Search This Blog

Sunday, October 17, 2010

HII NAYO KALI KINOMA

SEMA " a, e, i, o, u"  ........       " a, i, o, e, uuuu"

SEMA "aaaa!!!"..........."aaaaa!"

HAYA BASI....1 +3 sawasawa na ngapi?    ........... Sawasawa na "aaaaaa"


Hii ni kwa kuwa anayefundishwa au kuelekezwa inaonekana hafuatilii kabisa!!!!!!!! Hii ndiyo elimu bora!? Angalia tofauti zilizopo ndo utangundua jamii imejiandaaje na kuinua kiwango cha maendeleo katika nchi hii ya Tanzania.

YANGA YAIDUNDA SIMBA CCM KIRUMBA





















YANGA jana iliendelea kuinyanyasa Simba msimu huu baada ya kuichapa bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.

Simba inafungwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuchapwa mabao 3-1 kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya Ngao ya Hisani iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Jerryson Tegete ndiye alipeleka msiba kwa mabingwa hao watetezi, Simba, baada ya kufunga bao hilo katika dakika ya 70 baada ya kuwatoka mabeki wa Simba na kumchambua kipa Juma Kaseja wa Simba kabla ya kuujaza mpira wavuni. 


Katika kipindi cha kwanza cha mechi ya jana, Simba walianza mpira kwa kasi na kufanya shambulizi zito katika dakika ya tatu ambapo Emmanuel Okwi akiwa na kipa Yew Berko alishindwa kufunga baada ya kipa huyo wa Ghana kuucheza mpira na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Baada ya kosakosa hizo za Simba, Yanga walitulia na kuanza kupanga mashambulizi langoni mwa Simba, hata hivyo, washambuliaji wake hawakuwa makini kuweka mpira kimiani.


Simba walianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanya shambulizi lililozaa kona lakini haikuzaa matunda.

Na katika kipindi hicho ndipo mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Yanga, Kostadin Papic kwa kuwatoa Abdi Kassim na Athumani Iddi ‘Chuji’ na kuwaingiza Geofrey Bonny na Yahaya Tumbo yalipozaa matunda kwani yalionekana kuamsha ari na Yanga kufanya mashambulizi mfululizo langoni mwa Simba.

Akizungumzia mechi hiyo, kocha wa Simba Patrick Phiri alisema amekubali matokeo na kwamba wachezaji wake wangeweza kushinda kama wangetumia vizuri nafasi walizopata katika kipindi cha kwanza, kwa vile ndio walicheza vizuri zaidi.

“Lakini katika kipindi cha pili wachezaji wangu walionekana kushindwa kucheza hasa katika dakika za mwisho na hapo ndipo Yanga walipotumia makosa hayo kupata bao lililowapa ushindi,” alisema na kuongeza kuwa hana wasiwasi na mwamuzi Ramadhani Kidiwa kwani alichezesha vizuri.

Naye kocha wa Yanga, Papic alisema ameridhishwa na matokeo na kukiri kwamba Simba waliwazidi katika kipindi cha kwanza lakini aliwapa maelekezo wachezaji wake walipokuwa mapumziko na kubadilika kipindi cha pili kilichozaa bao la ushindi. Kwa ushindi huo, Yanga inaongoza ligi kwa pointi 19 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 16.

Katika mechi hiyo, Simba ndio walikuwa wa kwanza kuingia uwanjani ambapo waliingia saa 8:48 mchana wakifuatiwa na Yanga walioingia saa 9:30.

Timu zilipangwa kama ifuatavyo; Simba: Juma Kaseja, Haruna Shamte, Amir Maftah, Juma Nyoso, Joseph Owino, Jerry Santo, Rashid Gumbo, Hilary Echesa, Emmanuel Okwi, Patrick Ochan, Amir Kiemba.

Yanga: Yew Berko, Shadrack Nsajigwa, Stephen Mwasika, Isaack Boakye, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Ernest Boakye, Athumani Iddi ‘Chuji’/ Yahaya Tumbo, Abdi Kassim ‘Babi’/ Geofrey Bonny, Jerryson Tegete, Nsa Job, Nurdin Bakari.



