Search This Blog

Tuesday, September 27, 2011

JE HII NDIYO TANZANIA TUNAYOITAKA WAKATI WA UCHAGUZI??

CCM ndo wanaoongoza kwa ushawishi wa vurugu maeneo mengi kama Igunga kwa kuwatisha wananchi ili ichaguliwe. Je ndiyo Tanzania tunayosikia ni nchi ya amani? Kama ni amani mbona Viongozi kama huyu Aden Rage anapiga kampeni akiwa na bastola kiunoni. Nijuavyo mimi kila mikutano ya adhara huwa kuna askari wa kulinda usalama. Inakuwaje silaha hadharani hivyo???

Thursday, September 15, 2011

HAMA HAMA YA WAKUU WA MIKOA TZ

Na. JINA LA MKUU WA MKOA KITUO AENDAKO KITUO ATOKAKO
1. Bw. Saidi Mecki Sadiki DAR ES SALAAM RC - Lindi
2. Bw. John Gabriel Tupa MARA DC - Dodoma
3. Bw. Saidi Thabit Mwambungu RUVUMA DC - Morogoro
4. Kanali Joseph Simbakalia MTWARA RC Kigoma
5. Bi. Chiku S. Gallawa TANGA DC - Temeke
6. Bw. Abbas Kandoro MBEYA RC Mwanza
7. Bw. Leonidas T. Gama KILIMANJARO DC – Ilala
8. Dkt. Parseko Ole Kone SINGIDA RC Singida
9. Eng. Stella Manyanya RUKWA Mbunge V/Maalum
10. Bibi Christine Ishengoma IRINGA RC Ruvuma
11. Dk. Rehema Nchimbi DODOMA DC - Newala
12. Bw. Elaston John Mbwillo MANYARA DC – Mtwara
13. Col. Fabian I. Massawe KAGERA DC - Karagwe
14. Bibi. Mwantumu Mahiza PWANI Mbunge/NW Mstaafu
15. Bibi. Fatma A. Mwassa TABORA DC - Mvomero
16. Bw. Ali Nassoro Rufunga LINDI DC - Manyoni
17. Eng. Ernest Welle Ndikillo MWANZA DC - Kilombero
18. Lt. Col. Issa Machibya KIGOMA RC Morogoro
19. Bw. Magesa S. Mulongo ARUSHA DC - Bagamoyo
20. Bw. Joel Nkaya Bendera MOROGORO Mbunge/NW Mstaafu
21. Bw. Ludovick Mwananzila SHINYANGA Mbunge/NW Mstaafu


Miaka 50 ya Uhuru: UKWELI NA UONGO!


Hivi ni kweli kabisa kuwa 09/12/2011 tunasherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania??Sasa hivi kila idara ya serikali, mashirika na taasisi zake zinafanya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru.
Hebu tutafakari kwa akili huru kwa pamoja
1. Tanzania ilizaliwa mara baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kuungana tarehe 26/04/1964 ambako mpaka leo ni miaka 47 ya muungano kwa maana hiyo Tanzania ina miaka 47 na sio 50 kama tunavyorubuniwa nah ii serikali na kutumia fedha nyingi kutangaza eti miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
2. Kwanini Serikali isiseme tunasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika au Tanzania Bara badala ya kuendelea kusema Tanzania?? Na kama dhana ni miaka 50 ya uhuru basi ni UHURU wa TANGANYIKA na siyo Tanzania.
3. Siku ya sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania kama wanavyosema wimbo gani wa Taifa utaimbwa?Mungu Ibariki ambao ni wimbo wa taifa Tanganyika na Zanzibar kwa Ujumla au utaimbwa uliokuwa wimbo wa Tanganyika? Au ule wa wasanii wa bongoflava??
4. Siku ya sherehe bendera gani itapeperushwa na kupandishwa?hii inayotumika sasa ikiashiria Muungano wa Tanganyika na Zanzibar au ile ya Tanganyika ambayo daima mzee  Mtikila huipandisha?
5. Mgeni Rasmi atakuwa nani?Mhe Jakaya Kikwete ambae ni Rais wa jumla wa Tanzania bara na Zanzibar?
Imefika wakati wa kuwa na Bendera ya Tanganyika kama ilivyo Zanzibar, Jina la Tanganyika likaendelea kuwepo na kutambulika kama lilivyo la Zanzibar, Heri tukawa na Wimbo wa Taifa la Tanganyika kama ilivyokuwa zanzibar
Mbona Zanzibar wakisherehekea miaka yao mapinduzi huwa wanapandisha bendera yao?mbona wao wana imba nyimbo za kusifu mapinduzi na wimbo wa taifa lao?
Nawasilisha!!!!!!!



Monday, September 12, 2011

Katuni ya leo

CCM wameanza kwa kuhonga wali Igunga

Hapa ni wali

Hapa wakisomba watu kuwapeleka mkutanoni??
Jamani waungwana.....Hii siyo rushwa???

Hisia za Mhe. Zitto Kabwe juu ya msiba huu wa kitaifa

Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu Shakani
by Zitto Z Kabwe on Sunday, 11 September 2011 at 16:19

(Nimeandika makala hii nikiwa katika Benchi la Hospitali ya Mnazi
 
Mmoja hapa Zanzibar. Mniwie radhi kama kuna spelling mistakes kwani
nilitaka hisia zangu ziwe as raw as possible - Zitto Zitto and not
Zitto a Politician).

