Search This Blog

Monday, November 15, 2010

JE KUNA SALIO?????????????

"Aisee baba angu. Kumbe salio kidogo hiviiii!! Aisee Spika Makinda hajanipa pesa yangu ya vikao" Mrema

Sunday, November 14, 2010

MCHUMU MCHUMU TENAA MMWAAAAAAAA....

Kazi ipoooooo!!!!!!!!! kwa wapendanao.

50 CENT MFUASI WA FREEMASONS???

Cutris James Jackson III aka 50 Cent msanii mkali toka kwa Obama,amezua utata baada ya kuonekana ametupia kapelo yenye nembo inayofanana na dini ambayo inahusishwa na imani ya kishetani duniani,Fremasons. Nembo ya freemasons ni pembetatu na jicho moja na 50 Cent inasemekana alikua mstari wa mbele kuipinga dini hiyo hivi karibuni...ngoja tuone inakua vp,kama mwana ndio hivo tena au ni swagga tu!!!

Saturday, November 13, 2010

Friday, November 12, 2010

CUF, TLP, UDP na NCCR Mageuzi vyakataa kuungana na CHADEMA bungeni!!!! Kwa nini?? Sababu hizi hapa!!!!!!

Baada ya Chadema, kutangaza kiongozi wao wa kambi ya upinzani bungeni kuwa ni Mhe. Mbowe, vyama vingine vinne vimeamua kuungana na kuwa na kiongozi wao huko bungeni vyama hivyo ni TLP, CUF , UDP NA NCCR MAGEUZI- source TBC1( MUKTASARI WA HABARI). 


Ukiangalia ndoa ya CUF na CCM kule Zanzibar ni vigumu sana kuamini kuwa CUF inaweza kushirikiana na Chadema kwenye kambi ya upinzani. Sikushawishika kwa mara ya kwanza niliposikia kuwa eti CUF na Chadema watashirikiana. Labda kama CUF ni mbili. Lakini ikiwa CUF ni moja siamini kuwa CUF ile ile inaweza kuwa na muungano na  Chadema. 

CUF vile vile kwenye Bunge la Muungano wanajiona kama wamepotea kwani wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party. Wamepoteza nafasi yao ya kuwa main opposition party kwa Chadema si CCM. Kwa hiyo CUF haiwezi kumpenda Chadema. Hata ukiangalia kwenye uchaguzi, inaelekea mikakati ya CUF na CCM ilikuwa inafanana na wameshinda wote maeneo ya pwani. Kwa hiyo baadae ukiangalia vizuri kwenye tafakari yako, CUF wanajiona kuwa hawako tofauti sana na CCM.

Hata kampeni zao unaweza kuona kuwa CUF hawakuwa against CCM kihivyo. 

Jingine ni kuwa CCM wanauona wingi wa Chadema kama TISHIO kwao. Hivyo wako tayari kurefusha mkono kwa chama kingine. NCCR alikuwa ni direct ally wa CCM. Kampeni za Kawe zilithibitisha kuwa NCCR ilikuwa adui wa Chadema kuliko kuipnga CCM. Hili ni la muda kidogo. NCCR kina MPs wanne tu. Kwa hiyo CCM kumvutia CUF upande wake ni kupunguza nguvu ya upinzani kwani wabunge 45 wa Chadema ukijumlisha na 30 wa CUF, upande wa wapinzani ilikuwa inakuja na wabunge 75. Hiyo si nguvu ya kupuuza kwa CCM hivyo kwao itakuwa vizuri Chadema wakibaki peke yao.

Kwa ujumla ni kuwa katika Bunge lijalo UPINZANI itakuwa ni Chadema peke yao. Na hilo litawajenga zaidi. Hawa wengine kina UDP, TLP, NCCR na CUF obviously watahamia kwa CCM. Pepo zote za kisiasa zinaonesha hivyo.

BEAKING NEWS.......MARANDO KURA HAZIKUTOSHA ZA USPIKA

HESHIMIWA ANNE MAKINDA NDIYE SPIKA MPYA WA BUNGE BAADA YA KUMSHINDA MH. MGOMBEA MABERE NYAUCHO MARANDU KATIKA UCHAGUZI WA KUMPATA SPIKA MPYA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
HIVI SASA SPIKA HUYO MPYA ANASIMAMIA ZOEZI LA KUAPA LA WABUNGE WAPYA WA BUNGE HILI, ZOEZI AMBALO LINATARAJIWA KUCHUKUA SIKU 2



Kura zilizopigwa jumla ni 327
Zilizoharibika ni kura 9

Anna...kura 265....SPIKA 74.2%

Marando.....kura 53


Zoezi la upigaji kura za kumchagua Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilienda vizuri huku Anne Makinda (CCM) alimteua mbunge wa Ludewa Mh. Deo Haule Filikunjombe kusimamia kura zake na mgombea wa Chadema Mh. Mabere Marando alimteua Mh. Halima Mdea kwenda kusimamia kura zake.

KWA KAULI HII YA MAKAMBA...BASI KATIBU MKUU WA CCM ANAFAA KUWA MWANAMKE.

Nimevutiwa na hoja ya Mzee Yusuf Makamba kwamba safari hii Kamati Kuu ya CCM iliona ni vyema kupitisha mwanamke kwenye nafasi ya Uspika sababu ni wakati wao na kwa kuwa tangu uhuru hatujawahi kuwa na Spika wa kike.