NI WAKATI WA KUFANYA UAMUZI SAHIHI

Ewe mwananchi wa Tanzania.
Makala zimeandikwa, Katuni zimechorwa, Picha zimepigwa, nyimbo zimeimbwa, hotuba zimetolewa. Hakika ni wakati wako sasa kufanya uamuzi sahihi.

"Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 ni baina ya 
UADILIFU na UFISADI, baina ya UMAKINI na USANII, baina ya HAKI na DHULUMA!!"
TUWE MAKINI KUCHAGUA KIONGOZI SHUPAVU.

HAYA NDIYO MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA

ELIMU BORA SHULE ZA AWALI
ELIMU BORA SHULE ZA MSINGI NA IDADI IMEONGEZEKA SANA
SHULE ZA SEKONDARI KUNA MAABARA NA VIFAA VYOTE MUHIMU
WANAOMALIZA VYUO VIKUU AJIRA KEDEKEDE TOKA SERIKALINI
SHULE BORA
NYUMBA BORA  ZA WANANCHI MAANA KIPATO KIMEONGEZEKA
WANANCHI KUWA NA UWEZO WA KUMUDU MAHITAJI YAO MUHIMU
Zzzzzzzzzzzzzz!!!!! hivi anaota au ndo.......MPYA?



JAMANI WATANZANIA WENZANGU.............
GHARAMA YA KURA  KATIKA UCHANGUZI UJAO 2010, IZINGATIE KULETA MABADIRIKO YA KWELI NA APEWE  MTU ALIYE MAKINI ANGALAU KULETA MABADIRIKO YA KIUCHUMI NA KUWA NA MAISHA BORA YA UKWELI KULIKO HALI HII ILIYODUMU KATIKA JAMII KWA MIAKA ZAIDI YA 50. INAUMA SANA KUONA MAISHA HAYA YAPO KATIKA JAMII AMBAYO INA RASILIMALI ZA KUTOSHA. HATA MALENGO YA MILENIA YAMETUSHINDA KUYATEKELEZA, IMEBAKI NI BLAA BLAA TU.


NAWAKILISHA.






Saturday, October 16, 2010

DR. SLAA AZIDI KUITEKA JAMII

Mgombea urais kupitia chama cha Demokrasi na maendeleo (CHADEMA) Dk.Willibrod Slaa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Chato ,katika mwendelezo wake wa mikutano ya lala salama kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba 31 mwaka huu 2010. 

Wednesday, October 13, 2010

NAMNA GANI TUNAMUENZI BABA WA TAIFA?? 14/10/2010

            


















HAKUJALI KUCHAFUKA NA TOPE.                           MKEKA WA NINI SHAMBANI?
NI KIONGOZI GANI KATIKA AWAMU ZILIZOPITA HADI SASA AMEWEZA  KUENZI KWA VITENDO ALIYOYAFANYA MWALIMU NYERERE???? 
Tukumbuke mazuri aliyoyafanya Mwl. Julius K. Nyerere ili kuhamasisha jamii kushiriki kwa vitendo shughuli mbalimbali za kuinua uchumi wa Taifa letu.

NAWAKILISHA.

TZ BARA KAMPENI CHAFU HADI LINI?????????

Ebu ona wenzetu wa Zanzibar. Mabango yote yapo powaaaaaaa!!!!!!!!!! NO MCHANIKO.
Congratulations!!!!! People of Zanzibar.




CHECK UPANDE WA TANZANIA BARA SASA..........................

Je Huu Ni Uungwana ????????  Kuchana mabango ya wagombea????

Je Hili nalo Je????
Mbona halijachanwa? Au ndo Maisha bora kwa kila MTZ !!??



HII NAYO KALI KINOMA

NJIA RAHISI YA KUPUNGUZA UFISADI HII HAPA.