Jana asubuhi tarehe 10 Septemba 2011 Taifa liligubikwa na habari za
 
kushtusha za maafa. Mwanzoni taarifa zilisambaa kwamba zaidi ya watu
2000 walikuwa kwenye Boti MV Spice Islander lililopinduka na kuzama
mbele kidogo ya Nungwi likielekea kisiwani Pemba. Habari hazikuwa za
uhakika sana kwani vyombo vyetu vya habari na hasa Televeshini ya
Taifa havikuwa vikitoa habari juu ya ajali hii.

Habari zilisambaa kupitia mitandao ya intaneti na kufuatia uchu wa
 
habari nilianzisha #ZanzibarBoatAccident katika mtandao wa twitter ili
tuweze kufuatilia kwa karibu habari zote za ajali hii.

Habari zilisambaa kuwa Televisheni ya Taifa ilikuwa inaonyesha muziki
 
wa Taarab na Baadaye vipindi vingine vya kawaida bila kutoa habari kwa
Umma kuhusu msiba huu.

Watanzania waliokoa wakiwasiliana kupitia twitter na facebook walikuwa
 
na hasira sana na kituo cha TBC1 kutoonyesha au kupasha habari juu ya
ajali hii. Mpaka saa moja jioni kituo hiki cha Televisheni ya Taifa
kilikuwa kinaonyesha watu wakicheza muziki wa Kongo, wanawake
wakikatika viuno na hata ngoma za asili.

'Hallo, washa TBC1 uone Televisheni yenu inachoonyesha' yalikuwa ni
 
maneno ya Mwakilishi Ismael Jussa Ladhu aliponipigia kuonyesha
kusikitishwa kwake na kituo hiki. Mpaka jioni tulikuwa tumepata
taarifa kuwa Watanzania wenzetu 198 walikuwa wamepoteza maisha. 570
hivi walikuwa wameokolewa.

Binafsi nilipotembelea Hospitali ya Mnazi Mmoja niliweza kumwona Binti
 
aliyeitwa Leyla, akisoma darasa la Nne huko kisiwani Pemba. Leyla
alipona, aliokolewa. Nilimwambia leyla atapona na kurudi Shuleni.
Mpaka ninapoandika tumeambiwa kuwa Watanzania 240 wamegundulika
kupoteza maisha na zaidi ya 600 wameokolewa.

Napenda kuwapongeza sana waokoaji wetu, wavuvi wa kijiji cha Nungwi na
 
vijiji jirani, wamiliki wa mahoteli waliojitolea vifaa vyao kwenda
kuokoa watu na wanajeshi wetu wa majeshi ya ulinzi na usalama kwa kazi
hii kubwa ya kuokoa. Kwa kweli tumeokoa watu wengi kuliko
ilivyotarajiwa. Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi sana,
ilitulia na kuonyesha uongozi thabiti katika juhudi za uokoaji.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akafuta ziara yake huko
 
Canada, ziara iliyokuwa imeandaliwa muda mrefu na kwa gharama. Lakini
Rais aliona ni vema kupata hasara kuliko kuwa nje ya Nchi kipindi
hiki. Hakutaka hata kumtuma Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Alifuta.
Akatangaza siku 3 za kuomboleza.

Hata hivyo waandaaji wa Miss Tanzania waliona hasara kubwa kuahirisha
 
shindano la Urembo usiku huo. Wangepata hasara! Hata wafadhili wao
Kampuni ya simu za mkononi ya vodacom ambao miongoni mwa waliofariki
wamo wateja wa vodacom, waliendelea na shindano hili.

Jumatatu, tarehe 12 Septemba 2011 ni siku ya khitma ya kuwaombea marehemu wetu.
 

Nimeamua kutotumia simu yangu ya Voda kwa siku nzima, sina njia ya
 
kuiadhibu Kampuni hii isipokuwa kugoma kutumia simu yao japo kwa siku
moja kuonyesha kutoridhishwa kwangu na uamuzi wao wa kutojali msiba
huu kwa Taifa.

Misiba huweka jamii pamoja. Msiba huu uliotokea Zanzibar ni jaribio
 
kubwa kwa Umoja wa Taifa letu. Shirika la Utangazaji la Taifa
limeshindwa jaribio hili la kudhihirisha Umoja wetu katika kipindi
hiki. Nataraji wakubwa wa Shirika hili linaloendeshwa kwa kodi
watawajibika au kuwajibishwa!

Jumla ya Majeruhi na marehemu sasa inafikia zaidi ya Abiria 800!
 
Asubuhi ya jana 10 Septemba 2011 tuliambiwa na Serikali kwamba uwezo
wa Boti la MV Spice Islander ilikuwa ni abiria 500 na wafanyakazi 12.
Pia tumejulishwa kuwa boti hili lilikuwa la Mizigo na sio la Abiria.

Natumai mara baada ya kumaliza maombolezo haya ya siku tatu Wakuu wa
 
Mamlaka zinazohusika na usafiri wa Majini wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar watawajibika au kuwajibishwa. Mkuu wa Bandari ya Zanzibar
Mustafa Aboud Jumbe na Waziri wa Miundombinu Hamad Masoud wanapaswa
kufukuzwa kazi mara moja kama hawatawajibika wenyewe kwa kujiuzulu.

Kufukuzwa kwao kazi hakutarudisha ndugu zetu duniani bali itakuwa ni
 
somo kuwa hatutarudia tena kufanya makosa yaliyoleteleza ajali kama
hii.

Mwenyezi Mungu atupe subira wakati huu wa msiba mkubwa katika Taifa
 
letu. Alaze roho za marehemu wetu mahala pema peponi na awape unafuu
wa haraka majeruhi wetu.

Zitto Kabwe, Mb

NAUNGANA NA WATANZANIA WENZANGU KUWAPA POLE WOTE WALIOPATA AJALI NA MELI TOKA UNGUJA-PEMBA

Molla awe pamoja nasi