Search This Blog

Tuesday, May 29, 2012

Uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc na viongozi wa juu wa chadema


Kimbunga cha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), chaikumba Washington DC

Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa, Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi, Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, Dogo Janja, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.

Mhe. Leticia Nyerere (Picha ya kwanza kushoto) akiwa na Mhe. Maryam Msabaha kwenye uzinduzi wa watawi la Chadema Washington Dc

Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington Dc


Baadhi ya wakereketwa wachukua kadi baada ya uzinduzi wa tawi la chadema Washington

Mhe. Nassari Joshua (Dogo Janja) Akishanga mamia ya wana DMV waliofurika katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc

Mhe. Peter Msigwa akiandika masuali yaliokuwa yakiulizwa na baadhi ya wakireketwa

Mwanachama wa chadema kutoka Boston Ma na kamanda Doto wakiuliza masuali tafauti katika mpango mzima wa uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc uliofanyika jana Mei 27, kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.

Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania


Wana DMV wakisikiliza hutuba ya Mhe. Zitto Kabwe. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)


Viongozi wa Chadema wakijipanga mpango wa kuwapa wana DMV, kadi za chama

Wakereketwa wa Chadema wakiwa wameshikilia kadi zao za chama hicho


Mzee wa mipangilio a.k.a Cosmas akipata picha na Mhe. Zitto Kabwe, pamoja na wakereketwa


Mhe. Leticia Nyerere (Picha ya kwanza kushoto) akiwa na Idrisa Jumbe all the way from Dar na ni mdhamini wa pendo wa Mhe. Maryam Msabah ni Mbunge wa viti maalum Zanziba, pamoja na Mhe. Nassari Joshua (Dogo Janja) na mwana wa Mhe Leticia. Picha ya pili Kalley Pandukizi, Mwana Pamoja na Mh. Zitto Kabwe

Sunday, May 27, 2012

Zanzibar hali si shwari. Vurugu kila kona. Kisa Uamsho! Wanataka Taifa huru





Baadhi ya polisi wakionekana kutupa mabomu ya kutoa machozi



Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma
Tuachiwe Tupumuwe
Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma

Haya Shime Wazanzibari wakati wa Ukombozi Umeshafika Inshallah Hakuna Kurudi Nyuma









Hali imeendelea kuwa ni ngumu hapa Zanzibar huku matokeo kadhaa yakitokeza usiku wa jana lakini pia milipuko ya mabomu bado inaendelea huku baadhi ya Wananchi wakijipanga upya kuendelea na harakati zao juu ya kuishinikiza Serikali kukubali matakwa yao. Baadhi ya matokeo ambayo yameripotiwa jana usiku ni pamoja na kuchomwa kwa Kanisa hapa kariakoo,kuchomwa kwa baadhi ya magari na pia uharibifu wa majumba ni matokeo ambayo yamejitoikeza kutokana na vurugu ambazo zilianza jana jioni.
Polisi wakiwa na magari yao wanajaribu kutawanya vikundi vya watu na huku baadhi ya barabara kama vile Michezani zikionekana nyeupe bila watu. Bado hali ya Visiwani Zanzibar inaonesha kuwa ni ya wasi wasi mkubwa sana.Mabomu ya machozi yanaendelea kutupwa na Polisi wa F.F.U, ambao tayari wamelivalia njuga suala hili huku Wananchi na wao wakizidi kujipanga katika baadhi ya maeneo yao, matokeo haya inaonesha dhahiri kwamba pana kazi kubwa ya kufanywa kuituliza hali hii kwa wahusika.
Inshallah tutajaribu kupeana taarifa za Zanzibar kadri ya hali itakavyojiri, bado tunafuatilia kutaka kuona kwamba mhadhara uliopangwa na Jumuia ya uamsho kama utafanyika leo hii au la, baada ya kutokea hali hii ya vurugu hapa Visiwani.

CHADEMA yazindua M4C kwa kishindo DSM


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe, akiwahutubia wananchi wa jijini Dar es Salaam, waliohudhuria mkutano wa chama hicho uliofanyika kwenye Viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam leo, kuhusu Dira ya Mabadiliko 'Movement For Change'.


Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, akitembeza kibakuli kuchangisha fedha za kuendeshea Kampeni hiyo.


Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.