Kwa maoni yangu ni kuwa chama kama kinawathamini wanawake kingeanzia nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM kwani nayo haijawahi shikwa na mwanamke tangu uhuru  kuliko kukimbilia kwenye uspika ambao chama hakina uhakika wa kushinda moja kwa moja, ''charity begins at home''. Vinginevyo itakuwa siyo KUWAWEZESHA wanawake bali KUWAWEZA.


Hii statement inanikumbusha kauli aliyotoa Chiligati kuhusu kutoswa kwa Seleli kuwa aliachwa sababu hana mvuto, eti sababu alikuwa anatetea nafasi yake hakupaswa kupata idadi ndogo ya kura. Haijachkua muda tumegundua kuwa hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Kikwete naye hana mvuto. Toka ushindi wa 82% (2005) hadi kushindwa kwa 61% (2010) akiwa madarakani. Ama kweli nyani haoni kundule, na wanawake WAKIWEZWA, WANAWEZESHWA!

Mwanamke awe Katibu Mkuu CCM.

NAOMBA KUTOA HOJA

Thursday, November 11, 2010

WABUNGE WAANZA KUTINGA MJENGONI

Mhe. Mr. II akiwa mjengoni. Du amebadirika ghafra wajameni!!!!!!!!

Mhe. Sita na Mhe. Anne Malecela wakisalimiana

Kidume...Dr. Slaa akisalimiana na wabunge Dodoma.

Hebu mcheki Mhe. Vick Kamata mguuni ...ametinga kikuku jamani...mweeeee!!!!! Bunge la mwaka huu ni balaa...Biashara ni matangazo.

Mhe. Halima Mdee na Mhe. Sitta wakisalimiana.

Wednesday, November 10, 2010

MAPINDUZI MAKUBWA CCM HAYA HAPA......SITTA, CHENGE NJE USPIKA

ANNA MAKINDA

ANNA ABDALAH

KATE KAMBA
KAMATI Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi, imepitisha majina matatu ya Anna Abdallah, Anna Makinda na Kate Kamba kuingia katika mchakato wa kusaka atakayeiwakilisha CCM katika kuwania kiti cha Uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumbwaga Samuel Sitta aliyekuwa Spika wa bunge hilo.

Kamati hiyo kuu imefanya maamuzi hayo jana jioni Mjini Dodoma baada ya kupitia majina ya wanachama 13 waliojitokeza ndani ya CCM kusaka kuteuliwa kuwania nafasi hiyo nyeti katika Bunge ambacho ni chombo cha juu cha kutunga sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusufu Makamba alisema wamechukua uamuzi huo wakizingatia kuwa umefikia wakati wanawake waongoze vyombo vya dola.

"Watanzania wote wanafahamu utendaji wa Spika aliyepita hatuna tatizo naye, lakini chama chetu kupitia kamati kuu kimeona umefika wakati wanawake wawezeshwe kwa kupewa muhimili japo mmoja wa dola,"alisema kifupi Makamba.

SITTA USO KWA USO NA CHENGE
SIKU ZOTE WANGEKUWA HIVI.....TUSINGEYASIKIA YA UNAFIKI.


CHADEMA YAMTEUA MARANDO KUGOMBEA USPIKA

Mh. Mabere Nyaucho Marando


HABARI ZILIZOTUFIKIA PUNDE KUTOKA DODOMA ZINASEMA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KIMEMTEUA MWANASIASA MKONGWE MH. MABERE NYAUCHO MARANDO KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

WABUNGE WATEULE VITI MAALUMU WA CCM NA CHADEMA

Tume ya Uchaguzi imetangaza nafasi 104 ya wabunge wa viti maalumu kwa mgawanyo wake wa kuweza kuingazia uwiano wa wingi wa kura za ubunge. Hivyo baada ya kukokotoa uwiano wa viti hivyo CCM imejizolea viti 65, CHADEMA kimepata viti 23 na CUF kimepewa viti 10.

Katika bunge lililopita kulikuwa na Viti maalumu 75 ambapo CCM ilikuwa ina viti 58, CUF viti 11 na CHADEMA viti 6. Viti vingine 6 vimeachwa wazi vikisubiri matokeo ya majimbo 7 ambayo uchaguzi wake haukufanyika.

Yafuatayo ni majina ya wanaopewa nafasi kutajwa kuwa wabunge wateule kutoka CCM na CHADEMA. Chama Cha Wananchi CUF bado hakijapeleka orodha ya majina waliyopendekeza kuchukua nafasi zao 10.

MAJINA YA WABUNGE WATEULE
WA VITI MAALUMU WA CCM NI:

Wabunge 65 wateule wa Viti Maalumu toka CCM waliotajwa ni Sophia Simba, Gaudentia Kabaka, Ummi Mwalimu, Agness Hokororo, Martha Umbulla, Lucy Mayenga, Faida Mohamed Bakari, Felista Bura, Kidawa Hamid Saleh na Stella Manyanya.
Wengine ni Lediana Mng’ong’o, Sarah Msafiri Ally, Catherine Magige, Tauhida Galos Cassian, Asha Mohamed Omari, Rita Mlaki, Anna Abdallah, Fenella Mukangara, Terezya Huvisa na Al-Shaymaa Kwegir.

