi muda wote katika majukumu yake. Je, atakuwa anaingia nao kwenye vyumba vya kufundishia? Au nje ya darasa ni lazima kuwe na askari wa kutosha kumlinda??, Je wanafunzi wote wafanyiwe screening kabla ya kuingia kwenye kipindi au kama walikuwepo watoke wawe screened then waingie, kipindi si kitakuwa kimeisha kabla ya kuanza jamani!!!??. Na hizo kelele za ving'ora kila siku si itakuwa kero?? 

Kauli za JK huwa zinabeba maana anayoijua yeye. Mbona Shein ni Dr lakini haikuwahi kutokea kuambiwa akashike chaki kufundisha?. Hii itakuwa ni zaidi ya udhalilishaji na ni tatizo la JK kutokuzingatia hotuba ndio maana anajikuta kila siku yuko off-point.

Nadhani washauri wake wawe makini ila tuna mshukuru kwa kutufahamisha kuwa Makamu wa Rais hana kazi kubwa za cheo hicho hata kama atakaa Dodoma kuendelea kufundisha mambo pale Ikulu yataendelea tu.

Nawasilishaaaaaaaa!

Wednesday, November 24, 2010

BREAKING NEWS !!!! BARAZA LA MAWAZIRI TZ HILI HAPA...


1. Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mathias Chikawe
Ofisi ya Rais – Mahusiano na Uratibu:  Stephen Wassira
2.Ofisi ya Rais  – Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia
3. Ofisi ya Makamu wa Rais – ( Muungano)  Samia Suluhu
2. Ofisi ya  Makamu wa Rais – (Mazingira) Dr. Terezya Luoga Hovisa
4. Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge): William Lukuvi
2. Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu
5. Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Huruma Mkuchika
Naibu: Aggrey Mwanri
Naibu: Kassim Majaliwa
6. Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo
Naibu: Gregory Teu
NAibu: Pereira Ame Silima
7. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Shamsi Vuai Nahodha
Naibu: Balozi Khamis Suedi Kagasheki
8. Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani
9. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe Naibu: Mahadhi Juma Mahadhi
10. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi
11. Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo
Naibu: Benedict Ole Nangoro
12. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mnyaa Mbarawa
Naibu: Charles Kitwanga
13. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka Naibu: Goodluck Ole Madeye
14. Wizara ya Maliasili na Utalii Ezekiel Maige
15. Wizara ya Nishati na Madini William Mganga Ngeleja 1. Adam Kigoma Malima
16. Wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli
Naibu: Dr. Harrison Mwakyembe
17. Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu
Naibu: Athumani Mfutakamba
18. Wizara ya Viwanda na Biashara Dr. Cyril Chami
Naibu: Lazaro Nyalandu
19. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa
Naibu: Philipo Mulugo
20. Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Haji Hussein Mpanda
Naibu: Dr. Lucy Nkya
21. Wizara ya Kazi na Ajira Gaudensia Kabaka Makongoro Mahanga
22. Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Sophia Simba Umi Ali Mwalimu
23. Wizara ya Habari, Vijana na Michezo Emmanuel John Nchimbi
Naibu:Dr. Fenella Mukangara
24. Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel John Sitta
Naibu Dr. Abdallah Juma Abdallah
25. Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Prof. Jumanne Maghembe
Naibu: Christopher Chiza
26. Wizara ya Maji: Prof. Mark James Mwandosya
Naibu: Eng. Gerson Lwinge