Kutoka (kushoto) ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, Tundu Lisu na Godbless Lema.

Stars yatoa droo na malawi


Kikosi kipya cha timu ya Taifa Stars, kilicho chini ya Kocha mpya Kim Poulsen, kilichocheza mechi ya Kirafiki ya Kimataifa na Malawi leo katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kutoka sare ya bila kufungana.


Kiungo wa Taifa Stars, Mwinyi Kazimoto (kulia) akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa timu ya Taifa Malawi, James Sangala, wakati wa mchezo wa Kirafiki wa kimataifa baina ya timu hizo, uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni. Timu hizo zimetoka sare ya 0-0.


Kiungo Mshambuliaji wa Taifa Stars, Haruna Moshi 'Boban' (kulia) akijiandaa kumtoka beki wa Malawi, Limbikani Nzava, wakati wa mchezo huo.


Mshambuliaji wa Taifa Stars, Mrisho Ngasa (katikati) akiwatoka mabeki wa Malawi, wakati wa mchezo huo.


Mshambuliaji wa Kimataifa wa timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta (kulia) akimhadaa beki wa Malawi, wakati wa mchezo huo.

Thursday, May 24, 2012

Kamanda Mnyika ashinda kesi:


HOJA zenyewe zilizokuwa zinalalamikiwa na Hawa Nghumbi ni hizi:
1)Kwamba Mnyika alimtuhumu kuuza nyumba za UWT
2)Kutumia Laptop za Mnyika Kuhesabu kura
3)Kuingia watu wengi wa CHADEMA ktk chumba cha kuhesabia kura
4)Kuzidi kwa kura hewa 16,000
5)Kukosewa kwa karatasi za kujumulisha kura (form)


Hoja zote zimepigwa chini: Peopleeeeeeeessssss Poweeeeeeeeeeeerrrrrrrrrrr

Wednesday, May 9, 2012

Wakuu wapya wa Wilaya hawa hapa

1. Novatus Makunga Hai
2. Mboni M. Mgaza Mkinga
3. Hanifa M. Selungu Sikonge
4. Christine S. Mndeme Hanang
5. Shaibu I. Ndemanga Mwanga
6. Chrispin T. Meela Rungwe
7. Dr. Nasoro Ali Hamidi Lindi
8. Farida S. Mgomi Masasi
9. Jeremba D. Munasa Arumeru
10. Majid Hemed Mwanga Lushoto
11 Mrisho Gambo Korogwe
12. Elias C. J. Tarimo Kilosa
13. Alfred E. Msovella Kiteto
14. Dkt. Leticia M. Warioba Iringa
15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe Mbozi
16. Mrs. Karen Yunus Sengerema
17. Hassan E. Masala Kilombero
18. Bituni A. Msangi Nzega
19. Ephraem Mfingi Mmbaga Liwale
20. Antony J. Mtaka Mvomero
21. Herman Clement Kapufi Same
22. Magareth Esther Malenga Kyela
23. Chande Bakari Nalicho Tunduru
24. Fatuma H. Toufiq Manyoni
25. Seleman Liwowa Kilindi
26. Josephine R. Matiro Makete
27. Gerald J. Guninita Kilolo
28. Senyi S. Ngaga Mbinga
29. Mary Tesha Ukerewe
30. Rodrick Mpogolo Chato
31. Christopher Magala Newala
32. Paza T. Mwamlima Mpanda
33. Richard Mbeho Biharamulo
34. Jacqueline Liana Magu
35. Joshua Mirumbe Bunda
36. Constantine J. Kanyasu Ngara
37. Yahya E. Nawanda Iramba
38. Ulega H. Abadallah Kilwa
39. Paul Mzindakaya Busega (mpya)
40. Festo Kiswaga Nanyumbu
41. Wilman Kapenjama Ndile Mtwara
42. Joseph Joseph Mkirikiti Songea
43. Ponsiano Nyami Tandahimba
44. Elibariki Immanuel Kingu Kisarawe
45. Suleiman O. Kumchaya Tabora
46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa Siha
47. Manju Msambya Ikungi (mpya)
48. Omar S. Kwaangw’ Kondoa
49. Venance M. Mwamoto Kibondo
50. Benson Mpesya Kahama
51. Daudi Felix Ntibenda Karatu
52. Ramadhani A. Maneno Kigoma
53. Sauda S. Mtondoo Rufiji
54. Gulamhusein Kifu Mbarali
55. Esterina Kilasi Wanging’ombe (mpya)
56. Subira Mgalu Muheza
57. Martha Umbula Kongwa
58. Rosemary Kirigini Meatu
59. Agness Hokororo Ruangwa
60. Regina Chonjo Nachingwea
61. Ahmed R. Kipozi Bagamoyo
62. Wilson Elisha Nkhambaku Kishapu
63. Amani K. Mwenegoha Bukombe
64. Hafsa M. Mtasiwa Pangani
65. Rosemary Staki Senyamule Ileje
66. Selemani Mzee Selemani Kwimba
67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga Mlele (mpya)
68. Iddi Kimanta Nkasi
69. Muhingo Rweyemamu Handeni
70. Lucy Mayenga Uyui