Wengine ni Maria Hewa, Hilda Ngoye, Josephine Genzabuke, Esther Midimu, Maida Hamad Abdalla, Asha Mshimba Jecha, Zarina Madabida, Namalok Sokoine, Munde Abdallah na Benardetha Mushashu.
Pia wamo Margreth Mkanga, Angellah Kairuki, Zainab Kawawa, Mwanakhamis Said, Riziki Lulida, Devotha Likokola, Christina Ishengoma, Mariam Mfaki, Margreth Sitta na Subira Mgalu.

Wengine ni Vicky Kamata, Pindi Chana, Fatuma Mikidadi, Getrude Rwakatare, Betty Machangu, Diana Chilolo, Fakharia Shomari Khamis, Zaynabu Vulu, Abia Nyabakari na Pudenciana Kikwembe.

Wengine ni Rita Kabati, Martha Mlata, Dk Maua Daftari, Elizabeth Batenga, Azza Hamad, Mary Mwanjelwa, Josephine Chengula, Bahati Abeid, Kiumbwa Mbaraka na Roweete Kasikila, Anastazia Wambura, Mary Chatanda, Rosemary Kirigini, Mariam Kisangi na Kemilembe Lwota
-------------------------------

MAJINA YA WABUNGE WATEULE 23
WA VITI MAALUMU WA CHADEMA NI:

Lucy Owenya, Ester Matiko, Mhonga Ruhwanya, Anna Mallac, Paulina Gekuli na Conchesta Rwamlaza, Suzan Kiwanga, Suzan Lyimo, Grace Kiwelu, Regia Mtema, Christowaja Mkinda, Anna Komu, Mwanamrisho Abama, Joyce Mukya, Leticia Nyerere na Chiku Abwao.

Wengine ni Naomi Kaihula, Grace Kiwelu, Rose Kamili, Christina Lissu Mughiwa, Raya Ibrahim, Philipa Mturano, Miriam Msabaha na Rachel Mashishanga.

Tuesday, November 9, 2010

Wembe ni ule ule!!!!!!!!!!!!!

HALMASHAURI NANE KUONGOZWA NA UPINZANI


Halmashauri nane nchini zitaongozwa na vyama vya upinzani baada ya kupata viti vingi vya udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa wiki iliyopita.
Halmashauri hizo ni Karatu, Manispaa ya Moshi, Kigoma Mjini, Moshi Vijijini, Ukerewe, Jiji la Mwanza, Kasulu na Mbulu.
MWANZA
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kitaliongoza Jiji la Mwanza linaloundwa na majimbo ya Ilemela na Nyamagana kufuatia kushinda kata 11 dhidi ya kata nane zilizochukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uchaguzi katika kata za Mirongo na Mkuyuni uliahirishwa hadi baadaye. Hata hivyo, matokeo yake hayawezi kusababisha athari yoyote kwa kuwa hata kama CCM itashinda itakuwa na viti 10 na isitoshe kata hizo inasemekana ni ngome za Chadema.
KARATU
Katika matokeo ya udiwani Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilishinda halmashauri ya Karatu kwa kupata kata 10 na kata nne kuchukuliwa na Chama Cha mapinduzi (CCM).
UKEREWE
Katika Jimbo la Ukerewe, Chadema imefanikiwa kupata viti 13 kati ya 24 vya udiwani hali inayokiwezesha kuongoza halmashauri hiyo, CCM imepata viti 10 huku CUF ikiwa na kiti kimoja.
KiGOMA MJINI
Chadema imeshinda katika kata 10 wakati CCM imeshinda katika kata tisa.
JIMBO LA MOSHI MJINI
Chadema italiongoza jimbo la Moshi Mjini baada ya kupata kata 17 kati ya kata 21. CCM imepata kata nne.
MOSHI VIJIJINI
Halmashauri ya Moshi Vijijini inayoundwa na majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo, itaongozwa na Chadema kwa kushirikiana na TLP baada ya kupata viti 16 dhidi ya 15 za CCM.
Katika Jimbo la Moshi Vijijini CCM ilipata kata tisa, Chadema kata saba na TLP sifuri wakati katika Jimbo la Vunjo TLP ilipata kata saba, Chadema kata mbili na CCM kata sita.
KASULU
Halmashauri ya Kasulu pia imekwenda kwa upinzani uliopata madiwani 14 dhidi ya madiwani 11 wa CCM. Halmashauri hiyo itaongozwa kwa pamoja kati ya Chadema kilichopata viti madiwani wane na NCCR-Mageuzi kilichopata madiwani 10.
MBULU
Halmashauri ya Mbulu itaongozwa na Chadema baada ya kushinda kata 17 dhidi ya kata 15 zilizochukuliwa na CCM.
ARUSHA
Hata hivyo, katika Jimbo la Arusha Mjini huenda likaongozwa kwa mseto baada ya Chadema kupata madiwani 8, TLP 1 na CCM 10. Kwa kuwa Chadema kilishinda ubunge na mbunge ni sehemu ya madiwani, hivyo chama hicho na TLP vitakuwa na madiwani 10 sawa na CCM hivyo kuongoza kwa mseto.
Hata hivyo, idadi ya madiwani wa viti maalum inaweza kuamua ni chama kipi kiongoze halmashauri hiyo. Chadema kimepata madiwani 8, TLP 1 na CCM 10.

UCHUMI UNAKUA????!!!! EBU CHECK BEI YA MADAFU YETU


KIKOSI CHA KILIMANJARO STARS KWA AJILI YA TASKER CUP HIKI HAPA


Kocha mkuu wa timu ya Taifa,Jan Poulsen akitangaza kikosi ya timu ya Kilimanjaro Stars leo katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka nchini (TFF).Wachezaji waliotajwa na kocha ni Akitangaza kikosi hicho kocha mkuu wa timu ya taifa Jean Paulsen amewataja wachezaji Juma Kaseja wa Simba, Shaban Kado na Said Muhando ambao ni magolikipa.Amewataja wachezaji wengine kuwa ni Shadrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasyika, Haruna Shamte, Idrisa Rajab na Juma Nyoso ambao ni mabeki.
Viungo ni Shaaban Nditi, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Jabir Azizi, Nizar Khalfan, Meshack Abel, Mohamed Banka na Kigi Makasi.Amewataja washabuliaji kuwa ni Danny Mrwanda,Mrisho Ngasa, John Bocco, Thomas Ulimwengu, na Mshabuliaji Gaudence Mwaikimba.Kikosi hicho ndicho kitakacho shiriki katika mashindano ya Cecafa Tusker Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 27 mpaka Desemba 10,2010.katikati ni Meneja wa bia ya Tusker,Nandi Mwiyombella na kushoto ni Afisa Uhusiano wa SBL,Imani Lwinga

MPANGILIO WA SHUGHULI ZA MKUTANO WA KWANZA WA BUNGE

TAREHE 8 - 17 NOVEMBA 2010

JUMATATU
08 Novemba, 2010
Tangazo la Rais Kuitisha Bunge
JUMANNE
09 Novemba, 2010
* Wabunge kuelekea Dodoma
* Kusajili Wabunge Wateule Dodoma
JUMATANO
10 Novemba, 2010
Usajili kuendelea Dodoma - Katibu wa Bunge

ALHAMISI
11 Novemba, 2010
Saa 4.00 Asubuhi
* Mikutano ya Kamati za Vyama vya Siasa
* Kikao cha Briefing UKUMBI WA BUNGE

Saa 10.00 Jioni
Kupokea majina ya wagombea Uspika (Nomination day)

IJUMAA
12 Novemba, 2010

* Mkutano wa Bunge wa Kwanza.
* Kikao cha Kwanza kuanza kwa kusomwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
* Uchaguzi wa Spika.
* Kiapo cha Spika.
* Wimbo wa Taifa na Dua
* Kiapo cha Utii kwa Wabunge Wote.

JUMAMOSI ASUBUHI
13 Novemba, 2010
Wabunge kuendelea Kuapishwa

JUMATATU
15 Novemba, 2010
Wabunge kuendelea Kuapishwa

JUMANNE
16 Novemba, 2010 Asubuhi
Wabunge kuendelea Kuapishwa

Mchana
* Kuthibitisha Jina la Waziri Mkuu
* Waziri Mkuu kutoa Neno la Shukrani
* Uchaguzi wa NAIBU SPIKA

JUMATANO
17 Novemba, 2010
Asubuhi
Waziri Mkuu Kuapishwa IKULU -CHAMWINO

10. Saa 10.00 Jioni
RAIS KULIHUTUBIA BUNGE UKUMBI WA BUNGE

NENO LA SHUKRANI - WAZIRI MKUU

HOJA YA KUAHIRISHA BUNGE

USIKU Tafrija ya Rais kwa Wabunge wote Viwanja vya Bunge

* ENDAPO ITAKUWA SIKUKUU TAREHE 15 AU 16 NOVEMBA, 2010 BUNGE LITASITISHA SHUGHULI ZAKE HADI SIKU INAYOFUATA. OFISI YA BUNGE

Monday, November 8, 2010

CHENGE KUGOMBEA USPIKA!! Aaaaaah!!!

Pichani Mh.Andrew Chenge Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki na Mwanasheria mkuu wa Zamani wa Tanzania akiongea na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Protea Courtyard Upanga SeaView leo ambapo amesema ana nia ya kugombea Uspika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Amesema ameamua kugombea Uspika wa ili aweze kusimamia na kutibu majeraha ambayo yamesababishwa na uongozi uliopita kwa wengine.

Mswali ya kujiuliza ni haya:
1. Chenge ana kesi ya kifisadi Mahakamani, atawezaje kutibu majeraha ya kiutendaji wakati yeye ni mahututi?
2. Chenge ana kesi ya mauaji ya raia kwa kugonga na gari, je atawezaje kuwatetea walioathirika bungeni wakati ameshindwa kuwasaidia ndugu na jamaa wa wale aliwaua?



Saturday, November 6, 2010

MADAI YA DR. SLAA YASIPUUZWE HATA KIDOGO, YANA MSINGI.

Ndugu zangu wazalendo wa nchi hii,

Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini mkubwa mwenendo wa matokeo ya uchaguzi kutoka maeneo mbalimbali hususan kwa nafasi ya urais. Kwa wale wenzangu walioanza kufuatilia mapema kabisa, lazima watakuwa wameshtuka sana na namna "trend" ya matokeo ya urais ilivyobadilika ghafla. Matokeo ya awali kutoka mikoani yalianza kuonyesha tofauti ndogo ya kura kati ya Dr. Slaa na Jakaya Kikwete. Hali hiyo iliendelea kwa kipindi kirefu na kwenye baadhi ya majimbo kama Iringa, Mbeya, Moshi na Arusha Dr. Slaa alikuwa anaongoza kwa mbali kabisa. Baadaye nilishtuka nilipoambiwa kwamba matokeo ya urais yatakuwa yanatangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) na siyo wasimamizi wa uchaguzi kutoka kwenye majimbo. Kama suala la uchaguzi ni la wazi na huru, kwa nini wasimamizi wa uchaguzi wasitangaze tu matokeo ya urais sambamba na matokeo ya ubunge na udiwani. Ni nini kilichozuia????? Uhuru wa kutoa matokeo ulikuwa wapi???? Au wasimamizi wa kwenye majimbo hawakuwa na haki ya kutangaza matokeo ya uraisi????? 

Ndugu zangu ninachokiona hapa, ni kama kuna ujanja ulifanywa,  pia sisi watanzania wazalendo hatutakuwa hata mara moja kukaa kimya na kuridhika na matokeo ya urais yaliyotangazwa na NEC. Ninawaomba sana tena sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati wote nchini wafuatilie mlingano wa matokeo (yaliyoidhinishwa na mawakala wa vyama husika) kutoka kwenye majimbo na matokeo yanayotangazwa na NEC. Sina hakika kama jambo hili linaweza kuruhusiwa lakini ninaona kuwa ni jambo la msingi sana. Lazima wananchi tujiridhishe kwamba kilichotangazwa na NEC kwamba ndiyo jumla ya kura za urais kwa mgombea fulani kutoka jimbo fulani lazima iwe kweli ndiyo jumla ya matokeo ya vituo vyote vya jimbo husika. Ninawaomba sana viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati mlifuatilie jambo hili kwa ukaribu sana kwani inawezekana hapa ndipo ujanja mkubwa uliofanyika ili kuwezesha chama tawala kuendelea kuongoza nchi hii.

Ndugu zangu, ninaandika haya kwa uchungu mkubwa sana baada ya kusoma maoni ya wananchi ninaokutana nao mitaani na hata ninaposoma kwenye mitandao. Ukweli ni kwamba watanzania wengi hivi sasa wameichoka CCM na wanataka mabadiliko. Hali hii imeonekana dhahiri wakati wa mikutano ya Chadema kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini.  Tafadhali viongozi wa Chadema, CUF na wanaharakati tusiwakatishe tamaa wananchi lazima tuthamini na kuenzi harakati za wananchi kutaka mabadiliko. 

HAINGII AKILINI MTU UMPIGIE KURA MBUNGE WA CHADEMA HALAFU KURA YA URAIS UMPE MGOMBEA WA CCM . MTU UNACHAGUA SERA ZA CHAMA SIYO SURA YA MTU. MIFANO:

JIMBO:                        CHAMA:-----------UBUNGE:------RAIS:

ARUSHA MJINI - CHADEMA...................56,208..... .......54,208
                       CCM................... ....36,107..................39,107

MBEYA-MJINI:CHADEMA..................46,411.... ..............42,917
                     CCM............... .........24,236...................32,249

NYAMAGANA: CHADEMA...............38,171....................30,991
                     CCM.....................27,883......................32,320
 ILEMERA :CHADEMA................31,256......... .............29,701
                 CCM......................26,870........................9,143
 MASWA MAGH: CHADEMA......17,456............ ..........11,742
                    CCM..................12,824........................17,104
 MASWA MASH: CHADEMA......17,075.......................12,203
                        CCM.............. 17,014.......................21,150

 Kali zaidi ni hii ya JIMBO LA Musoma mjini: Kutoka KURA 14,723 za Mbunge wa CCM na kuongezwa kufikia KURA 49,858 za KIKWETE.

MUSOMA MJINI CHADEMA......21,335................23,211
CCM.....................................14,723................49,858???
Tutafakari hili.


Hebu angalia hali halisi. Na hili pia halihitaji elimu ya juu kulielewa na kulichambua. Wapiga Kura Waliojiandikisha ni: 20,137,303.
 Na Waliojitokeza Kupiga Kura Ni: 8,626,283 sawa na asilimia 42.84%.
Hii ina maana waliojiandikisha lakini hawajapiga kura ni: 11,511,020 sawa na asilimia 57.16%.
Ni jukumu letu pia kuangalia ni kwa nini wapiga kura wengi hawakujitokeza. Tusaidiane kuangalia sababu hizi nami nitaanza kwa chache ambazo nimezifanyia utafiti kwa kuwauliza wale ambao walijiandikisha lakini hawakuweza kupiga kura:

1. Hawakuona majina yao ingawa walijiandikisha
2. Walikuwa safarini nje ya Wilaya, Mkoa au Nchi
3. Walikuwa sehemu tofauti na waliojiandikisha
4. Walikuwa wagonjwa
5. Kuna ambao wamefariki katika kipindi cha uboreshaji wa daftari na kipindi cha kupiga kura
6. Kuna walioondolewa kwa madai kuwa wamekufa lakini wako hai.
Mie nadhani tayari kulikuwa na mazingira ya kuchakachua kura ndiyo maana idadi ilikuwa kubwa sana. haiwezekani kweli zaidi ya nusu ya wapiga kura wasiende kupiga kura wakati hamasa ilikuwa kubwa sana. Haiwezekani. Kuna namna.
Je, kwa maoni au utafiti wako ni sababu gani nyingine zilizowafanya watu wasijitokeze kupiga kura?



Jambo lingine lililodhihilisha kuwa CCM hawana sera ni pale  Prof. Lipumba kumpa JK ilani ya CUF eti iwasaidie kuchukua mambo! Wao CCM wanayo ya kwao na Lipumba anajua hilo ila Prof kwa ujanja aliitoa ili kuonyesha kuwa CCM hawana sera za maana wajifunze kuweka sera za kunufaisha taifa. That was a smart move. Nadhani pia CCM wanatafuta ya Chadema iweze kuwasaidia kwa siku za usoni.

Friday, November 5, 2010

HAYA NDIYO MATOKEO YA MWISHO YA URAIS YALIYOTANGAZWA NA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI



MATOKEO RASMI YALIYOTANGAZWA LEO
1. KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO: 96, 933 (1.12%)

2. KIKWETE JAKAYA MRISHO/CCM: 5,276,827 (61.17%)

3. SLAA WILLIBROD PETER/CHADEMA: 2,271,941 (26.34%)

4. LIPUMBA IBRAHIM HARUNA/CUF: 695,667 (8.067%)

5. RUNGWE HASHIM SPUNDA/NCCR-MAGEUZI: 26,388 (0.31%)

6. MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT/TLP:17,482 (0.20%) 
7. DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA/UPDP: 13,176 (0.15%)
----------------------------------------------
WALIOJIANDIKISHA KUPIGA KURA: 20, 137, 303
WALIOJITOKEZA KUPIGA KURA: 8, 626 (42.64%)
KULA HALALI ZILIZOPIGWA: 8,398,394
KURA ZILIZOHARIBIKA 227,889 (2.64)

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ( NEC), Jaji Mstaafu, Lewis Makame leo jioni amemtangaza mshindi wa kiti cha urais wa Tanzania wa mwaka 2010 kuwa ni Ndugu Jakaya Kikwete kutoka Chama cha Mapinduzi(CCM).

Matokeo hayo ya uchaguzi huo, yalitangazwa leo majira ya saa kumi jioni na Mwenyekiti huyo katika viwanja wa Karimjee jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Jaji Mstaafu , Makame alisema kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwaka 1977 mgombea wa kiti cha urais atatangazwa kuwa amechaguliwa kuwa rais iwapo tu amepata kura nyingi kuliko mgombea mwingine yeyote.

Aidha Makame alisema kwa mujibu wa ibara ya 47(2) ya Katiba hiyo, mgombea wa kiti cha urais akichaguliwa basin a mgombea mwenza wake atakuwa Makamu wa Rais.

NANI ALAUMIWE??? TUME? AU MPIGA KURA?

Ukiangalia kwa makini hiyo fomu/ karatasi ya kupigia kura utagundua kuwa mpiga kura aliwapigia wagomea watatu (3) badala ya mgombea mmoja. Je ni nani wa kulaumiwa??? Je TUME ya uchaguzi haijafanya kazi ya kushota kuielemisha jamii kuhusu upigaji wa kura??? Je mpiga kura amekiuka maagizo ya upigaji kura? 

Thursday, November 4, 2010

WAKATI WA UCHAGUZI TULIMUENZI MWL. NYERERE?

Pichani anaonekana Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere akiwa amepanga foleni kusubiri kupiga kura  yake wakati wa chaguzi mbalimbali zilizokuwa zinafanyika nchini enzi za uhai wake. Ninachojiuliza ni hivi???? Mbona viongozi wetu siku hizi hawapangi foleni??????????  Au huwa wamechoka????????? Au ni kutokuona umuhimu wa kujali utu wawatu au  mtu mwingine??????
Katika uchaguzi wa mwaka huu sikuweza kuona Kiongozi yeyote wa ngazi ya juu wa Serikali na Chama akiwa amepanga foleni kusubiri kupiga kura badala yake walikuwa wanakuja na Msafara wa watu kibao. Je ni kwa vipi tulimuenzi Mwl. Nyerere wakati wa kupiga kura? Nawauliza nyie viongozi!!!!!!!!!

Swali jingine la nyongeza...Naomba kwa wale walio na kumbukumbu mnipe majina ya hao wengine waliopo kwenye foleni na baba wa Taifa tafadhali.... hasa huyo mwenye kofia hapo mbele na hao wawili walio nyuma ya Mwalimu.

MISS TZ AREJEA KUTOKA CHINA


Kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Kamati ya Miss Tanzania Bw. Albert Makoye, pamoja na Mrembo wa Chuo Kikuu Kikuu Huria Christina Justine, na Miss Shinyanga 2010 Buduri Ibrahim kwa pamoja wakiwapokea Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel na mshindi wa pili Glory Mwanga kushoto kwa Genevieve, na Miss Temeke mshindi wa pili Anna Daudi ambao waliwasili jana kwenye uwanja wa ndege wa Mwlimu J.K.Nyerere wakitokea Sanya China katika mashindano ya urembo ya dunia.
Mrembo Anna Daudi na Glory Mwanga walikwenda Sanya China kumpa sapoti Miss Tanzania 2010. pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw. Hashimu Lundenga, Katibu Mkuu Bosco Majaliwa, na mama wa Miss Tanzania 2010 Mrs. Mary Emmanuel Mpangala.

Dr. Slaa na "The dream team" mjengoni


Kikosi ambacho tayari kimeshajihakikishia namba mjengoni.

SAMWEL SITTA ACHUKUA FOMU KUWANIA U-SPIKA WA BUNGE


Spika anayemaliza muda wake Mhe. Samuel Sitta  amechukua fomu ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge katika Bunge la Kumi kwenye uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mapema wiki ijayo mjini Dodoma.

Spika Sitta amechukua fomu hiyo kupitia chama chake cha CCM katika ofisi ndogo za CCm Lumumba, Dar es Salaam na kuijaza kisha kuirudisha jana baada ya kukamilisha mahitaji yote ikiwa ni pamoja na kugharamia fomu hiyo kwa kiasi cha Tsh 500,000/= kwa mujibu wa taratibu wa chama hicho.

kwa Mujibu wa ibara ya 84 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977, chama chochote cha siasa kilichosajiliwa kina haki ya kushiriki katika Uchaguzi wa Spika kwa kumpendekeza mwananchama wake mmoja ambaye ni Mbunge au asiye Mbunge mwenye sifa za kuwa Mbunge kuwa Mgombea wa nafasi hiyo.
Wagombea wengine waliojitokeza kugombea kiti hicho ni pamoja na Mbunge metule wa Same Mashariki, Anne Kilango-Malecela, Mbunge Mteule wa Njombe Kusini, Anna Makinda na Mwalimu wa Shule ya Sekondari Tambaza, Bw. Salim Kungulilo.

WABUNGE WATEULE WALIOTANGAZWA HADI SASA

(inaendelea kubadilika kadiri matokeo
yanavyotolewa na Wasimamizi wa vituo).
1.Ubunge Babati Vijijini - Jitu Soni/CCM

2. Ubunge Kilombero - Regia Mtema/CHADEMA

3. Ubunge Mkuranga - Adam Kighoma Malima/CCM

4. Ubunge Singida Kaskazini - Lazaro Samwel Nyalandu/CCM

5. Ubunge Sikonge - Said Nkumba/CCM

6. Ubunge Bukene - Selemani Jumanne Zedi/CCM

7. Ubunge Igalula - Athuman Rashid Futakamba/CCM
Ubunge Tabora Kaskazini - CCM

8. Ubunge Ukonga - Eugene Elishiringa Mwaiposa/CCM
9. Ubunge Segerea - Dk. Milton Makongoro Mahanga/CCM

10. Ubunge Igunga - Rostam Aziz/CCM
11. Ubunge Liwale - Faith Mohammed Mitambo/CCM
12. Ubunge Njombe Mjini - Anna Makinda/CCM

13. Ubunge Ileje - Nikusama Kibona/CCM
14. Ubunge Kigoma Kusini - David Kafulila/NCCR Mageuzi

15. Ubunge Kilwa Kusini - Bungaro Said/CUF

16. Ubunge Muhambwe - Felix Mkosamali/NCCR Mageuzi
17. Ubunge Kilwa Kaskazini - Mustapha Mangungu/CCM
18. Ubunge Bagamoyo - Dk. Shukuru Kawambwa/CCM

19. Ubunge Bariadi Mashariki - John Momose Cheyo/UDP
20. Ubunge Bariadi Magharibi - Andrew John Chenge/CCM

21. Ubunge Bukombe - Prof. Kayigela Kahigi/CHADEMA
22. Ubunge Kalenga - William Mgimwa/CCM
23. Ubunge Mbozi Mashariki - Godfrey Zambi/CCM
24. Ubunge Korogwe Vijijini - Steven Ngonyani/CCM

25. Ubunge Pangani - Salim Pamba/CCM

26. Ubunge Same Magharibi - Dk. Mathayo David/CCM
27. Ubunge Mtera - Livingstone Lusinde/CCM

28. Ubunge Nzega Mjini - Dk. (Medical Doctor) Hamisi Andrea Kigwangalla/CCM

29. Ubunge Kigamboni - Dk. (Medical Doctor) Faustine Ndugulile/CCM

30. Ubunge Muleba Kaskazini - Charles Mwijage/CCM

31. Ubunge Kawe - Halima James Mdee/CHADEMA

32. Ubunge Muleba Kusini - Prof. Anna Kajumulo-Tibaijuka/CCM

33. Ubunge Same Mashariki - Anne Kilango-Malecela/CCM

34. Ubunge Mufindi Kusini - Menrad Lutengano Kigola/CCM
35. Ubunge Mufindi Kaskazini - Mahmoud Hassan Mgimwa/CCM
36. Ubunge Kondoa Kaskazini - Zabein Muhita/CCM
37. Ubunge Bahi (ipo Dodoma) - Omary Badwel/CCM

38. Ubunge Monduli - Edward Lowassa/CCM

39. Ubunge Hanang - Mary Nagu/CCM

40. Ubunge Singida Mashariki - Tundu Lissu/CHADEMA

41. Ubunge Misungwi - Mawematatu Charles Kitwanga/CCM

42. Ubunge Kwimba - Masoor Sharif/CCM

43. Ubunge Mbulu - Mustapha Quorro Akonaay/CHADEMA

44. Ubunge Karatu - Israel Yohana/CHADEMA

45. Ubunge Ubungo - John Mnyika/CHADEMA

46. Ubunge Manyovu (awali liliitwa Kasulu Magharibi) - Albert F. Ntaliba/CCM

47. Ubunge Rorya - Lameck Airo/CCM

48. Ubunge Sumbawanga Mjini - Aeshi Khalfan Hilal/CCM

49. Ubunge Tanga - Omar Noor Rashid/CCM

50. Ubunge Busanda (wilaya ya mkoa mpya wa Geita) - Bi. Lawrencia Bukwimba/CCM
51. Ubunge Mbozi Magharibi - Silinde David/CHADEMA

