Search This Blog

Monday, April 23, 2012

SAINI ZIMETIMIA!!!!!!!!!!


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU BUNGENI KWA MUJIBU WA KATIBA
IBARA YA 53A NA KANUNI YA BUNGE, KIFUNGU CHA 133 KUWASILISHWA KWA
SPIKA KESHO TAREHE 23/04/2012


• Masharti yametimizwa; wabunge 73 wazalendo wamesaini
• Ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’


Mnamo tarehe 19/04/2012 wakati nahitimisha hoja ya Kamati ya Bunge ya
Mashirika ya Umma nilieleza kusudio langu la kuwaomba waheshimiwa
wabunge waniunge mkono katika kutia saini zisizopungua asilimia 20 ya
wabunge wote ili kuweza kutimiza matakwa ya Katiba ibara ya 53A kwa
ajili ya kuwasilisha Bungeni hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.
Mnamo tarehe 20/04/2012 niliandaa orodha ya waheshimiwa wabunge wote
na kuisambaza ndani na nje ya ukumbi wa Bunge ili waheshimiwa wabunge
wote waweze kutia saini hizo, na mpaka leo tarehe 22/04/2012 orodha
hiyo imetimiza idadi ya wabunge wazalendo wanaopigania uwajibikaji 73
kutoka vyama vyote vyenye uwakilishi Bungeni, isipokuwa chama cha UDP
ambacho kina Mbunge 1 na hajatia saini waraka huo mpaka sasa.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kifungu cha 133 (1) kinasomeka “Mbunge
yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa Spika ya kutaka kuleta
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa mujibu wa ibara ya 53A ya
Katiba” na kwa mujibu wa kifungu kidogo cha (3) kinasomeka “hoja ya
kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa na Bunge
isipokuwa tu kama;


(a) “taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na kuungwa mkono na Wabunge
wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote itatolewa kwa Spika, siku
zisizopungua kumi na nne kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;”


Hali kadhalika kanuni za Bunge Kifungu cha 133 (4) kinasomeka kuwa
“hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya
Katiba,itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na itaamuliwa kwa
kura za siri”.


Hivyo basi baada ya kutimiza matakwa ya kikatiba na kanuni za Bunge
kesho tarehe 23/04/2012 tutawasilisha rasmi kwa Spika Taarifa ya
Maandishi kwa mujibu wa kanuni 133 (1) na (3) ya hoja ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu kwa kushindwa kusimamia uwajibikaji wa Serikali
Bungeni kwa mujibu wa ibara ya 52 na hivyo kulinda Mawaziri wenye
kusababisha matumizi mabaya ya fedha za umma na kulisababishia hasara
taifa.


Tunatarajia kwamba siku kumi na nne baada ya kuwasilisha hoja hiyo
Bunge litakutana kwa haraka kujadili hoja hiyo ili kuwezesha
uwajibikaji na hatua kuchukuliwa za kuhakikisha mapendekezo ya ripoti
za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na maazimio ya Bunge
yanatekelezwa. Hoja hii ni mwendelezo wa ‘Operesheni Uwajibikaji’
hivyo tunaomba wabunge wazalendo na watanzania wote waiunge mkono ili
kuimarisha Uwajibikaji wa Viongozi, kupambana na ubadhirifu na
kunusuru uchumi wa nchi na kuchangia katika ustawi wa wananchi.
Kwa niaba ya wabunge wazalendo waliotia saini kuunga mkono taarifa ya
hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu ni;

…………………………….
Kabwe Zuber Zitto.
Mbunge Jimbo la Kigoma Kaskazini.
22/04/2012.