MAJINA 63 WAKUU WA WILAYA WA ZAMANI NA
VITUO VYAO VYA KAZI

NA. JINA KITUO CHA KAZI
1. James K. O. Millya Longido
2. Mathew S. Sedoyeka Sumbawanga
3. Fatuma L. Kimario Igunga
4. Capt. (Mst.) James C. Yamungu Serengeti
5. Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato Maswa
6. Sarah Dumba Njombe
7. Jowika W. Kasunga Monduli
8. Elizabeth C. Mkwasa Bahi
9. Col. Issa E. Njiku Misenyi
10. John B. Henjewele Tarime
11. Elias W. Lali Ngorongoro
12. Raymond H. Mushi Ilala
13. Francis Miti Ulanga
14. Evarista N. Kalalu Mufindi
15. Mariam S. Lugaila Misungwi
16. Anna J. Magowa Urambo
17. Anatory K. Choya Mbulu
18. Fatma Salum Ally Chamwino
19. Deodatus L. Kinawiro Chunya
20. Ibrahim W. Marwa Nyang’hwale (mpya)
21. Dkt. Norman A. Sigalla Mbeya
22. Moshi M. Chang’a Mkalama (mpya)
23. Jordan M. Rugimbana Kinondoni
24. Georgina E. Bundala Itilima (mpya)
25. Halima M. Kihemba Kibaha
26. Manzie O. Mangochie Geita
27. Abdula S. Lutavi Namtumbo
28. Zipporah L. Pangani Bukoba
29. Dkt. Ibrahim H. Msengi Moshi
30. Col. Cosmas Kayombo Kakonko (mpya)
31. Lembris M. Kipuyo Muleba
32. Elinasi A. Pallangyo Rombo
33. Queen M. Mlozi Singida
34. Juma S. Madaha Ludewa
35. Angelina Mabula Butiama (mpya)
36. Hadija H. Nyembo Uvinza (mpya)
37. Ernest N. Kahindi Nyasa (mpya)
38. Peter T. Kiroya Simanjiro
39. John V. K. Mongella Arusha
40. Baraka M. Konisaga Nyamagana
41. Husna Mwilima Mbogwe (mpya)
42. Sophia E. Mjema Temeke
43. Francis Isaac Chemba (mpya)
44. Abihudi M. Saideya Momba (mpya)
45. Khalid J. Mandia Babati
46. Anna Rose Nyamubi Shinyanga
47. Dani B. Makanga Kasulu
48. Amina J. Masenza Ilemela
49. Mercy E. Silla Mkuranga
50. Christopher R. Kangoye Mpwapwa
51. Lt. Edward O. Lenga Kalambo (mpya)
52. Halima O. Dendego Tanga
53. Lephy B. Gembe Dodoma
54. Saidi A. Amanzi Morogoro
55. Jackson W. Msome Musoma
56. Elias C. B. Goroi Rorya
57. Lt. Col. Benedict Kitenga Kyerwa (mpya)
58. Erasto Sima Bariadi
59. Nurdin H. Babu Mafia
60. Khanifa M. Karamagi Gairo (mpya)
61. Gishuli M. Charles Buhigwe (mpya)
62. Saveli M. Maketta Kaliua (mpya)
63. Darry Rwegasira Karagwe

Saturday, May 5, 2012

Baraza jipya hili hapa:


