Search This Blog

Wednesday, August 31, 2011

Eid Mubarak

Blog hii inawatakia Eid Mubarak

KIZUNGUMKUTI CHA VITAMBULISHO VYA TAIFA.


Mchakato wa Vitambulisho vya Taifa umeanza tangu mwaka 2007 (kama sikosei). Ni baada ya Baraza la Mawaziri kuubariki Februari 2 mwaka huo. Mwaka 2012 mchakato huu utatimiza miaka mitano. Unagharimu Shilingi bilioni 222! Hiki ni kioja !
Maana; mpaka mradi huu uje ukamilike, basi, yumkini kuna watanzania ambao watakuwa wameshakufa hata bila kuvikamata hivyo vitambulisho vyenyewe. Na pia tujiulize; katika hali yetu ya sasa, mradi wa vitambulisho vya kitaifa unakwamishwa na nini? Kwa hali hii kama wananchi walio wengi wangeambiwa wachague leo, kati ya kitambulisho na nafuu ya bei ya mafuta na sukari, basi, haraka wangechagua kuwepo kwa unafuu wa mafuta na sukari.

Ni tangu enzi za Waziri Joseph Mungai, akaja Lawrence Masha, na sasa Vuai Nahodha. Kila mmoja anakuja na lwake! Bunge la Bajeti 2009 yalisemwa haya na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha:“Naomba kuwathibitishia Watanzania kupitia Bunge lako tukufu kwamba, mradi wa vitambulisho utakamilika kwa kufuata sheria na utaratibu, bila mizengwe, kwa uwazi unaostahili na bila upendeleo,”
Akasimama mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, (CCM) na kusema kwa jazba;“Kama waziri mwenyewe hajui kinachoendelea katika wizara yake ina maana hakuna kinachoendelea. Halafu anatuambia mchakato unaendelea, mchakato gani huo?” aliuliza Shelukindo.
Naibu Spika Anne Makinda akasimama na kutamka: “Mheshimiwa waziri na mheshimiwa mbunge, hapa tunasikilizwa na wananchi nchi nzima. Wanachotaka kujua ni je; vitambulisho watavipata au hawatavipata? Hilo ndilo wanalohitaji na sio kuna nini”.
Waziri Masha akasimama na kusema; ” Mheshimiwa Naibu Spika, vitambulisho vitapatikana ndani ya mwaka huu wa fedha 2009/2010.”
Naam, mpaka hii leo ni August 2011 hakuna cha kitambulisho cha kitaifa wala nini! Waziri Masha alituongopea Watanzania, na hajawahi kutuomba radhi na hayuko tena bungeni. Nani wa kutuomba radhi kwa uongo huu wa serikali ya CCM?????

Serikali iwe wazi kama kuna tatizo la utekelezaji wa mradi wa vitambulisho vya taifa lieleweke ili wadau waweze kutoa maoni mazuri ya uharakishaji wa utekelezaji huo.
Nawasilisha.

Thursday, August 18, 2011

Raha ya SIMBA SC ilipatikana hivi.......

Mafisango akimdhibiti Nsajigwa

Cholo akimdhibiti Tegete

Boban na ball control.....Nsajigwa mmmmh!!!

Victor Costa na Tegete

Cholo akihakikisha Kiiza hapiti

Goooooooooooooooooooooooooooo!!!!!!!!!

Kiduku.....................

Ngao ya Jamii ikikabidhiwa kwa Kaseja wa Simba Sports Club

Thursday, August 11, 2011

HAPPY BIRTHDAY, SOPHY

Salaam na Heri ya maisha marefu.
Natumai kuwa u-mzima na unaendelea vema na harakati za mapambano ya maisha.
Blog hii inakutakia maisha marefu kwa kuonyesha MANENO mazuri, MATENDO safi na MAWAZO thabiti.  Happy birthday  to you!!!




Sunday, August 7, 2011

CHADEMA YATIMUA MADIWANI 5 ARUSHA

CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI DODOMA.
Kamati Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :

1. 
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia wala kuutambua mwafaka huo. 


2. 
Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza maelekezo hayo.
3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.

Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama wa CHADEMA wa uwajibikaji.

Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu:


i) 
Ndugu Estomih Mallah


ii) 
Ndugu John Bayo


iii) 
Ndugu Charles Mpanda
iv) Ndugu Rehema Mohamed

v) 
Ndugu Reuben Ngowi
Watajwa hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07 Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.
4. Aidha, Kamati Kuu imepokea taarifa ya mazungumzo baina ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, na Waziri Mkuu, Mhe Mizengo Pinda, juu ya nia na azima ya kumaliza tatizo la mgogoro wa umeya Arusha, waliyoyafanya asubuhi ya siku ya Jumamosi, Tarehe 06 Agosti 2011 nyumbani kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma.

Kamati imezingatia kuwa:
a. Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu wamekubaliana kuunda Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia mgogoro wa umeya wa Arusha itakayojumuisha wajumbe kutoka sehemu mbili zinazohusika katika mgogoro huu ambazo ni CCM na CHADEMA

b. 
Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano itaundwa haraka iwezekanavyo, na kwa vyovyote mgogoro wa u meya Manispa ya Arusha ulikubalika uishe ndani ya mwezi mmoja tangu tarehe ya mazungumzo ya Mwenyekiti wa Taifa na Waziri Mkuu


c. 
Uenyekiti wa Kamati ya Kitaifa utakuwa chini ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Ndugu John Tendwa, na kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa ataratibu uundwaji wa Kamati hiyo ya Kitaifa.


5. 
Kamati Kuu imetambua juhudi za Waheshimiwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, kwa hatua yao chanya ya kumaliza mgogoro wa Arusha.


6. 
Pamoja na hatua njema kuelekea kumaliza mgogoro wa umeya Arusha, Kamati Kuu ya CHADEMA itaendelea kusitisha kumtambua rasmi Meya wa Arusha hadi pale mazungumzo yaliyoanishwa hapo juu yatakapokamilika na mwafaka bayana kupatikana.
Imetolewa na:……………….Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
MWENYEKITI WA TAIFA

Saturday, August 6, 2011

Mpango wa kuinua elimu nchini huu hapa!!!! Wadau mpo???

Mwalimu wa Shule ya Msingi Bungo mkoani Morogoro akisimamia mitihani ya darasa la nne

nani anayemuonea mwenzake HURUMA? je ni anayetoa futari au anayepokea? Check picha.

Hapa mtoto yatima kuna kitu moyoni mwake anajiuliza na kushangaa!!! Lakini mtoaji wa futari wala inaonekana hajali mshangao wa mtoto!! Kuna  jambo zito mtoto analo moyoni. Kuna siku atasema!!!