Sunday, April 22, 2012

Wabunge wazalendo hawa hapa:

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefanya zoezi la kukusanya sahihi za wabunge ili aweze kuwasilisha bungeni hoja kutokuwa na imani na waziri mkuu. Picha na Edwin Mjwahuzi
Saturday, April 21, 2012 5:46 AM01. Mhe. Rashid Ali Abdallah – cuf
02. Mhe . Chiku Aflah Abwao- chadema
03. Mhe . Saluim Ali Mbarouk – cuf
04. Mhe . salum Khalfam Barwany – cuf
05. Mhe . Deo Haule Filikuchombe- ccm
06. Mhe.Pauline Philipo Gekul- chadema
07. Mhe. Asaa Othman Hamad-cuf
08. Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
09. Mhe.Naomi Mwakyoma Kaihula – chadema
10. Mhe . Sylvester Kasulumbayi- chadema
11. Mhe. Raya Ibrahim Khamis - chadema
12. Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga - cuf
13. Mhe. Susan Limbweni Kiwanga- chadema
14. Mhe. Grace Sindato Kiwelu –chadema
15. Mhe. Kombo Khamis Kombo – cuf
16. Mhe. Joshua Samwel Nassari – chadema
17. Mhe. Tundu Antiphas Lissu- chadema
18. Mhe Aphaxar Kangi Lugola- ccm
19. Mhe susan Anselim Lymo- chadema
20. Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
21. Mhe. John Shibuda Magalle – Chadema
22. Mhe. Faki Haji Makame- Cuf
23. Mhe . Esther Nicholas Matiko- chadema
24. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
25. Mhe. Freman Aikaeli Mbowe- chadema
26. Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – chadema
27. Mhe. Halima James Mdee-chadema
28. John John Mnyika- Chadema
29. Mhe. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
30. Mhe . Maryam Salum Msabaha- chadema
31. Mhe. Peter Msingwa-chadema
32. Mhe. Christowaja Gerson Mtinda- chadema
33. Mhe. Philipa Geofrey Mturano- chadema
34. Mhe. Christina Lissu Mughwai- chadema
35. Mhe. Joyce John Mukya – chadema
36. Mhe. Mchungaji Israel Yohane Natse – chadema
37. Mhe. Philemon Ndesamburo- chadema
38. Mhe. Ahmed Juma Ngwali- - cuf
39. Mhe. Vincent Josephat Nyerere- chadema
40. Mhe. Rashid Ali Omar- cuf
41. Meshack Jeremiah Opulukwa- chadema
42. Mhe. Lucy Philemon Owenya- chadema
43. Mhe. Rachel Mashishanga- Chadema
44. Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – chadema
45. Mhe. Conchesta Rwamlaza – Chadema
46. Mhe. Moza Abedi Saidy- cuf
47. Mhe. Joseph Roman Selasini – Chadema
48. Mhe. David Ernest Silinde- chadema
49. Mhe Rose Kamili Sukum - chadema
50. Mhe. Cecilia Daniel Paresso- chadema
51. Mhe .Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
52. Mhe. Magdalena Sakaya – Cuf
53. Mhe Rebecca Mngodo- Cuf
54. Mhe. Sabreena Sungura -chadema
55. Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
56. Mhe. Rukia Kassim Ahmed (Cuf)
57. Mhe. Mustapha Boay Akoonay (Chadema)
58. Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
59. Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
60. Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
61. Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
62. Mhe Haji Khatibu Kai (CUF)
63. Mhe. Anna Marystella John Malack -Chadema
64. Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF)
65. Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
66. Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
67. Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
68. Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
69. Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
70. Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
71. Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)

Saturday, April 21, 2012

Breaking news: Mawaziri 7 wajiuzulu

Taarifa za uhakika zilizotufikia ni kuwa Mawaziri waliokubali kujiuzulu  ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami;  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

 
Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni:
 
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu. 

Friday, April 20, 2012

Picha ya wiki


Kama vile anasema "Aaaaaah jamani si mimi ni mkulima tu, hayo mengine siyajui wajameni"

Mmmmmmmmmmmh

KANUNI INASEMAJE juu ya hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu?

SEHEMU YA KUMI NA TATU (ya kanuni za kudumu za Bunge Toleo la 2007)
HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU

133.-(1) Mbunge yeyote anaweza kutoa taarifa ya maandishi kwa
Spika ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu
kwa mujibu wa Ibara ya 53A ya Katiba.