ORODHA YA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI


MAWAZIRI

1. OFISI YA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
Ndugu Stephen M. Wasira, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, (Utawala Bora)
Ndugu George Mkuchika, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (UTUMISHI)
Ndugu Celina Kombani, Mb.,

2. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MUUNGANO)
Ndugu Samia H. Suluhu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (MAZINGIRA)
Dr. Terezya P.L. Huvisa, Mb.,

3. OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji)
Ndugu Mary M. Nagu, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Hawa Ghasia, Mb.,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge)
Ndugu William V. Lukuvi, Mb.,

4. WIZARA

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Ndugu Samuel J. Sitta, Mb.,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Ndugu Shamsi Vuai Nahodha, Mb.,

Waziri wa Ujenzi
Dr. John P. Magufuli, Mb.,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dr. Hussein A.H. Mwinyi, Mb.,

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Dr. Shukuru J. Kawambwa, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Sophia M. Simba, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Bernard K. Membe, Mb.,

Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Mathias M. Chikawe, Mb.,

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Emmanuel Nchimbi, Mb.,

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Dr. David M. David, Mb.,

Waziri wa Kazi na Ajira
Ndugu Gaudentia M. Kabaka, Mb.,

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Prof. Makame M. Mbarawa, Mb.,

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Prof. Anna K. Tibaijuka, Mb.,

Waziri wa Maji
Prof. Jumanne Maghembe, Mb.,

Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum
Prof. Mark Mwandosya, Mb.,

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Eng. Christopher Chiza, Mb.,


Waziri wa Uchukuzi
Dr. Harrison Mwakyembe, Mb.,

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dr. Fenella E. Mukangara, Mb.,

Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Khamis Kagasheki, Mb.,

Waziri wa Viwanda na Biashara
Dr. Abdallah O. Kigoda, Mb.,

Waziri wa Fedha
Dr. William Mgimwa, Mb.,

Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo, Mb.,

5. NAIBU MAWAZIRI

OFISI YA RAIS
HAKUNA NAIBU WAZIRI

6. OFISI YA MAKAMU WA RAIS

Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais
Ndugu Charles Kitwanga, Mb.,

7. OFISI YA WAZIRI MKUU

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Majaliwa K. Majaliwa, Mb.,

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI)
Ndugu Aggrey Mwanry, Mb.,

8. WIZARA MBALIMBALI

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira
Dr. Makongoro M. Mahanga, Mb.,

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Ndugu Adam Malima, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi
Ndugu Pereira A. Silima, Mb.,

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara
Ndugu Gregory G. Teu, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi
Ndugu Benedict N. Ole-Nangoro, Mb.,

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Ndugu Mahadhi J. Maalim, Mb.,

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
Ndugu Goodluck J. Ole-Medeye, Mb.,

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
Ndugu Ummy A. Mwalimu, Mb.,

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Ndugu Philipo A. Mulugo, Mb.,

Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Abdulla Juma Abdulla, Mb.,

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Ndugu Lazaro Nyalandu, Mb.,

Naibu Waziri wa Ujenzi
Ndugu Gerson Lwenge, Mb.,

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,
Dr. Seif Suleiman Rashid, Mb.,

Naibu Waziri wa Nishati na Madini
Ndugu George Simbachawene, Mb.,

Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia
Ndugu January Makamba, Mb.,

Naibu Waziri wa Uchukuzi
Dr. Charles J. Tizeba, Mb.,

Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Ndugu Amos Makala, Mb.,

Naibu Waziri wa Maji
Eng. Dr. Binilith Mahenge, Mb.,

Naibu Waziri Nishati na Madini
Ndugu Stephen Maselle, Mb.,

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Ndugu Angela Jasmine Kairuki, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Janet Mbene, Mb.,

Naibu Waziri wa Fedha
Ndugu Saada Mkuya Salum, Mb.

Bila shaka wengi wanataka kuwafahamu waliopoteza nyadhifa zao. Orodha hii mpya ndefu nimepembua kujua ni nani yumo na ni nani hayumo, na yafuatayo ni majina ya waliokuwa Mawaziri ambayo siyaoni kwenye safu mpya:
  1. Aliyekuwa Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo
  2. Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja
  3. Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige
  4. Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Omary Nundu
  5. Aliyekuwa Waziri wa Afya, Dkt. Hadji Mponda
  6. Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami