Search This Blog

Sunday, May 27, 2012

Zanzibar hali si shwari. Vurugu kila kona. Kisa Uamsho! Wanataka Taifa huru





Baadhi ya polisi wakionekana kutupa mabomu ya kutoa machozi



Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma
Tuachiwe Tupumuwe
Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma

Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma









Hali imeendelea kuwa ni ngumu hapa Zanzibar huku matokeo kadhaa yakitokeza usiku wa jana lakini pia milipuko ya mabomu bado inaendelea huku baadhi ya Wananchi wakijipanga upya kuendelea na harakati zao juu ya kuishinikiza Serikali kukubali matakwa yao. Baadhi ya matokeo ambayo yameripotiwa jana usiku ni pamoja na kuchomwa kwa Kanisa hapa kariakoo,kuchomwa kwa baadhi ya magari na pia uharibifu wa majumba ni matokeo ambayo yamejitoikeza kutokana na vurugu ambazo zilianza jana jioni.
Polisi wakiwa na magari yao wanajaribu kutawanya vikundi vya watu na huku baadhi ya barabara kama vile Michezani zikionekana nyeupe bila watu. Bado hali ya Visiwani Zanzibar inaonesha kuwa ni ya wasi wasi mkubwa sana.Mabomu ya machozi yanaendelea kutupwa na Polisi wa F.F.U, ambao tayari wamelivalia njuga suala hili huku Wananchi na wao wakizidi kujipanga katika baadhi ya maeneo yao, matokeo haya inaonesha dhahiri kwamba pana kazi kubwa ya kufanywa kuituliza hali hii kwa wahusika.
Inshallah tutajaribu kupeana taarifa za Zanzibar kadri ya hali itakavyojiri, bado tunafuatilia kutaka kuona kwamba mhadhara uliopangwa na Jumuia ya uamsho kama utafanyika leo hii au la, baada ya kutokea hali hii ya vurugu hapa Visiwani.

No comments:

Post a Comment