  • Ufisadi - tatizo sugu na hatari linalodidimiza maendeleo ya Afrika kumbe linaweza kupunguzwa kwa kutumia njia rahisi tu. Utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia unaonyesha kwambaserikali zenye wanawake wengi madarakani (mf. Wabunge, Mawaziri) zina viwango vidogo vya ufisadi ukilinganisha na zile zilizosheheni wanaumeRwanda - nchi ambayo inaongoza duniani kwa kuwa na wanawake wengi bungeni na serikalini inatajwa sana kuwa mfano wa kuvutia kuhusu suala hili. Ni kwa sababu hii kujitokeza kwa wanawake wengi kugombea ubunge na uwakilishi kule Haiti katika uchaguzi wa mwaka huu kumeleta matumaini makubwa kwamba pengine ufisadi utapungua.
  • Tafiti mbalimbali zimeonyesha kwamba wanawake wana huruma kuliko wanaume, wana moyo wa kujinyima, wanaaminika zaidi na ni wepesi wa kuona na kukiri makosa na hatimaye kuomba msamaha. Pengine ni kutokana na sababu hizi wanawake pia wana uwezekano mdogo wa kuiba mamilioni ya pesa za umma na kuwaacha wananchi wanyonge wakiteseka (wengi wao wanawake wenzao; na watoto). 
  • Serikali zenye wanawake wengi madarakani pia zina uwezekano mkubwa zaidi wa kuendeleza sera imara zenye kumakinikia sekta za afya na elimu ya watoto, usawa kwa wanajamii wote na kuendeleza uchumi imara.

KABLA YA MECHI YA SIMBA NA YANGA- FM ACADEMIA KUWASHA MOTO

UTAMBULISHO WA ALBUM MPYA VUTA NIKUVUTE KWA WAKAZI WA MWANZA SIKU MOJA KABLA YA KIPUTE CHA WATANI WA JADI SIMBA NA YANGA, FM KUANGUSHA KAZI IJUMAA HII.

ATM NAKO KUNA VIJIMAMBO!!!!!!!!!

Mshikaji umepata dharura baada ya mishemishe kibao town, then unaamua kwenda kwenye ATM angalau kuvuta kiasi uweze kujikimu. Eeeeh!!!!!!Kuingia tu unakutana na maneno hayo hapo juu. Duuuu! ni kasheshe hasa kama ishu yenyewe imesababishwa na kukuwepa umande ndo hivyo tena na ka-muda nako kamebaki kiduuuuchu! Mwana waneeee weeeeee

KUKUMBATIANA NI DAWA!!!!!!!!

Inasemekana kukumbatiana na rafiki,ndugu,jamaa,mpenzi kwa angalau sekunde 20 kila siku kuna manufaa kiafya.Kitendo cha kuunganisha mwili wako na mtu mwingine kwa upendo inasaidia kuondoa stress kwa wakati huo haimaanishi ndio tiba ya stress.

Haya tukumbatiena kwa afya ya akili.

JAYDEE KUWA BALOZI KWA WANAWAKE WENYE FISTULA


Namba zinazoonekana kwa nyuma ndio namba ambazo unatakiwa kupiga endapo umepata kujua kuna mgonjwa wa Fistula mahala na hana uwezo wa kifedha kufika hospitali, au kama huna pesa kwenye simu unaweza kutuma sms ya tafadhali nipigie kupitia namba hizo.
CCBRT watawasiliana na wewe na kufanya taratibu zote za kufikisha mgonjwa/ wagonjwa hospitalini kwao kwa gharama za hospitali...Kwakuwa wanatoa matibabu bure

..........................................................................................................................

KAMA MWANAMUZIKI WA TANZANIA, NASHUKURU KUWA JAMII YA WATANZANIA WENZANGU WANAPOKEA VIZURI KAZI YANGU YA SANAA YA MUZIKI.

KWA JINSI HIYO BASI……, NA MIMI NINALO JUKUMU LA KURUDI KWA JAMII YANGU NA KUSHIRIKIANA NAO KATIKA HARAKATI ZA KUJIKWAMUA KUTOKA KATIKA MATATIZO MBALIMBALI KAMA VILE MAGONJWA NA UMASIKINI.

NINAYO FURAHA KUWAFAHAMISHA KUWA, MIMI KAMA MSANII NINAE ANGALIWA NA KUSIKILIZWA NA JAMII YA WATU WENGI PANDE MBALI MBALI ZA TANZANIA.