(2) Hoja yoyote ya kutaka kupitisha Azimio la kura ya kutokuwa na
imani na Waziri Mkuu haitatolewa Bungeni endapo:-

(a) haina uhusiano na utekelezaji wa majukumu ya
Waziri Mkuu yaliyoainishwa katika Ibara ya 52 ya
Katiba;

(b) hakuna madai kwamba Waziri Mkuu amevunja
Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(c) haijapita miezi sita tangu alipoteuliwa; au

(d) haijapita miezi tisa tangu hoja ya namna hiyo
ilipotolewa Bungeni na Bunge likakataa
kuipitisha.

(3) Hoja ya kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu haitajadiliwa
na Bunge isipokuwa tu kama:-

(a) taarifa ya maandishi iliyowekwa saini na
kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua
asilimia ishirini ya Wabunge wote itatolewa
kwa Spika, siku zisizopungua kumi na nne
kabla ya siku inayokusudiwa kuwasilishwa
Bungeni;

(b) Spika ataridhika kuwa masharti ya Katiba kwa
ajili ya kuleta hoja hiyo yametimizwa.

(4) Hoja inayotolewa chini ya Kanuni hii na iliyotimiza masharti ya
Katiba, itawasilishwa Bungeni mapema iwezekanavyo na
itaamuliwa kwa kura za siri.

(5) Hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa tu iwapo
inaungwa mkono na Wabunge walio wengi.

(6) Endapo hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu itapitishwa
na Bunge kwa kupigiwa kura na Wabunge walio wengi, Spika
atawasilisha Azimio hilo kwa Rais na mapema iwezekanavyo na
kwa vyovyote vile ndani ya siku mbili tangu Bunge lilipopitisha
Azimio hilo, Waziri mkuu atajiuzulu na Rais atamteua mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu
 

SAKATA LA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU: Unafiki wa wabunge wa CCM huu hapa

Hadi sasa hivi ni wabunge wawili (2) tu wa CCM kati wa 54 waliokwisha saini kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Kama walikuwa wanaongea kwa hasira toka juzi inashindikana nini kutokusaini??

Angalia orodha hii:
Majina ya Wabunge walio-sign Vote of No Confidence hadi sasa hivi 1.Rashid Ali Abdallah CUF
2.Chiku Aflah Abwao CDM
3.Salum Ali Mbarouk CUF
4.Salum Khalfam Barwany CUF
5.Deo H Filikuchombe- CCM
6.Pauline P. Gekul-CDM
7. Asaa O Hamad-CUF
8.Prof.Kuliyokela Kahigi- CDM
9.Naomi M Kaihula – CDM
10.Sylvester Kasulumbayi- CDM
11. Raya Ibrahim Khamis - CDM
12.Mkiwa H. Kiwanga CUF
13.Susan L Kiwanga-CDM
14.Grace S Kiwelu CDM
15. Kombo Khamis Kombo – CUF
16. Joshua S Nassari –CDM
17. Tundu A Lissu- CDM
18. Aphaxar K Lugola- CCM
19. Susan A Lyimo- CDM
20. Moses Machali – NCCR
21. John Shibuda Magalle CDM
22. Faki Haji Makame-CUF
23. Esther N Matiko-CDM
24. Joseph Mbilinyi- CDM
25.Freeman Mbowe- CDM
26. Kurudhum J. Mchuchuli – CDM
27.Halima Mdee-CDM
28.John Mnyika- CDM
29. Augustino L Mrema- TLP
30. Maryam S Msabaha- CDM
31. Peter Msingwa-CDM
32. Christowaja G Mtinda CDM
33. Philipa G Mturano- CDM
34. Christina L Mughwai- CDM
35.Joyce Mukya – CDM
36.Israel Y Natse – CDM
37. Philemon Ndesamburo- CDM
38.Ahmed Juma Ngwali-CUF
39. Vincent Nyerere- CDM
40.Rashid Ali Omar-CUF
41.Meshack J Opulukwa- CDM
42. Lucy Owenya- CDM
43.Rachel Mashishanga- CDM
44. Mhonga Ruhwanya – CDM
45.Conchesta Rwamlaza – CDM
46. Moza Abedi Saidy-CUF
47. Joseph R Selasini – CDM
48.David E Silinde-CDM
49.Rose Kamili - CDM
50. Cecilia Paresso- CDM