52. Ubunge Kibondo - CHADEMA

53. Ubunge Geita (wilaya ya mkoa mpya wa Geita) - Max Donald/CCM

54. Ubunge Nyang'hwale (wilaya ya mkoa mpya wa Geita) - Hussein Nassoro Mamari/CCM

55. Ubunge Ruangwa - Kassim Majaliwa/CCM

56. Ubunge Lulindi - Jerome Bwanaus/CCM

57. Ubunge Serengeti - Kebwe Stephen Kebwe/CCM

58. Ubunge Mwibara - Alfax Lugora/CCM

59. Ubunge Masasi - Mariam Kasembe/CCM

60. Ubunge Makete - Dk. Binilith Mahenge/CCM

61. Ubunge Ukerewe - Salvatory Naluyaga Machemuli/CHADEMA

62. Ubunge Manyoni - John Chiligati/CCM
63. Ubunge Bunda - Stephen Wassira/CCM
64. Ubunge Kasulu Vijijini - Agripina Z. Buyogela/NCCR-Mageuzi

65. Ubunge Morogoro Kusini Mashariki - Lucy Nkya/CCM
66. Ubunge Bukoba Mjini - Khamis Kagasheki/CCM

67. Ubunge Njombe Kaskazini - Deo Sanga/CCM

68. Ubunge Njombe Magharibi - Gerson Hosea Lwenge/CCM

69. Ubunge Morogoro Kusini - Innocent Karogoresi /CCM
70. Ubunge Dodoma Mjini - David Malole/CCM
71. Ubunge Urambo Mashariki - Samwel Sitta/CCM
72. Ubunge Kyela - Harrison Mwakyembe/CCM
73. Ubunge Morogoro Mjini - Aziz Abood/CCM

74. Ubunge Arumeru Magharibi - Ole Sambu/CHADEMA
75. Ubunge Manyoni Mashariki - Lwanji/CCM

76. Ubunge Mkinga - CCM
77. Ubunge Kilosa - Mustapha Mkullo/CCM

78. Ubunge Namtumbo - Vita Kawawa/CCM

79. Ubunge Longido - Michael Lekule Laizer/CCM
80. Ubunge Kibaha - CCM

81. Ubunge Kisarawe - CCM

82. Ubunge Sumbawanga Mjini - CCM

83. Ubunge Moshi Vijijini - Cyril Chami/CCM

84. Ubunge Vunjo (ipo Kilimanjaro) - Augustine Lyatonga Mrema/TLP

85. Ubunge Mtwara Mjini - Murji Hasinen Mohamed/CCM
86. Ubunge Lindi - Salum Barwani/CUF
87. Ubunge Tabora Mjini - Ismal Aden Rage/CCM

88. Ubunge Arumeru Mashariki - Jeremia Sumari/CCM
89. Ubunge Mwanga - Jumanne Maghembe/CCM

90. Ubunge Siha (ipo Kilimanjaro) - Aggrey Mwanri/CCM
91. Ubunge Mbeya Mjini - Joseph Mbilinyi (Mr. II aka Sugu)/CHADEMA

92. Ubunge Chato (awali liliitwa Biharamulo Mashariki) - John Magufuli/CCM
93. Ubunge Moshi Mjini - Philemon Ndesamburo Kiwelu/CHADEMA

94. Ubunge Songea - Dk. Emmanuel Nchimbi/CCM

95. Ubunge Bukoba Vijijini - Jasson Rweikiza/CCM

96. Ubunge Biharamulo Magharibi - Dk. Antony Mbasa/CHADEMA
97. Ubunge Kasulu Mjini - Machali Moses John/NCCR Mageuzi

98. Ubunge Mvomero - Amos Makalla/CCM

99. Ubunge Kigoma Mjini - Peter Serukamba/CCM

100. Ubunge Rombo - Joseph Selasini/CHADEMA

101. Ubunge Tarime - Nyambari Nyangweni/CCM
102. Ubunge Nyamagana - Hezekiah Wenje/CHADEMA

103. Ubunge Babati Mjini - Chambiri Werema/CCM

104. Ubunge Iringa Mjini - Mchungaji Peter Msigwa/CHADEMA

105. Ubunge Hai - Freeman Mbowe/CHADEMA
106. Ubunge Singida Mjini - Mohamed Dewji/CCM

107. Ubunge Musoma Mjini - Vincent Nyerere/CHADEMA
108. Ubunge Peramiho - Jenista Mhagama/CCM
109. Ubunge Mpwapwa - George Tau/CCM

110. Ubunge Arusha Mjini - Godbless Lema/CHADEMA

111. Ubunge Mbarali - Dickson Kiruvi/CCM

112. Ubunge Kigoma Kaskazini - Zitto Kabwe/CHADEMA
113. Ubunge Korogwe Mjini - Yusuf Nassir/CCM

114. Ubunge Ilemela - Hayness Samson/CHADEMA

116. Ubunge Kongwa - Job Ndugai/CCM
117. Ubunge Mtwara Vijijini - Hawa Ghasia/CCM
118. Ubunge Maswa Magharibi - John Shibuda/CHADEMA
119. Ubunge Tandahimba - Juma Njwayo/CCM
120. Ubunge Meatu - Meshack Opulukwa/CHADEMA
121. Ubunge Kibakwe - CCM
122. Ubunge Maswa Mashariki - Sylvester Kasulimbayi Mhoja/CHADEMA
123. Ubunge Urambo Magharibi - Prof. Juma Kapuya/CCM
124. Ubunge Bumbuli - January Makamba/CCM

Jumla ya majimbo ya Uchaguzi Tanzania 2010 ni 239.