LEO HII NIMEUNGANA NA HOSPITALI YA CCBRT KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

UAMUZI HUU UMEKUJA BAADA YA CCBRT KUNIALIKA KUTEMBELEA WODI MBALIMBALI ZA WAGONJWA ZILIZOPO HOPITALINI HAPA.

LAKINI BINAFSI NILIGUSWA ZAIDI NA WANAWAKE WANAOSUMBULIWA NA UGONJWA WA FISTULA, UKIZINGATIA PIA MIMI NI MWANAMKE NIKAKUBALI KUUNGANA NA CCBRT ILI KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUOKOA MAISHA YA WANAWAKE WALIO WENGI..

TANGU NIZALIWE MPAKA NAKUWA MKUBWA NA KUFIKIA HATUA NILIOPO HIVI SASA, NAKIRI SIKUWAHI KUSIKIA WALA KUONA MGONJWA WA FISTULA. MPAKA NILIPOTEMBELEA HOSPITALI YA CCBRT

NIMESIKITISHWA ZAIDI BAADA YA KUELEZWA KUWA WANAWAKE WENGI WENYE UGONJWA HUU HUSHINDWA KUFANYA KAZI WAKATI MWINGINE HATA KUTENGWA AU KUJITENGA NA JAMII ZAO WANAMOISHI KUTOKANA NA KUWA WANAVUJA HAJA NDOGO AU HAJA KUBWA KILA MARA BILA WAO WENYEWE KUPENDA WALA KUJIJUA. KWAKUWA WANAKUWA WANASHINDWA KUJIZUIA.

HIVYO KUPELEKEA WANAWAKE HAO WENYE FISTULA KUENDELEA KUISHI MAISHA DUNI YA UPWEKE NA KUENDELEA KUWA MASKINI


LABDA NIONGELEE KWA KIFUPI KUHUSIANA NA FISTULA.

NI UGONJWA UNAOWAPATA WASICHANA NA WANAWAKE WAKATI WA KUJIFUNGUA NA HII HUTOKANA NA KUSHINDWA KUFIKA VITUO VYA AFYA VYENYE HUDUMA YA UZAZI.

FISTULA NI UGONJWA UNAOZUILIKA NA UNATIBIKA.

HAKUNA MWANAMKE ANAETAKIWA KUISHI NA FISTULA HASA UKIZINGATIA CCBRT INATOA MATIBABU, USAIFIRI, CHAKULA NA MALAZI BURE KWA WAGONJWA WOTE WANAOSUMBULIWA NA FISTULA.

JUKUMU LANGU KUBWA KATIKA UBALOZI HUU NI KUSIMAMA NA KUTUMIA SAUTI YANGU, NA NAFASI NILIONAYO KATIKA JAMII KAMA MWANAMUZIKI KUTOA WITO KWA WAGONJWA WENYE FISTULA NA HATA WALE WANAJAMII WENGINE WOTE WANAOFAHAMU WAGONJWA HAO, WAJE CCBRT KUPATA MATIBABU NA HUDUMA ZOTE BURE.

NITAFANYA HAYO POPOTE NITAKAPOPATA NAFASI YA KUONGEA NA JAMII INAYONIZUNGUKA, AMA IWE KATIKA MAONYESHO YANGU AU MAHOJIANO NA VYOMBO VYA HABARI.

NITAFANYA HIVYO PIA KATIKA MITANDAO YA KIJAMIII, NINAYOHUSIKA NAYO KAMA BLOGS NA FACEBOOK NA HATA KATIKA MATANGAZO YA TV, RADIO NA VIPEPERUSHI.

ILIMRADI TU UJUMBE UWAFIKIE WANAWAKE WENYE FISTULA WAJE KUTIBIWA BURE CCBRT.