51.Kabwe Zuberi Zitto- CDM
52. Magdalena Sakaya – CUF
53. Rebecca Mngodo- CDM
54. Sabreena Sungura -CDM

Thursday, April 19, 2012

CCM YAZIDI KUBOMOKA

 
UPEPO mbaya unaonekana kukikumba Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa viongozi wake kukihama chama hicho, umeingia katika Mkoa wa Mwanza, ambapo Diwani wa Kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema mkoani hapa, Hamis Mwangao Tabasamu ametangaza kuihama CCM na kujiunga na Chadema.

Diwani huyo ambaye amejipambanua kwa kupiga vita ufisadi ndani ya wilaya hiyo, ametangaza azma yake hiyo katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika Ryan's hoteli, na kupokelewa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema).

Diwani Tabasamu ambaye jumamosi amepanga kuhudhuria na kuhutubia mkutano mkubwa utakaoongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbrod Slaa kata ya Nyampulukano, amekuwa ni miongoni mwa viongozi wengine wa CCM kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema ndani ya muda wa wiki moja.

Hivi karibuni, aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Mkoa wa Arusha, James Milya alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote kisha kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Mbali na Milya, viongozi wengine kadhaa akiwemo diwani wa Kata ya Sombetini mkoani Arusha, Alphonce Mawazo (CCM), juzi alikihama chama chake hicho kisha kujiunga na Chadema, chama ambacho kinaonekana kuiweka pabaya CCM na Serikali yake kwa ujumla.

Akizungumza mchana huu wa leo, katika kikao chake na waandishi mbele ya Lema ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Taifa, diwani Tabasamu ambaye aliwahi kuibua tuhuma za ufisadi katika halmashauri ya Wilaya ya Sengerema alisema: "Kuanzia leo (jana), natangaza rasmi kukuhama CCM na kujiunga na Chadema".

Alisema, lengo lake la kuhama kutoka ndani ya CCM si la kushawishiwa na mtu ama kiongozi yeyote, bali ni dhamira yake ya kweli kama Mtanzania halisi mwenye uhuru wa mawazo, na kwamba amechoshwa na siasa za 'majitaka' ndani ya CCM.

Kwa mujibu wa diwani huyo wa Nyampulukano wilayani Sengerema, kuondoka kwake CCM inatokana na kushindwa kuafikiana katika maslahi ya wananchi, ambapo alidai wapo baadhi ya viongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo wanakumbatia vitendo vya kifisadi.

"Uamuzi wangu huu wa kuhamia Chadema kutoka CCM unatokana na kushindwa
kuafikiana katika mambo yanayogusa maslahi ya wananchi katika
halmashauri ya wilaya ya Sengerema.

"Mafisadi wameliteka baraza la Madiwani la Sengerema!. Kwa maana hiyo natangaza rasmi leo, najiuzulu nafasi zangu zote ndani ya CCM, na nahamia Chadema", alisema Tabasamu ambaye amewahi kuingia mgogoro na mkuu wa wilaya hiyo, Elinas Palagyo kwa kile kinachodaiwa msimamo wake wa kupiga vita ufisadi.

Alizitaja sababu nne za kuhama ndani ya chama hicho tawala kuwa ni pamoja na kuwepo kwa madiwani wengi wa CCM wasio wazalendo kwa kuruhusu kuhamishwa mnada wa ng'ombe kutoka Kijiji cha Ibondo Nyampulukano kisha kuhamishiwa Kata ya Sima.

