Search This Blog

Friday, April 20, 2012

KANUNI INASEMAJE juu ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu?

SEHEMU YA KUMI NA TATU (ya kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007)
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

133.-(1) Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa
Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
kwa mujibu wa Ibara ya 53A ya Katiba.

(2) Hoja yoyote ya kutaka kupitisha Azimio la kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu haitatolewa Bungeni endapo:-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya
Waziri Mkuu yaliyoainishwa katika Ibara ya 52 ya
Katiba;

(b) hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(c) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa; au

(d) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa
kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa
na Bunge isipokuwa tu kama:-

(a) taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na
kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua
asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa
kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne
kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;

(b) Spika ataridhika kuwa masharti ya Katiba kwa
ajili ya kuleta hoja hiyo yametimizwa.

(4) Hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya
Katiba, itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na
itaamuliwa kwa kura za siri.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo
inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa
na Bunge kwa kupigiwa kura na Wabunge walio wengi, Spika
atawasilisha Azimio hilo kwa Rais na mapema iwezekanavyo na
kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha
Azimio hilo, Waziri mkuu atajiuzulu na Rais atamteua mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu
 

No comments:

Post a Comment