NDUGU ZANGU WAANDISHI WA HABARI, NAOMBA MJIUNGE NAMI KUWA SHUJAA WA WANAWAKE WENYE FISTULA

ASANTENI SANA

LADY JAYDEE a.k.a KOMANDOO

Monday, October 11, 2010

KIDUME NI NANI??????? KUDAAADEKI

Kuna wengine wakishwa kunywa bia ya 4 tu maneno kibaaaaoooo!!!! Mara mchongo huu mara michongo miiiingi kichizi isiyokuwa na tija kwa jamii. Hebu checkshia babaake Dogo anakamua ile mbaya. Hapo anamalizia bia ya 30 tu na ameagiza kreti ingine akomae nayo. Weweeeeee!!!!!

KWA KUMBUKUMBU ZAKO

UNAUKUMBUKA HUU MTI?????
Enzi za utawala wa Kijerumani mti huu uliopo katikati ya jiji la Mwanza ulitumika kwa kuwanyonga wananchi wa Tanganyika enzi hizo pale walipokutana na hatia.
Mamlaka ya Jiji la Mwanza umeuhifadhi kwa ajili ya kumbukumbu hiyo.
Kwa sasa mti huu unaonekana hivi. Umepakwa rangi ili kuweka hiyo kumbukumbu ya mti huo wa kihistoria vizuri zaidi.


BREAKING NEWS

Shirikisho La Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemsimamisha kazi afisa habari wake, Florian Kaijage (pichani) kutokana na fedheha ya kushindwa kutimiza itifaki muhimu ya kupiga nyimbo za taifa wakati wa mechi ya Taifa Stars na Morocco jumamosi jijini.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga amewaambia waandishi wa habari jijini leo kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete, mashabiki na wageni wengine na mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka kote duniani.

Amesema TFF imemua kumwajibisha Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo. Aidha alisema wakati amesimamishwa kaijage ataisaidia timu itakayoundwa kuchunguza jambo hilo na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa yeyote Yule atakayebainika kuhusika kwa tukio hilo.

Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mchezo na Brazil ambapo safari hii wahusika walipewa jukumu la kuhakikisha kuwa wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.

“Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya tff kuomba radhi kwa Mheshiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco” alisema tenga.

Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za police/jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.

JAMANI HIVI NI VIJIMAMBO TU

Kitu zaidi hatari kwao ni nini????? Wote 8 hawajavaa HELMET. Trafic mpoo?
Wewe twanga tu mimi iko sikia maneno yako!!!!! Mmmmmmh
The use of  locally available  materials. Are they environmental friendly???
Jamani tusiogope gharama kufunga ndoa. Kuna namna ya kupunguza gharama.
Wanameremetaaaaa!!!! Wanameremeta!!!!!!!!!!!!
Hey hey!!!!! Jamani huyu mdau anahitaji mapoudaaaaa??!!!
My heart will go on...........
......nakuambia rudisha kitambulisho changu cha kupigia kura.....
Alambaaa  Alambaaa!! Aaaaaam!! Aaaaam!
Nibebe!!!  Nibebe!! Nibembeleze Nibeeeeebe ..
Utaipenda










Sunday, October 10, 2010

TAIFA STARS YAPIGWA 1-0 NA MOROCCO.

Rais Kikwete akiwasalimia washaabiki wakati akienda kukagua vikosi vya taifa Stars na Morocco jijini DSM. Moroco walishinda 1-0.
Kikosi cha Taifa Stars kilichoanza na Morocco
Kikosi cha Morocco
Nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa (kushoto) akisalimiana na mwenzake wa Morocco, Kharja Houssine kabla ya gemu kuanza jijini DSM
Mshambuliaji wa Stars, Danny Mrwanda anayechezea soka la kulipwa huko Vietnam (katikati) akiwa amebanwa na wachezaji wa timu ya Morocco, Kharja Houssine (kulia) na Soulaimani Rachid. 
Hekaheka langoni mwa Morocco
Mshambuliaji wa Morocco, Chamakh Marouane ambaye anaichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza akiipangua ngome ya Stars wakati wa mchezo wa kufuzu Fainali za Afrika uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Taifa stars walipewa support na washahabiki ili washinde mechi hiyo muhimu lakini ngoma ikawa ngumu. 
Checkshia babaakeee!!!!!!!!! Lakini tulitoka vichwa chini.