Sababu nyingine ni ucheleweshaji wa makusudi kuunda halmashauri ya mji
wa Sengerema kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka huu, kupunguzwa kwa mipaka ya mji mdogo bila kufuata vikao halali vya kisheria.

Nyingine ni halmashauri ya wilaya hiyo ya Sengerema, iliyopo chini ya uenyekiti wake, Mathew Lubongeja (CCM), kushindwa kuwachukulia hatua watu aliowaita wezi waliotajwa na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), PPRA, ambapo alidai maelekezo ya CAG kuhusu kuchukuliwa hatua watuhumiwa wa ufisadi kutotekelezwa hadi leo.

Awali, akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari, Lema alimpongeza diwani huyo wa Nyampulukano kwa kuondoka ndani ya CCM na kujiunga na Chadema, na alisema huo ni uamuzi sahihi na wa kijasiri unaolenga kuikomboa nchi hii kutoka CCM.

"Nakupongeza sana mheshimiwa Tabasamu kwa kuondoka CCM na kuja Chadema chama makini. Nawaomba sana na madiwani, wabunge na viongozi wengine wa CCM wawahi kujiunga na Chadema kabla safina haijafungwa", alisema Lema.

Tuesday, April 3, 2012

CCM kwisha kazi

Image Detail


Hakuna ubishi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeisha, kimeishiwa, kinachusha na kimeishachokwa na watanzania kutokana na uhuni ambao kimekuwa kikiufanya kwa miaka zaidi ya 50.


Baada ya kung'atuka kwa mwanzilishi wake marehemu mwalimu Julius Nyerere, mvuto wa chama ulikwisha hasa baada ya kuanzishwa kwa sera mama ya ufisadi iliyojulikana kama Ruksa chini ya aliyemrithi mwalimu, Ali Hassan Mwinyi ambaye hata hivyo hatajwi sana kwenye ufisadi ingawa ndiye chimbuko lake.


Mwinyi licha ya kuanza kubomoa misingi madhubuti hasa maadili ya uongozi, alimchosha Nyerere kiasi cha Nyerere kudhani kuwa angeweza kupata mtu aliyemuamini na kumfahamu ambaye angerejesha chama kwenye mstari. Kosa kubwa! Mwalimu alimpendekeza na kumpigia debe mwanafunzi wake Benjamin William Mkapa aliyekuwa rais wa awamu ya tatu na ambaye atakumbukwa kwa kusimika mizizi ya ufisadi na ujambazi kwenye serikali ya Tanzania. Mkapa alivuruga akafanya biashara ikulu na kujimilkisha mali ya umma. Ili kujihakikishia usalama baada ya kufanya uhujumu kwa taifa, Mkapa alianzisha na kuunga mkono wizi wa pesa ya umma chini ya kashfa maarufu ya EPA.


Pesa ya EPA ilitumika kuhonga, kuchafuana,kupambana na hata kumalizana kisiasa nyenzo alizotumia rais wa sasa Jakaya Kikwete ambaye naye ameonekana kushabikia ufisadi kuliko hata Mkapa kutokana naye kuwa tunda la ufisadi. Huo ndiyo uhuni wa CCM tangu aachie ngazi Mwalimu Nyerere.


Ila kadri siku zinavyokwenda watanzania wanaanza kung'amua uhuni wa CCM kiasi cha kuanza kuitia adabu. Mfano wa karibu ni uchaguzi mdogo uliopita huko Arumeru Mashariki ambapo CCM ilipoteza pamoja na kujaribu upuuzi na uhuni wote bila mafanikio. Hakuna jambo ambalo limeivua nguo CCM licha ya uhuni wake wa muda mrefu kama kuwatumia wapiga debe wasiopiga miswaki sawasawa. Hawa ni kuanza Mkapa, waziri katika ofisi ya rais, Stephen Wassira na baba yao Livingstone Lusinde waliogeuza sera za chama kuwa uongo na matusi tena ya nguoni.


Hakika CCM inaanza kupata pensheni ya uhuni wake huku ikivuna ilichopanda. Je huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM? Alluta Continua.