Search This Blog

Friday, May 20, 2011

ETI KESHO NI MWISHO WA DUNIA???????

Nilisikia redioni, nikasoma mtandaoni na kwenye baadhi ya media, nikajionea na picha za watu wanaoamini kuwa kesho kutwa yaani tarehe 21 ni mwisho wa dunia, wanadai wamefunuliwa na ati imeandikwa hivyo ndani ya Biblia.  

Mwanzilishi wa UVUMI ama "UNABII" huo ni Mtangazaji wa na Rais wa Family Radio,  Harold Camping 
Camping anasema Tarehe 21 Mei ni siku ya unyakuo kwa wateule na kuwa miezi mitano baadaye yaani trh 21 Oktoba ndio mwisho wa dunia.  anadai hii ni kwa mujibu wa Biblia, japo sijaona popote anaponukuu andiko lisemalo hivyo. 
Kiasi gani mtabiri huyu yu sahihi? hii yanikumbusha Kibwetere wa Uganda. Je historia kujirudia???
Only time will tell. 
...and this is the Calculation as per Harold Camping:-

Another argument that Camping uses in favor of the May 21st date is as follows:
1. According to Camping, the number five equals "atonement", the number ten equals "completeness", and the number seventeen equals "heaven".

2. Christ is said to have hung on the cross on April 1, 33 AD. The time between April 1, 33 AD and April 1, 2011 is 1,978 years.

3. If 1,978 is multiplied by 365.2422 days (the number of days in a solar year, not to be confused with the lunar year), the result is 722,449.

4. The time between April 1 and May 21 is 51 days.

5. 51 added to 722,449 is 722,500.

6. (5 × 10 × 17)2 or (atonement × completeness × heaven)2 also equals 722,500.
Thus, Camping concludes that 5 × 10 × 17 is telling us a "story from the time Christ made payment for our sins until we're completely saved.

CHADEMA -IRINGA: nguvu zadi



Friday, May 6, 2011

UFISADI WA RIDHIWANI KIKWETE, DR SLAA NINAMUAMINIA!!


Sakata linalomhusu Ridhiwani Kikwete,mtoto wa Mhe. Jakaya Kikwete-kwa upande mmoja,na Katibu Mkuu wa Chadema Dkt Willibroad Slaa na Mwenyekiti wa chama cha DP,Mchungaji Christopher Mtikila-kwa upande mwingine, lina ukweli ndani yake. Ndani ya siku saba zilizotolewa na Ridhiwani kwa Dr. Slaa na Mtikila ili wakanushe lakini ebu tuangalie mazingira ya hili sakata yamekaaje.
Ridhiwani ni mwanasheria kitaaluma,pia  ni mtoto wa Mhe. Kikwete,kwa maana nyingine ufisadi huu unamhusisha pia baba yake (kwa maana ya kutumia fursa ya urais kumnufaisha mwanaye) inatarajiwa kuwa suala hapa sio kujisafisha yeye tu bali pia baba yake. Lakini kwa kuwa Dr. Slaa ni makini haya mazingira ni mepesi sana kwake kuyashughulikia.

Dokta Slaa,wengi tunamfahamu kama mmoja wa wanasiasa adimu kabisa ambao ni nadra kutoa matamshi pasipo kuyafanyia utafiti wa kutosha na kuwa na uthibitisho. Dr. Slaa hayumbishwi na nafasi ya mtu katika chama na serikali hasa linapojitokeza suala la uwajibikaji. Na pengine Mchungaji Mtikila, wengi tunafahamu kuwa Mtikila na mahakama ni kama mtu na nyumbani kwake na bado anatambulika kuwa anapoamua kupigania haki basi atakwenda umbali wowote ule pasipo kuchelea madhara ya kufanya hivyo.

Jumatatu ndo tutajua ukweli maana kama ni  kweli ufisadi wa Ridhiwani ukithibitika basi ni pesa zetu ndo ametafuna na kujinufaisha yeye na familia yake.
Aluta kontinua!!!!!!!!!!!!!!

Hii imekaaje???

Oyaaaaaaaaaaa!!!!! Chunga sana!!

Tuesday, May 3, 2011

OSAMA AUAWA

Osama bin Laden Mwanzilishi na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden, ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Pakistan, rais Obama amesema. Kiongozi huyo wa al Qaeda aliuwawa baada ya makabiliano na wanajeshi wa Marekani nje ya mji wa Islamabad kwa mujibu wa taarifa za kijasusi. Bw Obama amasema baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani yaliuchukua mwili wake. Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001. Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la al Qaeda lakini kuna hofu kuwa huenda kukatokea mashambulio ya kulipiza kisasi. Msako Bw Obama amesema taarifa za mahali alikojificha zilianza kupatikana Agosti mwaka jana. Kufuatia uchunguzi wa ujasusi waligundua amejificha mjini Pakistan. Wiki iliyopita rais Obama alitoa amri kwa shughuli ya ''kumsaka bin Laden'' kufanyika. Bw Obama amesema operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, kaskazini mwa Islamabad. ''Baada ya ufyatulianaji wa risasi, bin Laden aliuwawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani'' rais Barack Obama amesema. KUNRADHI kwa picha hiyo hapo chini.


Osama baada ya kipigo:
WASIFU WA OSAMA BIN LADENOsama bin Laden alizaliwa mwaka wa 1957, katika familia ya kitajiri nchini Saudi Arabia Ana zaidi ya ndugu na dada 50. Babayake Osama alimiliki kampuni kubwa ya ujenzi. Katika baadhi ya picha zake za utotoni, Osama ameonyeshwa akiwa amevalia mavazi ya kifahari na ya gharama kubwa, akiwa likizo katika miji mbali mbali barani Ulaya. Hata hivyo mwanzoni mwa miaka ya themanini alitapa mgongo maisha haya ya kifahari na kitajiri na kujiunga na vuguvugu la kupigania haki dhidi ya utawala wa Kisovieti baada ya majeshi yake kuishambulia Afghanistan. Wakati huo, akipigana pamoja na Waarabu wenzake, alizindua kundi la kigaidi la Al Qaeda. Mnamo mwaka wa 1998, alitangaza fatwa yaani vita vikali vya kidini dhidi ya Marekani. Osama alisema alikasirishwa na hatua ya Marekani kuweka majeshi yake katika ardhi ya Kiislamu, katika nchi mbalimbali Mashariki ya Kati. Alioa mke wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17 na baadaye akawaoa wake wengine wanne. Osama Bin Laden anaaminika kuwa na watoto 17.


BUSU LA KUMBUKUMBU

Kushoto ni Baba, na Kulia ni Mwana.